Hivi wafanyabiashara wenzangu, mliwezaje kudeal na mpinzani wako ambaye kakuzidi kila kitu!

Jig
Jifunze kuwa Bora ktika huduma na kauli pia jaribu kuweka bei rafiki kujenga jina taratibu ili nawe uwe na wateja wako wa kudumu.
 

Kwanza napenda kukupongeza kwa hatua uliyofika ya kuwa na biashara yako kutoka kufanya biashara za watu. Lakini napenda pia kukupongeza kuwa ujue biashara haina ujanja, wala huyo jirani yako sio kuwa anafanya uchawi wala nini, usije kudanhanywa ukaenda kwenye ushirikina.
Yeye kuwa na wateja sio ajabu kwakuwa yuko siku nyingi na anajuana na wateja wengi. Unachotakiwa kufanya wewe ni kuanza kujifunza sehemu ya kupata biadhaa nzuri na kwa bei nafuu ambayo wewe ukija kuuza usitake faida kubwa sana, ni bora upate faida ndogo uuze sana kuliko kusubiri faida kubwa ukauza kidogo.

Angalia sana na epuka madalali, jaribu kununua kwa mkulima mwenyewe. Biashara ni changamoto kikubwa kila siku jifunze kupunguza hasara na uwe rafiki wa wateja wako, ifike sehemu akija kwako anatakani kununua kwako na awe tayari kukusubiri kama umefunga duka, hakuna ujanja hapo.
 
Sawa ila hata mimi huu si mwezi wa tatu ila bado ngoma ngumuu, halafu soon tu natakiwa kulipa kodii afu hata faidaa haijaingia daah

Sikiliza, usikate tamaa.. akili yako ijikite katika kutafuta mbinu za kuboresha biashara yako, weka vitu extra ambavyo jirani hana, pata bidhaa nzuri zaidi uuze kwa bei iliyo rafiki kwa wateja wako, ikiwezekana uwe na variety ya mchele kwa kila kada ya wateja.
Mbona mapema, watu wanalipa kodi mara mbili kabla ya kuanza kuona faida.... uwe mvumilivu.
 
Kitu Cha kwanza kwenye biashara Ni position yaani biashara ilipo. Cha pili Ni position.
Cha tatu nidhamu na kuweka sura ya tabasamu hasa kwa wateja wa kike.
Cha nne. Unakonunulia mzigo.
 
Mzee pole kwa changamoto unazopitia mim mwenyew nauza mchele jumla nipo Mbeya ukitaji mchele mzuri , wakati unaweza nicheck PM
 
Una mawazo ya kibeki tatu, yawezekana hujawahi uza hata nyanya za gengeni.
Hakuna biashara ambayo washindani hawajifanyii evaluation na kujipima kulingana na market na industry. Na hiyo haiitwi wivu wala kijicho.
Sawa boss, nimekusoma
 
Big point brooo ila na kwenyew kununua moja kwa moja kwa mkulima ni mtihani kwa sabb kila mashine akienda tiyar kuna madalali wapo hapo
 
Mzee pole kwa changamoto unazopitia mim mwenyew nauza mchele jumla nipo Mbeya ukitaji mchele mzuri , wakati unaweza nicheck PM
Shida mim wateja wang wa kitonga. Mbeya bei zenu zipo juu sana mimi michele yang ya 1000, 1100, 1200, je unayo michele ya hio bei
 
Kitu kingine madalali ndo wanafanya biashara ionekane ngumu hasa wa morogoro ifakara wana tamaa kila mashine utawakuta wapo hapo mpka wanakela mchelee wanauza bei kubwa ukilinganisha na anayouza mwenyewe mkulima
 
aBuwash kwanza nakupongeza kwa kujiongeza, pili nakushauri ubadili mindset yako kuhusu mpinzani wako kibiashara, huyo sio mpinzani ila naye ni mpambanaji anafuta maisha kama wewe tu.
Ongeza ubunifu ktk bishara yako, ubora wa bidhaa zako, tafuta chimbo ambayo utaipata products kwa bei ndogo then uuze kwa faida bila kuathiri faida yako.
Focus na kuongeza ubora na huduma kama kuwa free delivery kwa maduka ya rejareja na offer kwa mamanitilie wanaonunua mchele kila siku n.k. In short kuwa positive na achana na kushinda na mtu usiyemjua.
 
Kitu kingine madalali ndo wanafanya biashara ionekane ngumu hasa wa morogoro ifakara wana tamaa kila mashine utawakuta wapo hapo mpka wanakela mchelee wanauza bei kubwa ukilinganisha na anayouza mwenyewe mkulima
Tafuta connection na wakulima, wenye mashine ili kuwaepuka madalali.
 
Lakwanza kabsa anza kwa kuchunguza jiran yako wateja wake anaishi nao vp, je bei zake vp je quality ya mzgo wake vp

Lapili jipe mda kua mvumilivu
La tatu acha kuangalia wengne jipange na biashara yako kla mtu na njia zake zakufanya biashara
Umenena vema mkuu
 
Umesema jirani yako ana muda mwingi katika biashara hiyo halafu unapànic kuona ana wateja wengi.
Jamaa anaonekana hana uvumilivu wa biashara,pili hakujipanga kufanya utafiti wa kutosha kuanzia bei za kununua shambani na bei za kuuzia sokoni.
Kitu kingine alikuwa anawaza akianza tu apate wateja wa ghafla na kupiga faida kitu ambacho hakipo kwenye biashara.
Kitu kingine anawatam
Uko sahihi.
Watu siku hizi wanauza kisomi.
Zama za kukaa dukani unangojea wateja wa kubahatisha zimepitwa na wakati.
Kwa mfano kuna jamaa yetu mmoja ni school mate wetu anauza biashara kama hiyo ya nafaka kwa jumla na rejareja yeye huwa anatutangazia kwenye magroup yetu ya whatsapp ina maana kila mwezi ana uhakika wa kupata wateja 10 kutoka kwenye group letu la whatsapp baada ya hapo akienda kuwatangazia wenye migahawa akiwapata watano basi biashara inaenda hata kama hajapata wateja wapya.
Cha msingi mtoa mada ajipange kutafuta wateja wake kwa kutumia hizi mbinu asiangalie au kuwatamani wateja wa mpinzani wake pengine aliwaandaa kwa muda wa miaka 10 hatoweza kuwahamisha kirahisi anavyodhani.
 
Ushauri huu nami nimeuchukua
 
Nina simu mbovuu haichukui kamera vizurii ndo maana nashindwa kujitangaza kweny mtandao
 
Nina simu mbovuu haichukui kamera vizurii ndo maana nashindwa kujitangaza kweny mtandao
Sio lazima kwa simu.
Kwenye mtaa unakoishi hakuna wamama wanauza migahawa?anza nao hao kuwashawishi kwa bei na ubora wa bidhaa yako yaani kwa mfano ukimpa punguzo la shilingi 200 tu kwa kila kilo moja maana yake anajua akinunua kilo 10 kwako ataokoa shilingi elfu 2 lazima aje kununua kwako.
Haya majirani zako unakoishi hawapiki mchele?watembelee mmoja mmoja na kuwaonyesha sampo ya mchele wako ukiwatangazia watu 10 kuna uwezekano mkubwa wa kuwanasa angalau watatu na wengine watakupa ahadi za siku zijazo.
Biashara ni kujiongeza ndugu ukisubiria ufundishwe kila kitu utachelewa sana kufanikiwa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…