Hivi unajua unaweza kutumia akili kidogo tu ukapata pesa nyingi?

Umeongea point ya muhimu sana hapa.Mimi nilikuwa nilinunua bodaboda used lakin ilikuwa imetumika kidogo maana mshua yule alimnunulia mtoto wake wa kiume ila dogo ubishoo wake akakataa kuwa bodaboda.Mshua akapaki mzigo hatimaye akatuuzia.
Tukatafuta kijana mmoja wa kanisani akawa bishoo akashindwa hata kupata 40 au 50 elfu kwa wiki wakti ndo bei ya kawaida kwa bodaboda alichofanya bila kukutaarifu sisi nae akawa anampa mshikaji wake ambaye wanafahamiana.Wakaanza kuikongoloa yani full kupiga pesa halafu kwetu wanaleta matatizo tu mara leo sijui blaabla tu kila wiki tena wanaleta blabla siku ya kukabidhi pesa,sasa yukawa tunajiuliza kwa nini wasiyutaalifu mapema?
Baadae mi na jamaa yangu tukachoka tukawanyang'anya pikipiki baada ya wiki kadhaa tukasikia mshikaji tuliyempa saiz kanunua yake,inamaana alikuwa anaficha hela ili aongezee anunue yake.Tukatafuta kijana mwingine ni mwaminifu na anatupa kiasi tunachotaka na kukitokea hitilafu kabla ya jumapili anatutaalifu na kwa ushahidi unaoonekana.

Kwa hiyo ukinunua, kitu kama ukampa mtu akusaidie kuendesha halafu akulipe kias kadhaa hakikisha unakuwa mfuatiliaji(management)na wakati mwingine unamwongoza(leadership)mfano kufanyia ukarabati chombo n.k.Sisi hatukufanya yote hayo kwa sababu tulikuwa wote wanafunzi mwaka wa 1 na jamaa yangu mwaka wa 3.Saiz jamaa amemaliza na yuko huru anaguatilia vizuri sana na kila hatua yuko nao.Saizi faida inapatikana.Ila ukiwa mwanafunzi au mfanyakazi kutwa kazini au chuoni basi hakikisha hata akisema amenunua sijui nini mwambie apige picha atume whatsup uone mwenyewe lakin kama yuko mbali na anauhakika humchunguzi anakuambia tu leo nimenunua helmet mpya ya abiria kumbe mwongo tu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Aseee unaakili umewaza mbali sana
Ila mimi natamani kufanya biashara tatizo naogopa kutapeliwa au kufilisika hata hivi nakabiashara ka handbags lkn kananinyima usingizi
Nadhani nahitaji mwongozo kidogo
 
Yes mkuu, kila mtu atachomoka na chake kimoja kidogo kidogo tu kisha

baadae atajikuta vyote ktk list anavifanya,muhimu "tuwe tofauti ktk utafutaji"

Dah Mkuu hivo vibanda natengeneza mwenyewe na gharama za ufundi ni hizo hizo ngoja hali ya hewa ikitulia ntafata idea zako[emoji120]


Sent from my iPhone using JamiiForums
 
Thanks so much for those ideas.
Kwa sisi tuliokua tunawaza vya mamilion kumbe vipo vidogo vya kukupa pesa daily Tena bila Kodi[emoji38]

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ni mawazo mazuri sana
Kikunwa mtu azingatie location
Naona zinatoka maeneo ya watu wengi
 
Mawazo yako yalikuwa mazuri kuijenga mada kwa upande mwingine, biashara yoyote ina pande mbili ambazo zinatakiwa kuzingatiwa kabla haijaanzishwa (ulikuwa sawa) ila approach pengine haikuwa nzuri sana ndio maana mtoa mada aka react negative.
 
Shukurani sana na ubarikiwe sana kwa kuwa na moyo mkunjufu wa kushare na wengine fikra chanya juu ya biashara kwahilo tunakushuru
 
Kiukweli katika kujifunza mambo ya biashara kwa vitendo na research za mtaani nimegundua kwamba watu wengi huwa tunafeli kwa kuwaza mavitu makubwa(projects kubwa) na kuzidharau projects ndogo ambazo ukizipatia ziko very consistent.
Wakati kumbe kuna viprojects vidogo vidogo ukiwa navyo vitatu unaishi mjini.

Kwa mfano maeneo ya nyumbani dar kuna vijana fulani wameungana wakaanzisha project ya kutengeneza maandazi na chapati jioni maeneo karibu na stendi.
Wanapika machapati/maandazi makubwa moja linauzwa kwa shilingi 500.

Basi wanauza sana,wako vijana wanne na wako bize muda wote yaani ni kama kiwanda lakini wamekodi eneo tu wakapanga meza zao wala hakuna cha fremu wala nini.
Sasa hapo mahali kuna kijiwe cha bodaboda wananunua sana wakichukua michapati miwili ndio kama dinner yao ndio imetoka hiyo.

Na projects ya aina hii nimeiona sehemu mbili tofauti maeneo ya nyumbani ni vijana wa kichaga na kihaya kundi lingine.
Ndio maana mtoa mada nimemuelewa vizuri sana.
 
Ninachokiona hapa haya yote yapo hata huyu anaebisha asionekane kama chama cha upinzani tu mkumbuke kuna Jambo alilowakumbusha na ni kubwa pia mfano mtu angeenda kununua pikipiki na kumpa MTU anayedhani ataleta hela, pasipo tahadhari matokeo Jamaa siku akijikwaruza kweny mishe za kawaida anaeenda uiuza pikipiki anakuja na kusema wamenikaba na kunipora! Hi mpingaji anakukumbusha ufanye kitu kuzuia Hilo labda kufunga ma GPS na kila unaloona linaweza saidia kuhakikisha unakuwa salamander kweny biashara na mbaya kwakuwa utakuwa ndo umeianzisha

Ola muanzisha maada unajua kutupanga madini kina language hapa nitakafanyia KAZI
 
Umesema mafanikio kwa kutumia akili kidogo! Vipi ulimwengu wa roho hata kama hujaenda shule pesa unabeba kwa kapu??
 
Kuna sehemu huwa napita asubuhi naona kina mama wauza mboga wa kutosha wanaweza kuwa hata 300 ,na huwa wanskaa pale Kama masaa 2 wanaondoka...huwa narafakari Hawa niwape huduma gani,na Mimi nipate riziki ,sijapata jibu Hadi Sasa!
Misaada please!
 
Kuna sehemu huwa napita asubuhi naona kina mama wauza mboga wa kutosha wanaweza kuwa hata 300 ,na huwa wanskaa pale Kama masaa 2 wanaondoka...huwa narafakari Hawa niwape huduma gani,na Mimi nipate riziki ,sijapata jibu Hadi Sasa!
Misaada please!

Kauze uji wa ulezi, chai ya moto, au vifungashio vya hizo mboga
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…