jooohs,
Hiyo mifano ya magari ya tshs 80 million kama Tata au Canter au coaster nilishasem sio mizuri kwa sababu kuna tofauti sana kati ya vyombo vya transport na vifaa katika hii list. Mimi mwenyewe niliwaambia nina kampuni ya tours na tunatumia landcruisers za 50 million tshs na kuendelea ambazo kampuni inakodisha kwa kampuni nyingine au nawapatia driver guides ambao wanazungusha wageni mbuga za wanyama.
Lakini kumbuka kampuni inafanya vetting ya uhakika sana kabla ya kumpatia mtu land cruiser. Mtu anafuatiliwa historia yake makazi yake, je ana historia ya udokozi na wizi au ni mwaminifu?, wazazi wake wako wapi? wanafanya nini?, ana familia manake mke na watoto?, je amejiaminisha na magari ya wengine tayari kabla ya magari yangu. Nk. Hiyo ndio process pia inatumika kumpa mtu bajaji, magari ya mizigo etc. Usipofanya hivyo eti
ukampatia tu kila anayekuja kutaka gari lako unafikiria itakuwaje kwa Tz yetu?
Pia kwa kampuni yangu, gari hailali kabisa nje kama wageni wameshamaliza kazi. Gari ikiwa na wageni, inajulikana kabisa inalala wapi. P
ia cruisers zote zina GPS tracking devices mbili ambazo madereva hawajui imewekwa wapi kwa gari. Kwa hio naomba muangalie tofauti ya process ya kukodisha magari kama Tata uliyoyataja na vyombo hivyo kama welders nk. Hivyo vyombo mfano mjini, utakodisha kwa waswahili wengi sana na utawajuaje? Na ukisema kitu cha milioni moja, milioni moja kuipoteza ni sawa? Kwani sio hela?
Nakubaliana nawe kuhusu kijijini.
Kijijini kila mtu anamjua kila mtu. Hapo lazima biashara iwe nzuri. Na kufuatilia historia ya mtu kwa kijijini ni rahisi sababu watu sio wengi na wenye udanganyifu na uswahili, udokozi/ wizi wanafahamika kabisa ni wakina nani. Kwa hio mtu kama huyo akija au rafiki yake, au ndugu yake, unampiga chini tu akitaka kukodi equipment.
Hapa tunaongelea mijini sababu asilimia yetu kubwa ni mijini. Mimi ndio swali langu hilo. Majiji kukodisha hivyo vifaa hakika utalizwa tu.
Naomba labda mtu aje na wazo lingine, lakini la kwako ndugu yangu bado halijatatua hii changamoto kabisa.
Risks zipo kila biashara, na kama nilivyosema ni muhimu kuzifahamu na kutafuta namna ya kuzikabili. Wizi upo kila sehemu, na ndio maana nimekutajia jinsi watu tunavyoukabili kwa kuwapatia watu magari ya thamani kubwa wayaendeshe. Pia kwa watu wenye maduka nk, wanaweka hatua muhimu kuzuia hilo. Lakini hizo idea za controla kwa mijini ni ngumu sana. Na sio sawa kuwaambia watu watafanikiwa kwa akili ndogo.
Hakuna biashara inayotumia akili ndogo. Mimi sikuwa na lengo baya tokea awali, nilitaka tubadilishane mawazo tu, ila controla akaanza kunishambulia na kujisifia sana wakati mimi najua kabisa wala hafanyi biashara yeyote. Ni mwandishi mzuri sana lakini.
Ila sasa kuandika mada inayotoka kichwani, na kuandika mada mbayo mtu una experience nayo ni vitu viwili tofauti kabisa. Na jinsi mdada/ mmama alivyonishambulia, inaonyesha hana ujuzi kabisa wa biashara.