Hivi unaanzaje kuwashtaki Qnet?

Hivi unaanzaje kuwashtaki Qnet?

Mimi bro wangu alinikomalia kinoma nijiunge nikamwambia sina pesa,akanishauri niuze baadhi ya assets gari/kiwanja nikawa nampotezea,siku moja yupo na partner wake wakawa wananikomalia zaidi,nikawaambia kwa kuwa wao wanaingiza pesa nyingi wafanye utaratibu wa kuwa wanakopesha watu wajiunge zaid,tokea hapo kimya had leo.
Goodmorning

Sent from my TECNO KA7 using JamiiForums mobile app
 
Goodmorning billionaire!

[emoji23][emoji23][emoji23] kuna ndugu yangu mmoja alinipigia Simu akaniambia niende Mikocheni kuna jambo anataka kuniambia akanielekeza karibu na kwa Mch. Mtikila nafika pale nakaribishwa aisee na watu waliofanikiwa wamenunua magari ya kifahari (sound) jamaa wanaongea wale acha, uzuri nilikua nishakutana nao watu jamii hiyo kama Forever Living nikawasikiliza tu.

Nilipotoka pale yule ndugu yangu nilimtukana acha kabisa. Yaani pamoja na usomi wangu lakini alikamatwa kipuuzi, hadi leo huwa analia.

Maisha ni kuchagua.
 
... kabisa kabisa, Kishimbe wa Kishimbe ni msukuma! ... shida ni kwamba mimi ni msukuma born town, yaani nimezaliwa mtaa wa Karuta, Mwanza city, Primary school Nyakabungo, Secondari Mwanza seko, High school Tambaza .... !
UTANIPATA WAPI?
😅😅😅😅
Sasa Mwanza napo ni town? Wasukuma buana.😀😀
 
Sister angu nilimshauri Sana Hawa watu MATAPELI, alliance hao, akanambia yaan ww siku ukiniona nimefanikiwa ndo utaamin, akapeleka laki Tano za kuniunga nikaona karudi na fuko limejaa madawa😂.

Kazi ikawa kwake kuzitembeza na kuziuza kwa watu Ili arudishe pesa yake na faida.

Hadi Leo ninapoandika hapa huu ni mwaka wa nne hakumpata mteja hata mmoja 😂,dawa zenyewe gharama. Kweli, amebaki navirutibisho tu anawapa wanae😂😂
 
Hivi unaanzaje kuwashitaki QNET?

Kikwelikweli kabisa QNET ni matapeli wanaotumia 'FEARS' za mtu kupitia njia ngumu ya kuupanda mlima mkali na mrefu kuyafikia mafanikio kwa kumpa 'shortcut' hewa! ... LAKINI, KWELI KABISA, HAWASHITAKIKI!

Wanachofanya QNET ni biashara halali kabisa ya kumuuzia mtu bidhaa, kwa ridhaa yake kabisa, na kisha kumuambia mteja kuwatafutia wateja wengine ili wakupe cha juu! ... na kadri unavyo'WALETA'[emoji28] wengi zaidi ndo unvyozidi kunufaika! ... yaani nikinunua mali ya shillingi million tano, japo bei halisi ni elfu hamsini, na nikawashawishi wengine kibao, basi naweza kupata hata million mia moja ... na hawakunyimi!
BIDII YAKO TU! [emoji28] WALETEE!

SASA WADAU HEBU NIAMBIENI, HASA WANASHERIA, TUNAWAFUNGULIA MASHITAKA QNET KWA VIFUNGU GANI VYA SHERIA?

NB: HAWA JAMAA WANA LESENI HALALI YA BIASHARA NA SERIKALI INAWATAMBUA! ... AMMA NIMELISHWA MATANGO-PORI?

WADAU, MJADALA HUO MEZANI HEBU LETENI HOJA TUKAWASEMEE HAWA QNET KWA MAMA!

UPDATE:
UKIPATA MUDA NA MB[emoji28]:
Wakati wa Mchonga na Sokoine (RIP) Mwaka 1984 serikali ilikuja na kamata kamata ya wafanyabiashara waliokuwa wanauza bidhaa zaidi ya bei kikomo.. Wakaitwa WALANGUZI na kitendo chenyewe kikaitwa ULANGUZI

Mashushushu wa serikali walitawanywa nchi nzima kuwakamata walanguzi.. Ni kosa kisheria kumuuzia mtu kitu juu ya bei kikomo. Qnet wanaweza kushtakiwa kwa hilo
 
Sister angu nilimshauri Sana Hawa watu MATAPELI, alliance hao, akanambia yaan ww siku ukiniona nimefanikiwa ndo utaamin, akapeleka laki Tano za kuniunga nikaona karudi na fuko limejaa madawa[emoji23].

Kazi ikawa kwake kuzitembeza na kuziuza kwa watu Ili arudishe pesa yake na faida.

Hadi Leo ninapoandika hapa huu ni mwaka wa nne hakumpata mteja hata mmoja [emoji23],dawa zenyewe gharama. Kweli, amebaki navirutibisho tu anawapa wanae[emoji23][emoji23]
Niliwahi kuitwa na ndugu yangu flani kuwa kuna fursa maeneo ya Mwenge Dar es Salaam Tz. Kufika nikaanza kuuliza ni fursa ya nini, wananijibu wewe tulia tu. Hahaha baadae nkaanza kusikia habari za Good morning nkajua tu nshaingia cha kike. Nilisepa bila kuaga
 
Kuna wale madogo wa mbezi walikuwa wanahojiwa...mmoja akasema yeye amenunua centa kwa million tano, mi nikajua hiyo centa ni gari...
Kumbe chakula!![emoji23][emoji23][emoji23]
Watu hawapo serious na hela zao kabisa[emoji23][emoji23][emoji23]
Hela yenyewe ilivyo ngumu hivi.
Bora hata angeenda kununua ka kiwanja baada ya muda angeona faida yake.
 
Mimi mama mkwe wangu alinikaribisha Qnet anile kichwa, kumbe mi ni muhuni kitambo, nikaenda nikala goodmorning za kutosha Halaf nikapita hivi. Wapo wengi, Ori flame, gnld, free cell, forever, desilake
Hii Desi kuna ndugu yangu alikuwa ananiforwadia mimessage yao wattsap kika mara mpaka kero.
Naona siku hizi katulia watakuwa washamla kichwa.
 
Wakati wa Mchonga na Sokoine (RIP) Mwaka 1984 serikali ilikuja na kamata kamata ya wafanyabiashara waliokuwa wanauza bidhaa zaidi ya bei kikomo.. Wakaitwa WALANGUZI na kitendo chenyewe kikaitwa ULANGUZI

Mashushushu wa serikali walitawanywa nchi nzima kuwakamata walanguzi.. Ni kosa kisheria kumuuzia mtu kitu juu ya bei kikomo. Qnet wanaweza kushtakiwa kwa hilo
Yalishapita hayo, siku hizi kuna biashara huria, tena siku hizi Serikali ndio mteja mkuu wa biashara ya kulanguliwa bei.

Hao Toyota wanawauzia serikali magari kwa bei mbaya ambapo serikali ingenunuwa wenyewe kiwandani Japan ingeokowa mabilioni ya pesa za walipa kodi.
 
Back
Top Bottom