Nilitamani kukuandikia insha ndefu sana maana unaonekana bado sana ktk Biashara,Ila nataka kukwambia kitu kimoja cha muhimu sana katika ujasiriamali/biashara kwa ujumla
Tuna cheza na Hatari ila Mjasiriamali/Mfanyabiashara alie kwiva hujua namna ya kudeal na hizo HATARI.Hata forex ina kitu inaitwa
STOP LOSS unaijua kazi yake hiyo kitu? huku kwenye biashara tuna
STOP HASARA
Unataka kujua STOP HASARA inavyofanya kazi? Penda kujifunza halafu ingia Field halafu nimalizie kitu kimoja,Siandikagi vitu ambavyo nasikia sikia kwa watu au kwenye vipindi vya radio,ukiona nimeandika kitu ujue nimeshakifanya
kama sijakifanya huwa nafungaga bakuli langu,ndio mana sinaga thread bandika bandua na si kwamba kila ninavyoandika ninachofanya kinafanikiwa kuna vinavyo feli sana tu ila kamwe hutoniona nikileta Ushuhuda wa kufeli kwangu humu JF ila ktk
Ninavyovileta humu na kuviandikia Kama mtu akivifata Probability ya Kufanikiwa ni 81%,ukiona kina ugumu au hakiwezekani Fahamu tu kuwa Haukujipanga.
Mechi yyte ili utoe matokeo mazuri yakupasa umjue Mpinzani wako kajiandaaje,ana silaha gani kisha ndio uingie vitani,ukienda kichwa kichwa bila kujiandaa utarudi mikono kichwani.
kwenye biashara unatakiwa uwe na vitu vifuatavyo
Taarifa sahihi,Mtaji,uzoefu,uthubutu.
DocJayGroup