Hivi vitabu wanavyotumia watoto wetu ni tatizo sana

Hivi vitabu wanavyotumia watoto wetu ni tatizo sana

Kama nilivyoandika hapo juu, mtaani kumejaa watu wengi wasio na ajira, kinachofanyika ni kuchangamkia fursa mkono uende kinywani.... mwisho wa siku ndio hayo matango pori yanatengenezwa.
Kabisa yaani Sasa hivi watu wanaangalia pesa Kwanza, ubora haupo kabisa
 
Safi. Baadhi Vitabu vya MEP hasa darasa la sita viliondolewa na TET katika matumizi kwa sababu ya makosa mbalimbali kama hayo.
Ahaa, shukrani kwa taarifa ila vip kwa madarasa mengine maana kuna shule nafundisha hivo vitabu vipo sana tu.
 
Ndio ni mwalimu
sawaa ila usijisumbuw sanaa.. subir next month kama utapanda daraja au la! acha kuwaza mambo yao!. walimu wengi tunafikiria sana kazi kuliko ata maisha yetu!
 
Walimu wengi magumashi huwa wanajiongeza na kujichapishia tu vitabu ili wawapige wazazi.
Unaweza kuta hapo katumia google translator kutengeneza hilo jedwali
 
Nilikuwa namfundisha mtoto wa sister mara nikafika kwenye jedwali hilo hapo chini, Sasa kila nikitafuta majibu naona chenga,dah sijui ni mimi kilaza au kitabu ndio kina shida?

Kama kitabu ndio kina shida kwanini hivi vitabu vipo mashuleni?

View attachment 1818330

Unaweza kuona aliyeandika hicho kitabu ana degree! Elimu sasa imekuwa changamoto sana nchi hii!
 
Kabla sija jibu. Nikuulize kwani wewe una taaluma ya ualimu?

Match the vocabulary in Column A with its coresponding meaning..... na wala siyo .... with their coresponding...,
Kweli mwandishi huyu ni kenge tu.
 
Ukistaajabu ya Mussa...

Mkuu hayo mambo yapo sana tu kwenye elimu yetu (vitabu) tunakumbana nayo sana tu kuanzia maudhui maana sarufi maumbo mpaka miundo

Halafu kuna mtu hapo anauliza mwenzake kama ni mwalimu ama laa! Kama alikusudia kumcrash mwenzie kuhusu kutoa msaada wa kimasomo kwa (kufundisha) mpwa wake basi nimwambie tu kuwa jukumu la kuelimisha watoto (jamii) si la mwalimu pekee bali ni la taifa kwa jumla mimi wewe na yeye, tofauti ni kwamba kila mtu atacheza na kiwango awezacho na kama tuonavyo hoja ndo hiyo iko clear kabisa jamaa wala hajaenda (hajampeleka dogo) chaka
 
Back
Top Bottom