magnifico
JF-Expert Member
- Jan 14, 2013
- 11,075
- 24,634
Oya Oya huyo. Muulize akicheza Senegal na Algeria anashangilia timu ipi na kwasababu zipi utasikia majibu yake.Ulisikia wakitamka hayo maneno? Au na wewe umewekewa caption na wabongo ukaingia mkingi bila kufanya research!
Sisi tunaona sawa tukisema Yanga atacheza na Waarabu, Ila Al Ahly akisema anacheza na Watu Weusi inakua nongwa. Hatujawahi kuwa proud kabisa na rangi yetu.
Angalia saizi Algeria anafikiria kujitoa CAF kisa upendeleo kwa Morocco ila angalia wanaongoza kwa kumshambulia ni Watu Weusi. Hata kureason anachopigania Algeria mtu mweusi kashindwa. Wamebaki kumuita Mbaguzi. Huyo Algeria moja ya uwanja wanaochezea timu ya Taifa unaitwa Nelson Mandela. Jenga bongo ita jina la Mwarabu uone moto wake.
Sikatai Waarabu ni wabaguzi kama zilivyo races zote ila mtu mweusi sio tu mbaguzi bali pia ni mbinafsi.
Akisikia mtu mweusi kapewa uongozi pale London anakenua meno yote, ila huku akipewa Bongo Zozo hakuna rangi ataacha kuiona.