Hivi urafiki wangu na wewe, unaletaje mazoea kwa wanangu?

"Huyo mtoto kakiacha sehemu si salama kikaibiwa!". Kama kiliibiwa shida iko wapi! Ampe hicho kitu chake kilichobaki.
 
We Mtanzania, haya maneno ulimwambia muhusika ama unamuogopa? Huyo mwanao ana umri gani mpaka kuja kusahau kitu cha thamani hivyo? Inawezekana jamaa ana malengo mabaya kwani si kawaida mtu mwenye akili timamu kufanya haya kwa mtoto, usikute jamaa anamjengea mazingira ya uaminifu ili hapo baadaye aje kula tunda kimasihara. Chunga sana urafiki wa namna hii.
 
"Huyo mtoto kakiacha sehemu si salama kikaibiwa!". Kama kiliibiwa shida iko wapi! Ampe hicho kitu chake kilichobaki.
Kitu gani ampe? Kwanini amwachie mtoto wakati kaja kauliza baba yuko wapi kamwambia hayupo? Kwanini akuondoka?
 
Badalisha heading huo sio urafiki bali tafuta neno lingine maana maelezo yako yanaonyesha hamna mazoea ya muda mrefu (how come awe rafiki yako maana rafiki ni neno la thamani sana)
 
Mimi hapo nimeishampa red card!
Nyumbani kwako alipajuaje mpaka kuingia ndani? Ulimkaribisha? Mimi kwenye mambo ya urafiki niko very strict, katika maisha yangu nina marafiki, ambao kwa sasa ni family friends, 2 . Hao tumetoka mbali sanaa tokea chuo, kazini and many others. Hawa ni zaidi ya ndugu, lakini the rest sitaki mazoea.
 
Unataka msaada wa mawazo alafu mambo unayaficha ficha, sasa kuna maani gani ya wewe kuomba msaada wakitu ambacho huwezi ukaeleza kwauwazi mtu ajue anakusaidia vipi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…