Uchaguzi 2020 Hivi upinzani ukichukua nchi Vyombo vya Habari na Wasanii wa Tanzania watakimbizia wapi nyuso zao?

Uchaguzi 2020 Hivi upinzani ukichukua nchi Vyombo vya Habari na Wasanii wa Tanzania watakimbizia wapi nyuso zao?

Sasa imekuwa rasmi wasanii hasa wanamuziki na tasnia karibu zote nchini wanamuunga mkono Rais. Hii sio dhambi, lakini pale msanii anapoimba nyimbo kupondea upinzani kana kwamba upinzani umeletwa nchini na shetani inashangaza sana...
Tangu gondwe ma muro na yule wa kisarawe na emanuel guhogela ateuliwe na rais kuna baadhi ya waandishi wa habari na wasanii wanawivu sana mdio maana wanajitahidi kujipendekeza
 
Tangu gondwe ma muro na yule wa kisarawe na emanuel guhogela ateuliwe na rais kuna baadhi ya waandishi wa habari na wasanii wanawivu sana mdio maana wanajitahidi kujipendekeza
Upumbavu sana kuitupa taaluma yake kisha unaliamuru tumbo likuongoze
 
Kura ni siri haijalishi CCM wana wanachama wangapi wanafuatwa na nani,wote hao ni wapiga kura na mara hii nakuhakikishia wafuasi hao wanafanya maamuzi magumu mbele ya sanduku la kupigia kura,wanaweka na kulinda uwanachama wao, ila kura mwaka huu wanaipeleka upinzani,kura ni siri hapa wenye viti na meza wa CCM wanalijua hilo,na wao kwa umoja wao maamuzi magumu wanajua vipi wanayapitisha,wanamwacha bashilu na polepole kupiga gitaa kumpigia mbuzi.

Nakuambia haludishi mtu kadi ya CCM ila badiliko la kuikataa CCM ni pale anapotumbukiza kura yake akijua ndani ya moyo wake mabadiliko ni lazima na mabadiliko hayo si ya hadharani ni siri bila ya kuharibu mlo wake,Wewe ulisikia wapi mtu kukamatwa kwa kuipigia CCM kura ya hapana ?Wapi ? Mwenyekiti wapi ulisikia?

Ulichokiona ni wale walioikataa CCM hadharani wakiandamwa hadi wanaamua kurudi eti nyumbani,mwaka huu wanaccm wanaikataa CCM kwenye sanduku la kura sio hadharani tena. Wala usiogope utajulikana hata ukijulikana CCM itakuwa umeshaiondoa sumu yake.
 
Sasa imekuwa rasmi wasanii hasa wanamuziki na tasnia karibu zote nchini wanamuunga mkono Rais. Hii sio dhambi, lakini pale msanii anapoimba nyimbo kupondea upinzani kana kwamba upinzani umeletwa nchini na shetani inashangaza sana...
Wanatunga nyimbo za kuwasifia na kuandika ccm
 
Sasa imekuwa rasmi wasanii hasa wanamuziki na tasnia karibu zote nchini wanamuunga mkono Rais. Hii sio dhambi, lakini pale msanii anapoimba nyimbo kupondea upinzani kana kwamba upinzani umeletwa nchini na shetani inashangaza sana...
Katika watu nimewaona Ni hovyo Sana Ni wana habari nyundo inayompondea upinzani ndiyo hiyo hiyo inatumika wapondea Wana Habari lakini wanajifanya hawalioni hilo kweli mungu anawaona na ipo siku wataumbuka
 
jamani Kuchukua Nchi sio sawa na kuchukua Jimbo, Nchi ni jambo jingine kabisaaaa
 
Mnavionea bure, hakuna atakayewalipia faini wakurusha mikutano ya Chadema, TCRA na ccm ni waangalifu sana inapokuja swala la vyombo vya habari kwenye upinzani.
 
Mnavionea bure, hakuna atakayewalipia faini wakurusha mikutano ya Chadema, TCRA na ccm ni waangalifu sana inapokuja swala la vyombo vya habari kwenye upinzani.
Sasa wakiamua kwa umoja wao kususia habari za Magufuli watalipishwa fine?
 
Kwani Simba ikishinda Mashabiki wa Yanga huenda wapi?.
 
Sasa wakiamua kwa umoja wao kususia habari za Magufuli watalipishwa fine?
Watafungiwa kwa miaka 5 na zaidi, na wanaweza wasipate usajili tena.

Muandishi gani anaweza kugoma au kususia kuandika habari za Magufuli?!
Hukuwaona jana kwenye press ya Polepole wamebanana, na wamenuna lakini wapo tu.

Usicheze na vitisho vinavyohusu kula ya mtu, waache uandishi halafu waishi vipi?!
 
Back
Top Bottom