Hivi vitu ndio vilinifanya nigome kutoka Jiji la Dar es Salaam

Acha ujinga, ulaya, Asia majiji asilimia kubwa yanajitegemea, karibu kila jiji lina viwanda, International airports, vyuo vikuu, na huduma nyingine nyingi, kama bandari nk mfano Bandari ya Liverpool, manchester nk, nimetolea mfano tuu wa mpira, kibongo bongo ni Simba na yanga tuu za Dar es salaam, wakati wenzetu kuna liverpool, Man united za nje ya london ambazo ndio kubwa pale,

kingine hilo gap la shanghai na Beijing au Mumbai na Delhi ki population nk sio sawa na Dar na Mbeya, ebooo
 
Unafananisha London mji wenye population ya almost million 10 na hivyo vimji vya Liverpool na Manchester serious
 
Watu wa arusha ule uvaaji wenu sasa[emoji3][emoji3][emoji3][emoji119][emoji119][emoji119]
 
Wasanii wengi sana wa mikoani walikuja kupata umaarufu tanzania nzima baada ya kuja dar.....kupigiwa ngoma zao redioni
 
Ndio shida ya kua na jiji moja nchi nzima

Yote haya ni by design,hujatoa msimamo wako kutokana na upenzi wa moyo wako,by design ni effect ya kua na sehemu moja tu yenye hadhi ya jiji kwenye nchi,hivyo best life inapatikana sehemu moja tu hakuna kwingine.

Kwenye nchi wangefanya balancing,pwani jiji moja central jiji moja,north jiji moja,south jiji moja na west jiji moja.Haya majiji yawe na hadhi moja,yenye nguvu moja yasipishane....

Shida iliyopo ni nchi nzima kukimbilia Dar es Salaam,maana hakuna majiji yenye hadhi sawa ku absorb these extra people....

Ni kama China kona zote za nchi kuna majiji yenye hadhi sawa,central Beijing,Pwani kuna Shanghai,south kuna Guanghzou,west kuna Urumqi,etc...Majiji yote yanameza idadi sawa za watu na opportunities ni sawa...

Tukiendelea hivi itafika kipindi Dar itameza nusu ya population ya Tanzania na the rest isambae mikoani put together...Yaani Dar imeze 30mil and another 30mil ibakie mikoani kote kwa pamoja,hiyo ni stupidity na inequality ya ajabu..

Nchi haina jiji jingine ukiacha Dar.....itafika kipindi kila anaetaka kuhamia Dar akate passport maalumu,otherwise urudi ulipotoka maana jiji halitaweza ku handle population kubwa hivyo,infrastructure hazitaweza,jiji litavunjika na ku collapse!
 
Mkuu hapo south tu majiji kiboa Yana hadhi sawa ila bongo nimzunguka IL dar hakuna hata inafika nusu kwa ule ukweli hapo Kenya wanatushinda mombasa ni sehemu ya biashara kwa vile Kuna bandari, Nairobi napo ni mji mkali sana kwa biashara pia ila njoo bongo dar ndo kila kitu bandari kubwa, airport kubwa, kila aina ya huduma ipo
 
Kwani uko ilipo hakua mitumba classic au kwanini wanawake wa mikoani hawajui kuvaa utakuta wana vaa magauni makubwa .
Magunia makubwa ndo nini? Acha kashfa.... mitumba ipo ila sio ya viwango au sio mingi kama Dar.
 
Kenya wamebalance vizuri.....Coast wana Mombasa ina hadhi nearly Nairobi

Central ndio wana Nairobi kama Nairobi

West wana Kisumu walao inasaidia kupunguza wakazi...

Shida ya Tanzania Dar ni too big yaani jiji linalofatia ni Mwanza ambayo GDP yake Dar imeizunguka mara tatu...what a joke!

Effect yake kila mtu anataka kuja Dar....infrastructure haitatosha kabisa...kuzuia itabidi waweke kipande system,kwamba anaetaka kuhamia Dar akate kipande au passport maalumu..Ukihamia kienyeji hutaweza kupata huduma za kijamii kama shule,etc maana huna kipande.Hii walifanya China miaka ya 80 maana walikua na Jiji moja tu lenye hadhi Shanghai.

Yaani Dar inabeba wakazi nearly 10mil,ni kama 20% ya population yote ya TZ.....na wanaongezeka....jiji la Mwanza linalofatia eti lina 1.2mil,what an imbalance aiseee?

Hili ni bomu halafu wanasiasa hawalioni.....

Yaani ni shida mpaka serikali kuhamia Dodoma bado ni mtihani,effect ni hii...waweke infrastructures watu watahamia...hela ndio hakuna!
 
Yaani we acha tu!! Dar imekuwa ndo kila kitu mavyuo yote huko soko kuu huko Ina hadhi tofauti na majiji mengine wala hamna uwiano.
 
Mkuu ulichoandika una uhakika nacho? Nina evidence za kutosha kuhusu waliozaliwa na kukulia Dar na kugoma kwenda mikoani
Na mimi nina evidence za kutosha za watu waliokulia na kuzaliwa dar ila hawapataki mpaka likizo wanapita mbio mbio mji vurugu tupu kila kitu shida tu
 
Magunia makubwa ndo nini? Acha kashfa.... mitumba ipo ila sio ya viwango au sio mingi kama Dar.
Wanawake na wanaume wa mikoani wanavaa manguo makubwa, Wanawake wavaa magauni makubwa
 
Ripoti ya repoa inaonesha asilimia 85 ya vijana wa Dar wanaishi kwa kipato cha chini ya laki tatu.
 
Unaelewa maana ya harakati? Wapi nimetaja fly over au bahari...jikite kwenye point mkuu...sehemu rahisi kutoboa ukiwa na connection sahihi ni DSM...na DSM ndo Tanzania mzee...[emoji3][emoji3][emoji3][emoji3]
You are right,huwa nikiwa natoka mkoa nawaaga watu kuwa naenda Tanzania [emoji137]
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…