Hivi wabunge wa CCM mnajisikiaje, wananchi hawafuatilii Bunge wanafuatilia kesi ya Mbowe?

Hii thread ndio imenijulisha kuwa Bunge lipo live.
 
Kwanza hawataki tukicheki bunge live eti Nape alisema nimuda wa kazi.
Marudio tukawa hatuangalii maana nimuda wa mapumziko
 
Hata wabunge wenyewe wengi wapo kule kwa sababu ya kutakiwa kuwepo na kupata posho,lakini kiukweli hata wao wapo kule kimwili Ila mawazo na akili zao zipo kwenye kesi ya Mbowe. CCM wanaujua ukweli mchungu huu kuwa Mbowe kasingiziwa Ila hawana pa kusemea.
 
Kumbe Bunge linaendelea?
 
Kwani Tanzania tuna bunge ?
 
Mimi ni CCM eroo sioni wanaotuwakilisha wanachokifanya. Maendeleo hayana chama
 
Dhambi ya usaliti au kushuhudia uongo ni mbaya sana ndio maana hata vitabu vitakatifu vimeilaani sana.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…