Hivi vitu ndio vilinifanya nigome kutoka Jiji la Dar es Salaam

Pamoja na hizo sifa ila Dar ndio Jiji linaongoza kuwa na ufirauni,maisha ya hovyo na kuwa na maskini wengi sana hapa Tanzania..

Kwa misingi hiyo hilo Jiji lilinishinda kiukweli na ambavyo watu ni wengi hadi Kero tupu..
Lete data hapa.
 
Hapana Dar haijafika ten milioni. Iko approximately five milioni
 
Hapana Dar haijafika ten milioni. Iko approximately five milioni
Mkuu

Dar inakaribia 10mil

5mil ilikua 2015.....

Gets your facts right.

10mil ni 20% ya population ya Tanzania nzima

Dar will break down,haina infrastructure ya kubeba watu kiasi tunachoenda.....
 
Mzee toa uzoefu wako kwa vijana wapate Darasa naamini utakuwa umetembea na kuishi mikoa tofauti.
Rizki inatafutwaa popote hata nje ya nchi kwahiyo msikibali kubali dsm tuu hata kama mambo hayajakunyookea.
 
Nikweli unezunguja nchi na dar ni baba lao kwa sababu asilimia 85 ya uchumi unatoka dar ila kila sehemu ni nzuri kuishi endapo mipango yako ya uchumi itafanikiwa na mtu husifia pale panapompa ugali wa kutosha huwezi kumwambia mtu wa mchimboni kahama eti dar panafaa ndio kila kitu ahamie huko wakati yeye anachimba dhahabu tu sasa dar akachimbe chokaa au mlina asali wa tabora ahamie dar
 
Wanaofatia baada ya dar (mwanza) hawabishani ila sasa hawa… au basi

Anyway kazi ipoo🥱[emoji81]
 
Hakuna harakati zozote dar zaidi ya udalali usitupige kamba, karibu chuga mkuu.
 
Dar itabaki kuwa jiji kuu la kibiashara na sababu ziko nyingi na wala sio jambo baya lakini hii ya watu kukimbilia Dar lilijengwa na siasa miaka ya nyuma ilikuwa hata passport lazima uende Dar mikoani ulikuwa hupati au ni shida watu walinyimwa hizi fursa kusudi na serikali ili wa control kila kitu lakini athari zake zinaonekana leo sasa nini kimefanyika, Mji mkuu umehamia Dodoma kwa hiyo shughuli nyingi zimehamia lakini pia na mifumo ya electronics siku hizi unapata sehemu yoyote na huduma zinasogea kwa watu ndio maana leo tunaambiwa kwa mara ya kwanza airport ya Zanzibar imeipiku Dar kwa kupokea watu na leo hii ndege nyingi zinaenda Kilimanjaro direct kama Qatar, Ethiopia na mashirika mengine leo Dar airport ukishuka kimyaa sio kama miaka ya nyuma, na hili la train na bandari kavu kama Dodoma na Isaka siijui litapeleka huduma sehemu nyingi na kufungua fursa. Hakuna ubishi Dar ni jiji kubwa sababu ziko nyingi sana kila mtu anajuwa kwanini lakini kesho bandari ya Bagamoyo ikikamilika sehemu ya cake itaondoka Dar na watu wanajazana sehemu sababu ya fursa na naona Bagamoyo itakuwa hivyo. Dar imenufaika sana siku za nyuma kisiasa kuwa kila kitu lazima uende Dar hata signature tu utaitafuta Dar ila haya yanabadilika taratibu mwisho wa siku makampuni yanatizama gharama za uendeshaji nafuu kwa Dar ilikuwa imepata bahati hiyo ila haya taratibu yatabadilika na yameanza ila naamini Dar itabaki kuwa lango kuu la kibiashara kuna miaka Zanzibar ilikuwa inakuja juu lakini maamuzi ya kisiasa yalifanywa kuimaliza ili Dar ibaki juu kutambulisha double taxation. Nchi ina watu mil 60 lazima kuwe na sera kupeleka fursa sehemu tofauti ili maendeleo yaende kila sehemu na hili kidogo linafanyika. Ila Dar kuna population kubwa sana ni kama wasindikizaji tu wanaishi maisha duni sana tena sana na wako asilimia ndogo wameshika uchumi. kuhitimisha Dar ni jiji la biashara na litabaki hivyo kitakachotokea tu wale waliokuwa nyuma wataanza kupunguza kidogo kidogo kutoka Dar sababu za sera za serikali kuhama itachukuwa muda ila watu watazoea na hii SGR na bandari kavu kama waliuvyofanya Kenya Naivasha na Mombasa wakaanza kulia ndio yanakuja sababu Bandari kavu kuwa kati ya mji mawakala watakuwa pale ni copy paste ya Mombasa na Naivasha... hitimisho Dar itaendelea kuwa#1 ila wengine fursa zitafunguka....
 
Watu hawaelewi ni nini maana ya capital city
 
Subiri waje washamba wa Arusha wanavyotoa povu
Mshamba wa AR chuga niko hapa.Hebu njoo nikupeleke kwa Mromboo.Huku sisi hatuuzi nyama kwenye vijiti ni kwa kilo halafu upaki hilo gari lako kizembe hapo Dar tunalileta huku tunalichinja au ndani ya saa moja unaweza kutana na gari yako na usiijue.
 
Boban wewe ni member maarufu group hili ila rafiki yangu hiyo namba 3 angalia itakutia umasikini na life span yako itakuwa fupi take care
 
Kuna mdogo wangu ni mwalimu hapa Dar anafanya private school wanamlipa 1m zilivyotoka ajira za serikali akaomba na akapata akapangiwa Nachingwea vijijivi huko ndani ndani kabla ya kwenda akaja kuniomba ushauri kwamba aende au aache. Nilimwangaliaaaaa nikatamani nimnase kibao ni vile tu ni mtu mzima mwenzangu.

Yani umekaa Dar more than 6 years ulishapata mguu wa kukanyagia una kibanda chako tayari alaf et unataka kwenda kuajiriwa na serikali huko Lindi huko kwa mshahara upi? Kwa maisha gani ya walimu?

Dogo nilimwambia yani kama kuna mistake utafanya ulaumiwe mpaka na vizazi vyako ni kupaacha Dar alaf uende huko Lindi. Jipange hapahapa mjini tengeneza chanel alaf uone Dar ilivyo rahisi. Dogo alinielewa na saiz naona maisha yameanza kumnyookea
 
kuna baadhi ya watu wanaishi tofaoti na dar mashi yao mazuli watoto wao wanasoma shule nzuli maisha safi kupata akuchagui wapi utapatia kama dar ujawekeza chochote bora usiishi kwenye mji huo masikini wanateseka sana
 
masiki wa dar anashida nyingi sana ila kwa alie wekeza yuko vizuli
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…