Hivi uzuri wa kocha wa Yanga Mwinyi Zahera ni upi ?

Hivi uzuri wa kocha wa Yanga Mwinyi Zahera ni upi ?

Mwinyi Zahera anazingua. Hawezi kutupangia wachezaji wabovu kama akina Ali Ali halafu tutegemee kupata matokeo mazuri.
 
Yanga ikiendelea kubaki na kocha huyu isiposhuka daraja itakuwa ajabu sana !
 
Huwa wanaposema simba ni mbumbumbu basi bila shaka mtoa mada anathibitisha hilo.Sema kwanza ubovu wa zahera ni upi na ndipo uulize ni kwa nini Yanga wanaendelea kumshikilia.sasa unamtuhumu zahera halafu hujaona kosa hata moja kwake.
Kuna mmoja alianzisha uzi kuhusu eti Zahera havai mavazi anayotaka yeye huku alifananisha na wa simba lakin sa simba juzi kaka benchi na jinsi.sasa simba sijui mnakwama wapi?
kama huna cha kuandika sio lazima uandike uzi ili uonekane umeandika.kaa kimya tu maana mpira ni data na fact wewe unaleta umbumbumbu kweli Rage hakukosea.
Mimi nimegundua uzuri wa Zahera ni ile michirizi utamu ya nyuma ya magoti ndo maana anapendelea sana vipensi... hahaha
 
FB_IMG_1572947314940.jpg
 
Tunamtakia kila la heri huko aendako, tunamshukuru sana kwa kuivusha timu yetu salama hadi kushika nafasi ya pili msimu uliopita baada ya mwalimu wa timu wa wakati huo (George Lwandamina) kukimbia.

Tutamkumbuka kwa kutusajilia wachezaji wengi wabovu na wa kawaida, huku akiwafungulia mlango wa kutokea baadhi ya wachezaji wazuri na muhimu kwenye timu.
 
Timu ya Yanga imewahi kuwa na na Makocha wengi sana wazuri kabisa na walioipa mafanikio makubwa sana timu hii , ikiwemo kubeba vikombe kadhaa lakini hawajawahi kusifiwa kama anavyosifiwa huyu kocha mbovu asiye na mafanikio yoyote aitwaye Mwinyi Zahera , hajawahi hata kubeba kikombe cha kunywea kahawa .

Amewapa nini wanayanga huyu mcongo ? au ni kweli kwamba Wacongo wanatumia ndumba kupumbaza wengine ? Huyu kiuwezo yuko nyuma mno kumlinganisha na Kataraiya Minziro lakini sifa anazopewa hata Man U hawakuwahi kumpa Alex Ferguson .

UPDATES
.................
View attachment 1254584
😂😂😂
 
Back
Top Bottom