Hivi unajua unaweza kutumia akili kidogo tu ukapata pesa nyingi?

Hivi unajua unaweza kutumia akili kidogo tu ukapata pesa nyingi?

Pale buguruni sheli kulikua kuna jamaa wawili mwaka 2016 ( sijui kama bado wapo hadi sasa) waliungana walinunua generator moja ya laki 4 wakawa wanawasambazia taa wale wafanya biashara wa matunda kuanzia saa 1 kamili jioni hadi saa 5 usiku kila mfanyabiashara analipia buku.

Hawa jamaa walikua wanapata si chini ya elfu 70 kwa siku wakati wao huweka mafuta ya elfu 10 tu kwa siku. Mtaji wao ni generator ya laki 4, idadi ya taa (energy sever) kwa idadi ya wafanya biashara waliopo, waya na holder za kuwekea bulb. Jamaa waliniambia jumla mtaji wao ni kama laki 7 tu ambayo wana uhakika wa kuiingiza ndani ya wiki mbili.

Ni biashara ambayo haina kodi sanasana kumpoza tu mwenyekiti wa mtaa wa eneo lile ili ufanye biashara kwa amani na serikali ya mtaa ikupe ushirikiano unapopata changamoto. Sasa hii idea unaweza kuihamishia kwnye eneo lako unaloishi au sehemu yoyote unapoona hiyo fursa.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
shiite,
Marakhaba.

Tatizo lako mkuu shiite ubongo wako una akili ila ulikua una u let down sana,yani akili ilishakwambia kuhusu hilo deal ila wewe kwa ubishi ukawa una delay delay,sasa usisubiri tena Usijiangushe bwana,Fanya kweli👊

Ubarikiwe na asante sana kwa moyo wako wa shukurani🙏
 
Abramovic,
Hiii nimeiona inafanyika sana sehemu nyingi siku hizi "watu wanajua tumia fursa sana miaka ya leo"
 
Hapo kwenye makabati ya chips unampa mtu analitumia siku mbili tatu analipiga bei anatembea na hutajua kakimbilia wapi au kunakuwa na mbinu gani ya kuthibiti usalama wa makabati?
 
Hapo kwenye makabati ya chips unampa mtu analitumia siku mbili tatu analipiga bei anatembea na hutajua kakimbilia wapi au kunakuwa na mbinu gani ya kuthibiti usalama wa makabati?
kabati la chipsi anapokuja lichukua kuna mtu anae enda kumpelekea

anapolirudisha kuna mtu analifata, ulinzi wa haya makabati ni very simple

hicho sio kikwazo kabisa hebu angalia kikwazo kingine na wala sio kabati.

Mtu hawezi kukimbia na kabati tu la 250,000,akaacha majiko,makarai,majalo,sahani,trei,vifaa vyote,nk

huyu mtu akitaka kuiba kabati hiyo siku kwanza hatowasha hata mkaa,ondoa wasi wasi.
 
✔✔✔
Asante sana mkuu.
Kuna mdau mmoja aliwahi pia kushare fursa ya kukodisha toroli kwa ajili ya ujenzi.
 
Back
Top Bottom