Nakumbuka wakati niko mdogo, mimi nyumban ndo first born....nilipita kipindi kigumu sana katika ukuaji, hasa nilikua naona waziwazi jinsi ambavyo wadogo zangu mapacha walivyokua wanapenda. Hawa mapacha ni wakike na wakiume, bwana hwa jamaa darasani walikua wazima..hivyo niliona ambavyo mama anampenda mdogo wangu wa kiume na baba alikua anampenda mdogo wangu wa kike. Iliniumiza na kuninyima raha, kuna siku tulikaa kibarazani, sijui ilikuaje tukawa tupo watatu mimi, mama na baba. Ndipo nikawaambia wazazi wangu kiukweli nyie mi hamnipendi mnawapenda hawa wenzangu, ila mama akapinga na akasema hapana si kweli.
Mimi kutokupendwa kwangu kulitokana na sababu nyingi, kama ugomvi aseeh wiki haipiti sijaleta kesi nyumbani, hizi ngumi nimepigana sana.
Kingine darasanai sikua nafanya vizuri kama watoto wengine, hasa huyu wakiume ndo alikua anakua wakwanza mara nyingi, huyu wa kike labda watatu hivi. Ila namba zangu mi huko 20 na kitu.
Kiukweli kutokuoneshwa sipendwi kulinikomaza kiakili, na nikaanza kupambana na kuwa mtu ambaye nataka kuwaonesha ndani yangu kuna kitu.
Kwasasa nyumban mi ndo napendwa hasahasa mama yangu, ananipenda sana na hilo nalijua na nampenda sana mama kuliko maelezo.
Nawasilisha.