Hivi unajua unaweza kutumia akili kidogo tu ukapata pesa nyingi?

Hivi unajua unaweza kutumia akili kidogo tu ukapata pesa nyingi?

Mtoa mada, nikupe pongezi kwa mada yako nzuri inaelimisha na kufungua watu ubongo, wafikirie nje ya box, ila kusema suala la kutumia akili ndogo napinga kabisa, ukitaka jambo lifanikiwe inahitaji akili kubwa, kufanya kazi kwa bidii + commitment

Biashara bila mkakati utaishia kufeli. Na wengi wanaishia kufeli kwa kukurupuka, kama mdau hapo juu ana chance kubwa sana ya kufeli (80%) (compactor) hajui chochote kuhusiana na biashara hiyo, hamna hajafanya market research, hajawai kuifanya ila kwa kuwa umemtajia 50,000/= kwa siku kachanganyikiwa. Sawa kabisa na wale wa kilimo cha matikiti

Ushauri wangu kwa wadau, hamna biashara inayohitaji akili ndogo, biashara zipo na zinaonekana tafuta ambayo una passion nayo, think big start small(kuwa na dira unataka kuifikisha wapi biashara yako) ikikua multiply it,(fungua matawi) ila ni akili kubwa, juhudi, utayari na huduma nzuri zitakufikisha unapopataka ila haya ya mtoa mada mwenye biashara 10 zinazofanya vizuri kwa kutumia akili ndogo mkikurupuka yatawaingiza chaka

Sent using Jamii Forums mobile app
 
13 mega pixel,
Indeed mdau nimeona tu post yako na najua kabisa una experience sana ya biashara. Kama watu hawatachukua kitu chochote katika post yako, kitu kimoja tu angalao basi wazingatie ni ulivyosema kuhusu passion.

Watu nimeona wanapenda kupewa idea za biashara. Na ndio tz yetu unakuta watu wanaiga kila mtu. Creativity na innovation ni ndogo sana. Kila mtu anafanya duka wakati kuna fursa nyingine nzuri tu sana.

Idea ya biashara nzuri kama ulivyosema ni ile ambayo mtu unaguswa sana nayo (you are passionate about it). Na pia ni muhimu na inasaidia mtu kuwa na ujuzi nayo angalao kwa kiasi fulani. Lakini passion huwa inasaidia hata mtu kujifunza hicho kitu kwa moyo sana na akapata ujuzi wa kufanikiwa vizuri kabisa. Vilevile passion itasaidia mambo yakiwa magumu. Sababu mtu ana-enjoy hicho kitu kwa moyoni, hata mambo yakiwa magumu bado anamudu kuendelea kupambana tofauti na kitu ambacho ni kama mzigo.

Mara nyingi watu walioajiriwa wanapenda field zao na ndio maana wamezichagua, na mtu anaweza kuanzia hapo. Kama mtu ni accountant, anaweza anzisha huduma binafsi ya mambo ya accountancy au hata akasaidia mambo ya hesaby za kifedha pamoja na mambo ya ushuru (taxes) kwa biashara ndogo ndogo kwa kuanzia. Kama mtu ni mwalimu, anaweza anzisha ufundishaji wa tuition hata nyumbani kwake kwanza. Kama ni computer expert, kuna njia nyingi ya kuanza kutoa huduma binafsi.

Point nyingine kubwa umesema ni kuhusu kuanza na kidogo huku mtu akiwa na lengo kubwa (Start small, but think big. Hata ngazi mtu unapanda kuanzia chini. Mtu anafanya kitu kwa moyo huku akibuni na kujifunza njia za kukuza kampuni ikawa kubwa sana baadaye. Mhasibu akawa na kampuni kubwa ya accounting and finance, mwalimu baadaye akawa na shule binafsi, computer expert pia hivyo hivyo.

Asante sana kwa mchango wako mjasiriamali mwenzangu.
 
DocJayGroup,
TANGAZA BIASHARA: Biashara ni kuitangaza (Marketing). Bila marketing, hakuna kitu. Kama mhasibu unaanzisha huduma ya kusaidia biashara ndogo ndogo mambo ya hesabu za fedha, mambo ya TRA nk, ni lazima ukatangaze huduma hiyo. Wafanya biashara wakufahamu. Kama ni mwalimu wa tuition. Hivyo hivyo. Unatangazia wazazi, wanafunzi nk.

MATOKEO: Lakini pia lazima matokeo (results) za huduma yako ziwe nzuri. Wanafunzi wasaidike. Tuition unayotoa ilete mabadiliko chanya. Hakika watakuja na kuja na kuja. Kama ni huduma ya uhasibu poa hivyo hivyo. Mtu unasaidia biashara ndogo zinaepuka matatizo ya TRA nk. Unawaonyesha hata namna ya kufanya mahesabu wao wenyewe nk.

Marketing italeta wateja, lakini Matokeo mazuri ndio yatakayofanya wateja walete wateja wengine na biashara ikue.
 
Shukrani sana mkuu kwa kushare nasi ideas ambazo kwa macho ya kawaida hauwezi kabisa kuziona .
 
Shukrani mkuu vp Biashara ya kununua air compreser kwa ajili ya kujaza upepo hivi ukimuachia mtu si anakuibia tu pesa

Sent using Jamii Forums mobile app
Biashara ambazo huwezi kujua kama hela imeingia au haijaingia,makabidhiano ni kwa makubaliano maalum,mfano bodaboda akipewa dereva hesabu kwa siku ni 8000 kila siku,hii 8000 kila siku ni "lazima"


afanye kazi asifanye boss haimuhusu,anataka 8000 yake iwe pale pale. na pia Kwenye hii Air compreser nayo hesabu ni kama boda boda,daladala,nk


kwanza kabla ya kumpa/kumuajiri mtu kaa kazini boss wewe mwenyewe kwa mwezi 1,hii ni ili kujua ofisi kwa siku inaingiza sh ngapi,ukikaa mwezi kisha kila siku ofisi inaingiza 15,000 kwenda mbele (tayari umeshajua income ya ofisi yako)


ndipo unaleta mtu sasa unamwambia kuwa nakupa ofisi hiii nataka kila siku unipe 10,000 unamwambia 10,000 lakini unajua kabisa anapata zaidi ya 10,000 lakini unamwambia vile ili nayeye apate chochote kitu,kwahiyo kwenye hii 10,000 hamna maelezo ya biashara mbaya au nzuri

hela ya ofisi 10,000 inahitajika,kama hawezi mweke pembeni Hafai huyo,ataekubali mpe kazi.
 
CONTROLA,
Ila pia asisahau huyo mtu atakayemweka awe ni mwaminifu sana kwa asilimia zote. Binafsi naamini watu wasio na uaminifu mkubwa, hawastahili kabisa kusimamia biashara.
 
DocJayGroup
Kwanza nitoe pongezi kwa kuweza kuchangamsha mada hii ,maana biashara yoyote bila kuingia lazima tujaribu ku analyse risk mbalimbali zinazoweza tokea. Watanzania wengi tunapenda kufanya investment kwa ajili ya generate pesa na pia wengi wetu tunapenda kufanya biashara ambazo sisi hatutojishughulisha nazo na ndio mwanzo wa matatizo.

Mleta mada kaleta mada nzuri na yenye kumjenga kila mmoja hivyo basi yafaa kila mmoja wetu ajaribu kuangalia risk mbali mbali zinazoweza tokea kabla ya kufanya kitu. Yaweza tokea mtu sasa ameenda chonga vibanda bila kujua wateja wake akiamini baada ya kumaliza kuchonga ata anza kupokea hesabu kwa siku.

Hakuna biashara rahisi kila biashara inachangamoto zake ..take risk kuwa na nidhamu mafanikio utayaona
 
Nimeipenda hii, na jenereta lipo hapa home alinakazi, kama kunaaliye interest tunaweza kushirikiana. Kwa aliye dar
Pale buguruni sheli kulikua kuna jamaa wawili mwaka 2016 ( sijui kama bado wapo hadi sasa) waliungana walinunua generator moja ya laki 4 wakawa wanawasambazia taa wale wafanya biashara wa matunda kuanzia saa 1 kamili jioni hadi saa 5 usiku kila mfanyabiashara analipia buku.

Hawa jamaa walikua wanapata si chini ya elfu 70 kwa siku wakati wao huweka mafuta ya elfu 10 tu kwa siku. Mtaji wao ni generator ya laki 4, idadi ya taa (energy sever) kwa idadi ya wafanya biashara waliopo, waya na holder za kuwekea bulb. Jamaa waliniambia jumla mtaji wao ni kama laki 7 tu ambayo wana uhakika wa kuiingiza ndani ya wiki mbili.

Ni biashara ambayo haina kodi sanasana kumpoza tu mwenyekiti wa mtaa wa eneo lile ili ufanye biashara kwa amani na serikali ya mtaa ikupe ushirikiano unapopata changamoto. Sasa hii idea unaweza kuihamishia kwnye eneo lako unaloishi au sehemu yoyote unapoona hiyo fursa.

Sent using Jamii Forums mobile app

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Yani niweke mill 4 huku nikitegemea kupata elfu 80 kwa mwezi hiv unaijua nguvu ya mill 4 wewe hilo sio wazo la biashara
 
Mii nilishafanya hii biashara ya kukodisha vitu tangu mwaka 2001-2003.
Karibu na pale mbezi Sasa kimejengwa kituo Cha mabasi. Niliweka mashine za kupiga matofali, vibao vya matofali, manailoni ya kufunika matofali ikija mvua.
Pia nilikuwa na welding machine 4 niliziweka hapa Sinza kwa Remmy Sasa Pana ukumbi unaitwa majestic hall. Nilikuwa nawakodisha mafundi uchomeleaji.
Nikawa na guta 2 zilikuwa zinapaki manzese.
Ic matumizi ya hivi vitu daah. Mtu akichukua kitu chako anavyokitumia yaani anakikomesha.
Hazingatii uwezo wa kitendea kazi. Mashine ndogo ya welding anataka aweke Moto mpaka mwisho ili skate chuma wakati Ile niya kuungia chuma na sio kukatia.

Baadae nilianza kukodisha screen kwaajili ya kombe la dunia Kama mtakumbuka mwaka 2002 world cup ilifanyika Japan na Korea. Jamaa walikodi mwezi mzima, lkn ilibidi wavunje mkataba kwa sababu hawakuwa na wateja maana mechi zilikuwa zinachezwa alfajili.

Ninachotaka kusema hapa unatakiwa kuwa makini Sana na kifaa chako. Matumizi ya wanaokodi huwa Ni mkomoeni. Vinginevyo kifaa chako kitachakaa kabla ya kukulipa..
Unaweza kukuta chombo kimewekwa upside down. Kipo kwenye vumbi, yaani unaweza kulia.
Kila mtu anawaza pesa, kila mtu kichwa chake ina picha ya mafanikio na asilimi 90% ya hawa watu wote wanaowaza pesa na mafanikio na maisha mazuri hufikiri pesa inapatikana kwa kufanya biashara tu, labda auze kitu fulani ndipo apate pesa.

Kuna njia nyingi za kupata pesa kwa wewe ulie na mtaji, hapo ulipo unaweza ukawa na pesa yako ila hujui uifanyie biashara gani au labda muda wa kusimamia hiyo biashara kwako ukawa mdogo hivyo unaogopa na hujui cha kufanya.

Sasa sikia leo nitakupa list ya vitu vya kufanya ujitoe na stress. Kuna watu najua hata tuongee na maturumbeta tupige ila hampo tayari kuacha kazi mnazofanya mjiajiri ila mpo tayari kuanzisha biashra ikafa, mkafungua ingine ikafa mkafungua tena na tena hamchoki ila sio eti mjiajiri najua mpo.

Sasa najua kuna watu mmeshajaribu kufungua biashara nyingi sana na mwsho kwasababu ya usimamizi biashara zote zimekufa, mmechoka na mmekata tamaa hamjui mfanye nini, hamna shida soma nitakavyoviandika leo kisha chomoka na kimoja kakifanyie kazi.

Leo naongelea biashara ya KUKODISHA VITU

Najua unaweza jiuliza utakodisha nini na kinauzwaje na kinakodishwaje,mimi leo ntawapa mfano ya ninavyovijua tu na ambavyo nina uhakika navyo, hivyo kama na wewe utapata idea usiache itoa yako ili namimi niipate nione nafanyaje.

1. VIBANDA VYA TIGO PESA
Nadhani wewe ni shahidi ya Mawakala wangapi unawakuta na miamvuli huko barabarani, nataka kukwambia kitu hao Mawakala sio kwamba wanapenda kukaa na miamvuli na meza tu ila sababu ni kwamba hana pesa ya kutengeneza kibanda,chakufanya wewe tengeneza kibanda kidogo cha wakala wa Tigo Pesa ambacho gharama yake kuanzia mabati, bomba mpaka kinakamilika ni 250,000 kwa kibanda kimoja, ina maana kama una Milioni 1 una uwezo wa kutengeneza vibanda vinne vilivyokamilika imebaki mtu kuchukua kwenda kufanyia kazi.

Kodi ya kukodisha hivi vibanda kimoja kwa mwezi ni 20,000 ina maana kwa vibanda vyako vinne una uhakika wa 80,000 kila mwezi hiyo ni uhakika yaani, sio ya kutafuta au kupigizana kelele na mtu na uchukuaji kodi wa hivi vibanda ni wa mwezi mtu akupe kodi ya mwezi tu kisha apige zake kazi.

2. BANDA LA BIASHARA
Hili banda halina utofauti na hilo banda la tigo pesa hapo juu tofauti yake ni ukubwa, kutegemea na uwezo wako ila kwa banda la ukubwa waupana futi 5 na urefu kwa futi 10 gharama ya ujenzi wa hili banda ni 500,000 hivyo ukiwa zako na 1M utaweza tengeneza mabanda mawili ambayo utayakodisha kwa wanaotaka yakodi bei yake kwa mwezi 30,000 to 50,000 kodi itategemea na wapi unaenda kumuwekea hilo banda, ukienda liweka sehemu nzuri kodi utaweza kumpa hata 60k to 100k na akalipa bila shida maana eneo hilo frem kodi ni 300k kwenda mbele. Assume una mabanda yako mawili ya kodi 50k kwa mwezi utakua unaingiza 100,000 isiyo na maelezo.

3. MASHINE YA KUCHOMELEA
Hizi mashine zipo za aina mbili kuna zile portable za kubeba halafu kuna yale transforma lake limesukwa na nyaya za aluminum, bei ya kuyanunua haya

- Portable: 400,000
- Kusuka: 300,000

Kukodisha haya ma mashine ni kwa masaaa 6 na masaa 12, kuna bei ya 6hrs na bei ya 12 hours, bei yake kwa 6hrs 20,000 na 12hours ni 30,000, ila kwa mashine portable 6hrs ni 30,000 na 12hrs 40,000.

Calculate hapo uone kwa siku utakuwa unaingiza sh ngapi, hii biashara ukijuana na mafundi welding kazi zitakuwa kila siku 5000 elfu kumi vitakuwa havikauki kwenye wallet/ pochi yako kiufupi huwezi kuwa na shida ndogondogo.

4. MUZIKI SPEAKER ZILE ZA KUCHOMEKA FLASH
Hizi speaker nilijaribu kununua kwa ajili ya ki pub changu uchwara fulani hivi sikuwaza kama hizi speaker ni dili basi wateja wale wale wakawa wakija wakisikia muziki wake wananiuliza kama nakodisha nikaanzaga zikodisha kama utani kwnye visherehe vya birthday huko mitaani, bei ni 50,000 kwa event 1 kiukweli hamnaga weekend hizi speaker nakosa simu ya kuombwa watu wakizitaka maana watu n wana sherehe kila leo na miziki yao ya subwoofer haitoshelezi haja zao.

Zitafute hizi speaker zinunue usiogope hela yako itarudi bila wasi wasi, zipo size tofauti ila kwakuwa unataka ya kibiashara nunua ya 600k to 700k hapo utapata heavy weight mziki kwa shughuli za mitaani, mfano ni kama hii Ailipu hapa chini japo kampuni zipo kibao zinazotengeneza hii mispika ya hivi.


5. KABATI ZA ALUMINIUM
Umeshaenda kununua chips mahali? Umeshaona chipsi zinawekwa kwenye nini? Basi tengeneza yale makabati nakuhakikishia hamna kikwazo kikubwa kwenye biashara ya chipsi kama KABATI Zero IQ ni shahidi muulizeni awambie mtu ataweza jidunduliza anunue kila kitu ila mtihani ukaja kwenye kabati.

Sasa tengeneza makabati yako ya 200,000 tengeneza makabati manne kisha yaweke mahali andika yanakodishwa, humalizi masaa 24 tayari ushapata mteja, haya makabati bei yake kabati per day ni 2000 maana yake kabati 1 kwa mwezi litakupa 60,000 x 4 = 240,000

Unaweza amua tengeneza vikabati vidogo kwa ajili ya mtu kuweka kachumbari na vitu vidogo vidogo ambavyo bei ya kabati kutengeneza ni 150,000 kisha wewe utalikodisha kwa 1000 per day x 30 days = 30,000 x 4(idadi ya makabati) = 120,000 kwa mwezi jumlisha bei ya makabati yako yote uone utakua na kiasi gani.

6. JENERETA
Kwa Tanzania yetu hii ndugu zanguni hii ni biashara nzuri sana, sijui kama utanielewa ila hii ni biashara ambayo ataekufata/ kukupigia simu unamtajia bei huku unakula karanga zako na hawezi kataaa wateja wapo kibao tena wengi tu, vuta picha watu wamekuja kwako kukodisha zile spika plus jenereta yani hela utayoingiza hiyo siku sijui nisemeje.

Kukodi jenereta bei inapatikana kwa aina ya jenereta anachukua kubwa au dogo na linaenda kufanya kazi kwa muda gani ila bei yake kwa dogo ni 30,000 na kubwa ni 50,000 muda ni 12hours.

7. UNA KIWANJA KIPO TU
Unaogopa nini kutangaza kuwa unakodisha eneo la mtu kufuga, au kufanya chochote akipendacho kwenye kiwanja chako kisha ukampa kodi yako kwa mwezi? Huna mpango wa kujenga leo wala kesho ila una likiwanja limekaa huko lipo tu linaoteana majani (ndugu yangu ile ni pesa umeikalia) huwezi itumia wape wengine watumie kisha atakulipa.

Unaona faida gani kusema nina kiwanja changu mahali ila kipo tu hukifanyii kitu? Huo ni uchoyo wa kusaidia wengine na Roho ya kimaskini iliyo ndani yako wape watu wafanye kazi na wewe upate hela (sikulazimishi) ila hii nayo ni fursa, usisubiri kudhani wapangishaji ni wenye nyumba tu utakuwa upo ulimwengu wa Analog.

Siku hizi kuna wababa wenye vibanda, baba wenye viwanja, mama mwenye vyombo, dada mwenye ma dryer, nk nk yaani fursa juu ya fursa ila ni lazima uwe na roho ya kutoa na kusaidia wengine nawe ndipo utafanikiwa kupitia wao.

Biashara ni nyingi sana wakati mwingine huna haja ya kufanya wewe biashara ukijiona huwezi biashara sio mbaya ukawasaidia wengine kisha na wewe ukajipatia kitu kupitia kuwasaidia huko maana mwisho wa siku na wewe unahitaji pesa.

Hizi biashara hazina gharama ukinunua hivyo vifaa gharama ya kuvitunza ni wewe mwenyewe tu, yule anayekutafuta lazima anakujua na yule ndio atakuwa jicho lako huko kifaa chako kinapoenda na kwa hivi vifaa kama makabati, mabanda nk ni vitu unavyoweza vizungukia hata wewe mwenyewe kuona usalama wake upo vipi.

Una pesa unataka kufanya biashara na huoni biashara ya kufanya, Fungua jicho lako angalia pembeni yako utamuona machinga katandaza vitu chini mfuate muulize nataka kukununulia meza uweke vitu juu kwa siku unipe 1000 au 500 upo tayari? akikubali kamtengenezee.

Ukimalizana naye angalia upande huu utamkuta mama ntilie anauza sana ana wateja sana ila wateja wake wanakalia viti vibovu, mfuate mwambie unataka mnunulia viti then atakulipa 2000 per day kwa viti na meza zako, akikubali kamfuatie vitu.

Inawezekana kama ukiamua kuwaza tofauti na wengine, sio lazima wote tuwe wakulima hebu mimi na wewe tuhakikishe yule mkulima analima vizuri tumpelekee maji ya kunywa, leso ajifute jasho, ajisikie anajaliwa halafu tuone kama akivuna atakuacha bure na tuone kama maisha hayatoenda, shida yetu binadamu tuliozaliwa na mwanamke tuna roho za UMIMI tukizikemea na kuzikataa hizi roho tutafanikiwa sana.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom