Hivi unajua unaweza kutumia akili kidogo tu ukapata pesa nyingi?

Hivi unajua unaweza kutumia akili kidogo tu ukapata pesa nyingi?

✔✔✔
Asante sana mkuu.
Kuna mdau mmoja aliwahi pia kushare fursa ya kukodisha toroli kwaajili ya ujenzi.
oooh asante mkuu 🙏

ni kweli kwenye ujenzi vipo vya kukodisha vingi tu

nipo na mwanangu mmoja hivi yeye anakodisha mbao za lenta, ana kila Mbao yani

masururu, manyundo makubwa,yani ana full mazaga ya fundi ujenzi,yuko vizuri

Halafu yeye kazi yake ni kushinda kwenye pool table lake kukusanya sh 200 zake.
 
Umenikumbusha nilipokuwa primary school enzi hizo sijui lolote kuhusu business...alikuwepo mwana mmoja naye tulikuwa naye darasa moja.

Huyu jamaa japo tulikuwa level moja kidarasa ila alikuwa mbali kiakili hasa kuhusiana na biashara. Jamaa alitengeneza mikokoteni ya mizigo ile ya matairi ya baiskeli...kama mitatu.

Akaanza kukodisha kwa wabeba mizigo stendi ya mabasi...kila siku jioni anaenda zake kuchukua pesa waliyokuwa wamekubaliana kwa siku.

Yaani hapo sisi tuko naye skuli huku yeye mtaani matoroli yake yanamletea pesa.
 
7.Biashara ya kuonesha Mpira

Hii ni biashara inayohitaji eneo unajenga banda zuri la kisasa una funga Tv Kubwa nzuri hata mbili dish la azam na dstv.

Ambapo kwa mechi kma eneo ni zuri hukosi 50,000 au hata 30,000....siku hizi mechi karbu kila siku na imekuwa ni ugonjwa kwa watanzania ni kweli wanapenda mpira,kwenye malipo unaweza kuwatoza kwa kiwanji kwa kuuza buku soda au kwa kiingilio na kwa hali ilivyo watanunua tu vinywaji maana dk 90 ni nyingi sana.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Vitendea kazi Kama driller ya umeme,screwdriver,msumeno ya umeme,mafundi selemala wengi hawana mitaji ya kununua vifaa hivyo ama hawana access navyo bado wanatumia misumeno ya kutumia misuli,etc
Ni kweli na kama ukienda kuvinunua ukaja navyo wakajua unakodisha basi

kila siku watakuja kukodisha maana kazi zao zitaenda kufanyika kwa haraka

lakini itakua ni bora na nzuri kuliko angetumia mokono pekee.
 
Tempus Fugit,
Wapo watu wamezaliwa akili zao zinawaza pesa tu na fursa

unafkiri huyo mtu ukimtafuta sasa hivi atakua na mikokoteni mingapi?

ukiachia mikokoteni,biashara zake nyingine? Maisha ni Akili.
 
Hapa umefungua akili za wengi Chief! Wakati nasoma nilikuwa nawaza tu kumbe hata wale wamama wanaokaanga samaki uswahili na kuziuzia juu ya ndoo kwenye sinia unaweza kula nao mkataba, ukaongea na serikali ya mtaa, ukajenga banda zuri, meza safi na biashara ikapanda hadhi.

Ni dhahiri kabisa kuna watu wanashindwa kununua bidhaa hizo kwa sababu ya mazingira. Kwa hiyo mazingira yakiboreshwa na idadi ya wateja itaongezeka

Sasa assume unakusanya sh.500 kila siku na wauzaji wako kama 10

Maana yake 500*10= 5000/-

5000*30=150,000/-

150,000*12=?

Nilipita Morogoro kipindi fulani mitaa ya mji mpya kina mama wengi wanakaanga samaki na wanauza pembeni ya barabara, hawana banda, wenye meza wachache.

Sehemu kama ile unairasimisha na inakupa pesa nzuri tu kwa mwaka ukiwa umekaa tu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
TheDek,
Hiii ni biashara nzuri pia lakini kwa mtu asie na muda wakukaa hapo kibandani

kwake ni kazi sana kuona faida maana akisema aweke mtu,lazima atamuibia vizuri mno

hii biashara ni nzuri inalipa lakiini yakuhitaji wewe mwenye biashara ukae Golini ukusanye sh 500 zako.

Tofauti na hapo hii sio biashara ya kufungua halafu umuweke mtu alete hesabu,Utalia machozi ya Lugola.
 
Uko sahihi sana Kingjr2 tatizo letu vijana na watu wengi tunapoona

mtu anauza samaki au biashara yeyote basi akili yetu inawaza na sisi tuuze samaki

au tufanye biashara ile ile anayoifanya yule mtu au mtu akibadilika saana basi na yeye utamkuta

anawaza auze kitu flani,kila mtu akili yake inawaza Kufanya biashara kwa aina moja TU.
 
Sharing is caring, ila watanzania wana uvivu wa asili, watayaacha hapa,hapa.
Hakika wote tungekuwa na mawazo kama haya, hawa wanaolilia ajira wasingekuepo.

Thanks nimeongeza kitu.
 
Back
Top Bottom