Hivi wadau mtu kuwa mnene sababu huwa ni nini je ni urithi au ni kula sana?

Hivi wadau mtu kuwa mnene sababu huwa ni nini je ni urithi au ni kula sana?

Unene asilimia kubwa unachangiwa na vyakula Ila wapo baadhi ni issue ya kurithi.
 
Hakuna unene wa kurithi, Uliona wapi Mababu (ancestors) zako wakiwa Wanene?

Unene unatokana Ulafi wa vyakula na vinywaji & Uvivu/Uzembe.

Ulafi & Uvivu/Uzembe ni mojawapo ya Cardinal sins.
 
Hakuna unene wa kurithi, Uliona wapi Mababu (ancestors) zako wakiwa Wanene?

Unene unatokana Ulafi wa vyakula na vinywaji & Uvivu/Uzembe.

Ulafi & Uvivu/Uzembe ni mojawapo ya Cardinal sins.
Wapo watoto wamezaliwa mabonge mkuu
 
Wapo watoto wamezaliwa mabonge mkuu
Hakuna Mtoto anazaliwa mnene/bonge, labda useme wapo watoto wanazaliwa na uzito kuwazidi watoto wengine.

Mtoto anakuwa bonge/mnene kulingana na vitu anavyolishwa baada ya kuzaliwa.
 
Siyo kweli Kuna vimbau mbau vinafukia msosi balaa
Kuna unene wa aina mbili Kiongozi.

1. Unene unaonekana kirahisi huu Mtu anakuwa na mafuta kwenye tissues mbalimbali (zionekanazo) ambao hupelekea kuongezeka uzito usio salama na unatambuka kama Obesity, ndio unaojulikana na watu wengi.

2. Unene ambao hauonekani kirahisi huu Mtu anakuwa na mafuta kwenye tissues za ndani kama vile Ini na maeneo mengine ya ndani, Inatambulika kama TOFI (Thin Outside Fat Inside) ndo hao unawaita vimbaumbau.

Aina ya pili ni hatare zaidi kwani ni rahisi mtu kufikiri yuko fiti kwakuwa ni kimbaumbau au sio mnene lakini ndani ni pamoto na hana ufahamu.

Pia kuna watu kama unavyosema wanafukia balaa lakini bado ni vimbaumbau, wengine kazi za kimetaboliki za miili yao ni kubwa. Huwezi kujilinganisha na mtu ambae mwili wake upo active muda mwingi ( mtu wa kazi kazi), lazima anachokula kitumike kiongozi hapo ndo Linakuja swala la Uvivu/Uzembe. Unakula muda wote msosi wa kutosha halafu hautumiki unategemea Mwili ufanyie nini kama sio kuhifadhi kama Mafuta?
 
Back
Top Bottom