Hivi unamshushaje Diamond?! Au Mnamaanisha Wasanii Wapya wa WCB?!

Hivi unamshushaje Diamond?! Au Mnamaanisha Wasanii Wapya wa WCB?!

Chige

JF-Expert Member
Joined
Dec 20, 2008
Posts
13,495
Reaction score
29,872
Kwanza niseme jambo moja... na hili nilizungumza tangu nilipoleta uzi wa awali kabisa wa post ya Sallam.

Ninachotaka kusema ni kwamba, Sallam needs to act as a man! Kama nilivyosema hapo awali, tatizo la Sallam sio mvumilivu! Ni utoto kama sio ujinga kumjia juu Ruge kwavile tu Ruge aliwaambia SHILAWADU wakashitaki!

Aidha, ni ujinga pia kudai SHILAWADU walienda kwa Mose kama namna ya kutaka kumshusha Diamond kwa sababu, umbeya ndio unawaweka mjini SHILAWADU na hii wala sio mara ya kwanza SHILAWADU kum-target Diamond Platnumz binafsi let alone Dancer wake!!

Hofu yangu ni kwamba, huenda Sallam ame-panic kuona promo za Aslay! Lakini kwa wanaowafahamu Clouds, hivi ndivyo wanavyofanya wanapokuwa na project na msanii fulani! Kama tunakumbuka, walim-promote sana Ali Kiba na Seduce Me yake kwa ajili ya Fiesta hadi wengine wakafikia kuongea kama tunayoongea sasa kwamba wanam-promote sana Kiba ili kumdondosha Diamond!

Project iliyopo mbele ya Clouds hivi sasa ni ya Nandy na Aslya, mosi kwa ajili ya Valentine na pili, kwa ajili ya Show itakayofanyika Escape I hapo February 17.

Now back to the topic.... hivi hao Clouds wanamshushaje shushaje Diamond Platnumz?!

Asilimia kubwa ya Wana-Bongo Flavor, wanakodolea sana macho Fiesta na ndio maana inapofika karibu na Fiesta, wasanii wengi wanaachia ngoma mpya ili kutega Fiesta (Puuzeni wanaosema Fiesta wanalipa 500K... kwa majority ya wasanii, Fiesta ni msimu wa mavuno).

Lakini wakati wengine huwa wanaitolea macho Fiesta, Diamond Platnumz sio mtu wa Fiesta tena! Sio mtu wa After School Bash! Sio mtu wa majority of the shows zinazoandaliwa hapa Tanzania!

That said, huwezi kumtisha Diamond kwa Fiesta!!!

Wengi wanataja power ya media... ni kweli kabisa na hapa nishasema sana hili! Hata hivyo, hiyo power ya media inategemea! Diamond leo hii anaweza kuishi raha mustarehe kwa kutegemea mashabiki wa Kenya peke yake ambako Clouds wala haifiki!

Tena hawa mashabiki wa Kenya, kv Wakenya wengi pia wapo ughaibuni, ndio wanunuzi wakubwa wa muziki online kuliko Watanzania!

Diamond leo hii ngoma zake zinapigwa throughout East & Central Africa na wala sio kwamba hizo nyimbo wanazipata kutokea Clouds.

Dakika kadhaa zilizopita nimeweka habari za uzushi zilizoripotiwa huko Ghana kwamba Diamond amefariki kwa ajali ya gari. Ukiangalia Waghana walivyo more concerned huko Twitter, ndipo utakapojua nguvu aliyonayo Diamond barani Afrika!

So, ili kumshusha Diamond unatakiwa kuwa na misuli ya kupiga fitina sio tu Tanzania bali Afrika Mashariki Yote especially Kenya & Rwanda and the rest of Afrika!!

Utakapojua nguvu ya Diamond, kwa kawaida huwa anaachia video Youtube usiku hata kabla hajafanya media tours! Na hadi anafanya tour, mara nyingi anakuwa tayari keshavuna Views zaidi ya 1 Million!!

Hiyo maana yake ni kwamba, tayari ana angalau Fans 1 Million ambao wala hawana muda wa kusubiria radio au tv ya mwananchi yeyote toka popote pale duniani!!

Sasa unapiga vipi fitina kwa wote hao?!

So, ingawaje media zina uwezo wa kumshusha msanii lakini kwa Diamond is kinda too late! Wanaweza tu kumtikisa lakini sio kumdondosha!

NOTE: Kama kuna msanii yeyote humu JF, please, don't be blinded by this post... hapa ni Diamond lakini kwa wewe, utadondoshwa tu kwa sababu huna base yoyote ya maana ya kuweza kushindana na watu kama Clouds!!!
 
Diamond kwa upande mwingine anapoteza fans kwa tabia yake ya kuwa na wanawake mbalimbali.. anashangaza kutokujua kujiendesha kimaisha hata kama ndio anapenda kuwa na wanawake kila siku. Halafu anafata walio na majina ambao hawamuongezei kipato.. badala hata ya kujipatia wanawake walio wa kawaida sana.. na kuyafanya kimya kimya.
 
Tatizo limekuwa kubwa baada ya kuja mbosso sielewi kuna nini kimejificha nyuma yake.
Just my hunch>>> Kwangu naona ni kama coincidence kwamba Mbosso amekuwa introduced kati kati ya project ya Aslay na Clouds!

Sasa ukiangalia inakuwa like "what's the hell is going on here?" Hizi promo za kufa mtu za Aslay ni ili kumzima Mbosso kabla hajafika popote, au?!

I'm not sure lakini nahisi kama promo anayopata Mbosso pale WCB ni kubwa kuliko aliyowahi kupata yeyote miongoni mwao! Na kama mawazo yangu ni sahihi, basi huenda hofu ni ile ile kwamba promo kubwa za Clouds zinalenga kumzima Mbosso na WCB kujibu mapigo, ndo maana na wao wanakaza zaidi!!!

Anyway, kwa sasa sitawahukumu Clouds...!! Nitasubiri kwanza show yao ya Escape I kisha nione nini kitafuata na Aslay wao manake isije ikawa watu wana-panic kumbe it's all about VALENTINE BUSINESS!!!
 
Kwani mabosi wa Diamond haswa ni akina nani.. ukiachana na hao mameneja? Si inajulikana na yanaandikwa humu kila kukicha au ni uongo?
 
Diamond kwa upande mwingine anapoteza fans kwa tabia yake ya kuwa na wanawake mbalimbali.. anashangaza kutokujua kujiendesha kimaisha hata kama ndio anapenda kuwa na wanawake kila siku. Halafu anafata walio na majina ambao hawamuongezei kipato.. badala hata ya kujipatia wanawake walio wa kawaida sana.. na kuyafanya kimya kimya.
Kwan kuwa na wanawake wengi TatiZo liko wapi.... mbona r Kelly anawanawake mia kidogo
 
Alishuswa Sugu aliyeanzisha Hiphop..
Alishushwa TID aliyekuwa nyota hatare..

Ashindikane Diamond..

All in All hakuna anayetaka kumshusha kaona yemwenyewe anashuka anasingizia watu wanataka kumshusha..
 
Kwani mabosi wa Diamond haswa ni akina nani.. ukiachana na hao mameneja? Si inajulikana na yanaandikwa humu kila kukicha au ni uongo?
Mabosi kivipi?! Kimsingi, Diamond ndie Boss na wapo pia partners kwenye shughuli zake!

Kwenye WCB, kuna watu wenye shares zao lakini bado hawawezi kuwa mabosi wa Diamond kwa sababu brand ni yake mwenyewe kwahiyo hao ni partners tu.

Leo hii ingawaje Bakhresa na Diamond ni kama mlima na kichuguu lakini Bakhresa aki-team up na Diamond kufanya kitu bado Bakhresa hawezi kuhesabika ni Boss wa Diamond hata kama share za Diamond kwenye project husika itakuwa ni 1%... hawa watabaki kuwa partners and no one is someone else's boss!

Na ingawaje Diamond huwaita akina Babu Tale "Boss", kimsingi Diamond ndie Boss wa wote hawa hata kama Sallam hivi sasa hataki kuitwa Meneja kwa sababu tu ana hisa zake pale WCB!!

Diamond ana uwezo wa kuwaambia wote hao hataki tena kusimamiwa na yeyote miongoni mwao!
 
Alishuswa Sugu aliyeanzisha Hiphop..
Alishushwa TID aliyekuwa nyota hatare..

Ashindikane Diamond..

All in All hakuna anayetaka kumshusha kaona yemwenyewe anashuka anasingizia watu wanataka kumshusha..
Sijaona yeyote miongoni mwa hao uliowataja mwenye sifa nilizotaja hapo!!!
 
Mabosi kivipi?! Kimsingi, Diamond ndie Boss na wapo pia partners kwenye shughuli zake!

Kwenye WCB, kuna watu wenye shares zao lakini bado hawawezi kuwa mabosi wa Diamond kwa sababu brand ni yake mwenyewe kwahiyo hao ni partners tu.

Leo hii ingawaje Bakhresa na Diamond ni kama mlima na kichuguu lakini Bakhresa aki-team up na Diamond kufanya kitu bado Bakhresa hawezi kuhesabika ni Boss wa Diamond hata kama share za Diamond kwenye project husika itakuwa ni 1%... hawa watabaki kuwa partners and no one is someone else's boss!

Lakini ingawaje Diamond huwaita akina Babu Tale "Boss", kimsingi Diamond ndie Boss wa wote hawa hata kama Sallam hivi sasa hataki kuitwa Meneja kwa sababu tu ana hisa zake pale WCB!! Diamond ana uwezo wa kuwaambia wote hao hataki tena kusimamiwa na yeyote miongoni mwao!

Hivi kama kutangaza zile karanga analipwa kiasi gani tena?

Na hao partners ni akina nani.. clouds nasomaga humu ni wamoja wapo au?
 
Hivi kama kutangaza zile karanga analipwa kiasi gani tena?

Na hao partners ni akina nani.. clouds nasomaga humu ni wamoja wapo au?
Project ambayo nina uhakika Kusaga alikuwa na mkono wake ni Chibu Perfume. Kuhusu Karanga, ndo vile tu watu hatutaki kuukubali ukweli mchungu hususani kama unamhusu mtu ambae usingependa awe!!!

And remember, hata siku aliposema amechomoa kusainiwa na Jay Z, watu humu JF walikejeli kweli kweli kwamba jamaa anapenda kiki na wakaja kunayamaza zilipotangazwa habari za kusainiwa na Universal!!

Lakini maajabu ya watu, ile kuwepo VEVO tu tayari wakaanza kusema mkataba wake na Universal umevunjwa as if VEVO ni kitu very special kwenye mikataba ya UMG!
 
Project ambayo nina uhakika Kusaga alikuwa na mkono wake ni Chibu Perfume. Kuhusu Karanga, ndo vile tu watu hatutaki kuukubali ukweli mchungu hususani kama unamhusu mtu ambae usingependa awe!!!

Diamond ameshakuwa brand ambassador wa kampuni mbalimbali na pia ameshahusika kwenye utangazaji wa bidhaa mbalimbali!

Je, umeshawahi kuona product yoyote akiipigia debe kama ilivyo kwa Diamond Karanga tena kwa muda mrefu hivi?! Na kwa mtu kama Diamond, kama suala ingekuwa ni kutangaza tu, and nothing less nothing more, hivi sasa Smart ingekuwa wameshamalizana na Diamond kwa sababu tayari Diamond Karanga inafahamika kila pahala!!

Sasa ya nini waendelee kuingia gharama za kumlipa kwa product ambayo tayari imeshafahamika wakati mtu mwenyewe ni very expensive!!

Au hivi tunaamini kabisa kwamba Smart wange-take risk ya kumpa mkataba mrefu kutangaza kitu kama karanga?!

Ninachotaka kusema hapa ni kwamba, the guy ana share yake pia pale na sio mtangazaji wa biadhaa kama ambavyo alikuwa anatangaza Chill Source!

Angalia hata kasi ya Joti katika utangazaji wa Joti Chipsy Snacks za hao hao Smart na kasi ya Diamond katika utangazaji wa zile karanga!!

And remember, hata siku aliposema amechomoa kusainiwa na Jay Z, watu humu JF walikejeli kweli kweli kwamba jamaa anapenda kiki na wakaja kunayamaza zilipotangazwa habari za kusainiwa na Universal!!

Lakini maajabu ya watu, ile kuwepo VEVO tu tayari wakaanza kusema mkataba wake na Universal umevunjwa as if VEVO ni kitu very special kwenye mikataba ya UMG!

Ila pia inawezekana kabisa kupewa pesa kila mwezi kama ilivyo kwake na wengi duniani.. hata kama ... imeshajulikana.. mkataba wa kuwa ni kwa muda gani ndio hapo umuhimu kwa wote..

Ila unakubali Clouds wamekuwa nyuma yake na hata hao mameneja bado wanafanya kazi nao hata kuonekana kama juzi hapa Nairobi na Joseph.
 
Diamond kwa upande mwingine anapoteza fans kwa tabia yake ya kuwa na wanawake mbalimbali.. anashangaza kutokujua kujiendesha kimaisha hata kama ndio anapenda kuwa na wanawake kila siku. Halafu anafata walio na majina ambao hawamuongezei kipato.. badala hata ya kujipatia wanawake walio wa kawaida sana.. na kuyafanya kimya kimya.
Hahahaaa,diamond naye ni rijaliii,wanawake wengi wanamfata fata na kumtega,sasa akishakula mavuno.Wanaona ndo muda wa wao kukua kistaa sasa.Hebu muone huyo Dada Hamisa tu,sa hivi kawaida staa mara10, na anajivunia kabisa bila aibu kuzaa na chibu.Na haya mambo hata kwa mastaa wakubwa yapo huko duniani.So ndo ajali zenyewe hizo.Kama mtu ataona ufans wake umefika mwisho basi anaacha tu anakaa pembeni au kujiunga na ile team HATERS siyo na CEO wa kudumu mradi tu use against na MONDI
 
Alishuswa Sugu aliyeanzisha Hiphop..
Alishushwa TID aliyekuwa nyota hatare..

Ashindikane Diamond..

All in All hakuna anayetaka kumshusha kaona yemwenyewe anashuka anasingizia watu wanataka kumshusha..
Unafananisha mlima na kichuguu weweee,hebu kaoge aisee upo analogies nn
 
Asee team dimondo give us a break khaa. Ruge ameshawasikia
 
Back
Top Bottom