Hivi Wachagga wanacheza soka? Nimewahi kuwasikia akina Mwakalebela, Minziro, Masatu lakini siyo Massawe au Mushi!

Hivi Wachagga wanacheza soka? Nimewahi kuwasikia akina Mwakalebela, Minziro, Masatu lakini siyo Massawe au Mushi!

johnthebaptist

JF-Expert Member
Joined
May 27, 2014
Posts
97,869
Reaction score
171,716
Naelewa kabisa michezo iko mingi kama darts, karats, nao, kukimbiza kuku nk ola kwenye kandanda Wachagga hawaonekani sijajua kwanini.

Nimewahi kuwaona akina David Mwakalebela, akina Minziro akina.Masatu na hata.Kibaden Mputa lakini sijamuona Massawe Mushi wala Kavishe

Hata kule Upareni hakunaga wasakata kabumbu

Why?
 
Watakuwepo mkuu, mfano yupo mkongwe Leodegar Tenga.
Tena alicheza akiwa meneja wa Landrover Tanzania Ltd akiwa na digrii ya uinjinia

Sema wachaga wengi hupenda kushika pesa kila siku aone hela inaingia mkononi
.Hizo pesa za kusubiri hadi msimu wa ligi uanze hawataki.Wanaona bora wachome nyama chuma!!

Kuna utani pia wanasema huwezi kuta bendi ya wachaga sababu waliwahi kuunda bendi ya wachaga watupu kuanzia wapiga vyombo na waimbaji nk na wakaagiza vyombo vya gharama Ulaya na wakafanya mazoezi ya nguvu

Ugomvi ukaja wakati wanajadili nani akae mlangoni kwenye ukumbi watakapokuwa wanaimba atakayekuwa anapokea pesa za viingilio.Kila mwana bendi akawa anataka akae yeye mlangoni apokee pesa za viingilio.

Hakuna aliyetaka kupanda jukwaani kutumbuiza .Kila mmoja haamini mwenzie kukaa mlangoni kupokea pesa za viingilio.

Bendi ikavunjika wakauza vyombo vya bendi wakagawana pesa kila mtu ajijue !! Ndio ukawa mwisho wa Chaga Jazz Band na haijawahi anzishwa tena!!!
 
Naelewa kabisa michezo iko mingi kama darts, karats, nao, kukimbiza kuku nk ola kwenye kandanda Wachagga hawaonekani sijajua kwanini...
Ila wewe jamaa una wawaza sana wachaga na Chadema! Mada zako nyingi ni kuhusu Chadema na Wachaga!

Mbona hujatolea mifano ya wanyalukolo wenzako waliowahi kucheza/wanaocheza mpira, kabla ya kukimbilia kwa Wachaga? Au nyinyi fani yenu ni kunywa tu ulanzi na komoni?
 
Unawajua Wana Paluhengo Lipuli FC?

Unacheza soka kisha unajipoza na Bamboo juice!
 
Kwa kweli hawawezi kuwa kama kina Ronaldo na Messi etc, kuwa unafanya kitu chenye short life span halafu unagain/unakuwa tajiri for the rest of your life span.
Nimependa sana ulivyo comment yani umeona mbali sana.uko Very Visionary Brother.
Haya sasa tuambie mchezaji gani wa kitanzania unaweza kumchukulia kama aliyefanikiwa kimaisha kupitia mpira.... Mjumuishe na Samatta kabisa.
 
Tena alicheza akiwa meneja wa Landrover Tanzania Ltd akiwa na digrii ya uinjinia

Sema wachaga wengi hupenda kushika pesa kila siku aone hela inaingia mkononi
.Hizo pesa za kusubiri hadi ligi hawataki.Wanaona bora wachome nyama chuma!!

Kuna utani pia wanasema huwezi kuta bendi ya wachaga sababu waliwahi kuunda bendi ya wachaga watupu kuanzia wapiga vyombo na waimbaji nk na wakaagiza vyombo vya gharama Ulaya na wakafanya mazoezi ya nguvu

Ugomvi ukaja wakati wanajadili nani akae mlangoni kwenye ukumbi watakapokuwa wanaimba atakayekuwa anapokea pesa za viingilio.Kila mwana bendi akawa anataka akae yeye mlangoni apokee pesa za viingilio .Hakuna aliyetaka kupanda jukwaani kutumbuiza .Kila mmoja haamini mwenzie kukaa mlangoni kupokea pesa za viingilio
Bendi ikavunjika wakauza vyombo wakagawana pesa kila mtu ajijue !! Ndio ukawa mwisho wa chaga jazz band na haijawahi anzishwa tena!!!
Wachaga sio watu[emoji23][emoji23]
 
Unawajua Wana Paluhengo Lipuli FC?

Unacheza soka kisha unajipoza na Bamboo juice!
Basi wataje kwanza hao wachezaji wa hiyo Lipuli ambao ni Wanyalu, kabla ya kuhamia kwa wachaga.

Na usije siku nyingine kuuliza tena kwa nini hakuna Wamasai na Wabarbaig wengi wanaocheza mpira wa miguu!
Jibu jepesi, ni kwamba; hizo jamii zimewekeza nguvu zao nyingi kwenye ufugaji, na pia maisha ya kuhamahama! Na siyo kwenye mpira.

Kama ilivyo kwa wachaga! Wengi wamewekeza zaidi kwenye elimu ya watoto wao na pia biashara. Wachaga siyo kama watu wa pwani, ambao muda wao mwingi wa jioni, vijana hutumia kwenye michezo.
 
Back
Top Bottom