Hivi vikundi ni hatari sana kwa afya

Lycaon pictus

JF-Expert Member
Joined
Jan 31, 2021
Posts
9,189
Reaction score
16,128
Marekani watu huwa hawali vikundu vya kuku. Sasa makampuni ya nyama za kuku yakaonelea kuwa kuvitupa ni hasara kubwa. Yakatafuta soko. Yakapata soko huko visiwa vya Samoa. Kwa miaka na miaka Samoa ikawa ndiyo wateja wakubwa wa vikundu kutoka Marekani.

Hivi vikundu vinakafuta mengi kupita kiasi. Hakuna sehemu ya kuku yenye mafuta kama hivyo na ni moja ya sababu Wamarekani walikataa kuvila. Ulaji wake husababisha uzito wa kupitiliza kwa kasi sana. Leo hii Wasamoa ndiyo watu wanaongoza kwa unene duniani na serikali yao inajitahidi kupiga marufuku uingizaji wa vikundu. Ni vidude hatari sana na bahati mbaya vimejipatia sana umaarufu maeneo ya uswazi.
 
Nilidhani kichwa cha uzi kimekosewa.Ndiyo,uzi nao una kichwa.🙏😜
 
Mimi nilipo soma haraka haraka nikajua inacho elezewa ni VIKINDU ya Kule kuelekea KISEMVULE....
 

Aisee
 
Mimi pasipo kula hicho kitu naona kama sijakula Kuku, hua naanza na hicho ndo vingine vifuate. Kwa ambao hamjawahi kula yaani ni kitamu balaa
 
Mbagala vinaaitwaa ngongingo

USSR
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…