Miongoni mwa vitu ninavyovishangaa ni hiki kitendo cha kukubali mchezaji kugawa jezi yako yenye jasho lako kwa mchezaji mwenzako kwa kigezo tu cha kukubali uwezo wako.
Kiuhalisia miongoni mwa silaha kubwa mtu akitaka akumalize kabisa (akuroge) kiurahisi basi akipata nguo ambazo umeshazivaa ,lile jasho lako ni silaha tosha la kukumaliza kishirikina.
Japo nguo ya ndani ni silaha kubwa zaidi lakini pia nguo nyingine yeyote yenye jasho lako mtu akiipata anakutengeneza vizuri tu.
Ndio maana utakuta mchezaji kawika ndani ya muda mfupi tu kisha nyota inazima au kupata majeraha ya mara kwa mara ambayo yanamfanya kukaa nje ta uwanja kwa kipindi kirefu .
Shitukeni nyie watu kama mlikuwa hamjui.