Hivi wafanyabiashara wenzangu, mliwezaje kudeal na mpinzani wako ambaye kakuzidi kila kitu!

Shukraniii sana mkuuu
 
Nitafute niwe nakuuzia mahindi na maharage kutoka shamba moja kwa moja kwa bei nzuri achana na madalali watakumaliza!
 
Kwanza, atoe punguzo la 200 p/kg wakati faida p/kg ni 180. Unataka apate lose?

Pili, kwa miaka yangu 31 sijawahi kuona mfanyabiashara akija kugonga kwetu na baadae kwangu akiomyesha sample ya mchele ili tukanunua dukani kwake.

Hizi biashara za mitandaoni kuna watu mnafanya zionekane ni ujinga.
 
Ngoja nikufundishe polepole utaelewa inavyoonekana wewe una uwezo mdogo wa kujiongeza unaishi kwa kukariri,ukishaona kichwa chako kipo hivyo wewe hufai kuwa mfanyabiashara maana biashara haikubembelezi ukibweteka utaa
mbulia sifuri na wenzako wanauza kama kawaida.
Haya chukulia mama ntilie alikuwa ananunua mchele kwa mangi kwa bei ya 1800 kwa kilo moja wewe unaenda kumwambia nitakuuzia kwa 1600 hii nayo hadi upelekwe shule kujiongeza?
 
Apunguze shilingi 200 kwa kilo?
Sasa mzee narudia kuwaambia kile ambacho huwa nasema humu JF. Ukiona muuza mchele anapata faida 200 kwa kilo ujue huyo ni gangwe kwenye field. Kama zingekuwa ndege hapo tunawataja Boeing na Airbus.

Hiyo ya majirani kununua mchele ni ngumu na hata wakinunua si ni kilo mojamoja sasa hiyo iendeshe duka. Ila kuhusu mamantilie hao almost kila muuza mchele mwenye akili timamu huwatafuta. Ila kwa taarifa tu hakuna watu wababaishaji na wapuuzi kama mamantilie. Yaani mnadai mafundi wa kibongo wababaishaji? Wajaribu mamantilie wa mtaani uone. Unaenda kudai hela yako anakuonyesha sufuria la wali ambavyo haujaisha anadai atauza kiporo kwa hasara.

Nimekumbuka jinsi nilivyotumia jumuiya na waumini kuuza mchele wangu. Mama yangu ni mtu wa kanisa alinitafutia wateja uko nikawakopesha, pia jumuiya yetu huwa siwakwepi hivyo walinunua sana.
Nilikuwa na kama tani moja ya kutest mitambo hapo soko la Tandika wamenipa bei ndogo sawa na niliyonunulia.
 
Mchele ambao bei ya sokoni ni 1800 na wewe ukauuza 1600 maana yake unafanya charity na wala hufanyi biashara. Its either wewe ni NGO au ni idara ya serikali una ruzuku na una msamaha wa kodi na tozo na unatoa huduma sio kupata faida. Tofauti na hapo hii kitu sio realistic kwenye industy ya mchele.

Profitability ya mchele ni max. 200sh/kg. Akipunguza 200 anaondoa maximum profit, sio minimum wala average, maximum my friend! Maximum yenyewe anaweza kuwa hajawahi ipata tangu aanze ukute anachezea kwenye net profit ya 100sh/kg (kawaida kabisa).
 
Hapo mwanzon nilikuwa siwajui wateja wang ila kwa sas nimejua wateja wang ni watu wa halii ya chini kwaiyo wanapenda mchele kitonga lakini pia uwe mzuriii ko nazanii asaiv nitaenda moja kwa moja mashineni na kuwachukulia mchele wanaohitajii

Mkuu mtoa mada kuna mahali amekiri mwenyewe kuwa wateja wake wanapenda bei za kitonga hana namna ni lazima aangalie jinsi ya kupunguza bei hata kama sio 200 niliyoitaja hapo kama mfano.
Halafu mkuu kwenye biashara nyingi za kitanzania bei ndio kigezo namba moja na hapo ndipo uchawi wa biashara ulipo.
Labda nikuulize swali moja wewe hujawahi kuona au kusikia mtu kaenda china kufuata mzigo kaumwaga kariakoo halafu baadae anagundua kuwa bei wanayouza wapinzani wake ni sawasawa na bei aliyouziwa china?Sasa jiulize wamenunua wapi bidhaa,
Sasa kwenye biashara yoyote ukiweza kufanya haya maajabu kwenye bei basi jua wewe tayari umeshatoboa na utajiri unapiga hodi
 
Hizo boiashara ulizosema hazina ushindani, unajijengea hisia zisizo kuwepo.

If you can't win them join them.
 
Ishu ni kuamini katika mungu ndumba sio nzuri mfanyabiashara mbaya analoga ila mfanyabiashara mzuri anaomba na kusali katika imani yake karma is a biitch kama umemkuta kaanza kabla yako jifunze kwake kama mko sawa mshauriane
 
Nawatamani sana wateja wa jumla ila wanataka mchele mzuri halafu kwa bei mteremko bila kujua mimi nakochukua nachukua bei kubwa
Jaribu kuweka dogo au mke dukani wewe mwenyewe nenda shambani kwa wakulima wenyewe. Usichukuwe kwa dalali wengi wao wapo kimaslahi tu sio kibiashara
 
Hama eneo
 
Huu mstari wa mwisho ndo umebeba mafanikio YA Biashara huwez fanikiwa Biashara kama spiritually una mikosi Na nuksi laana
 
Pole sana, wafanyabiashara wengi hawajiendeshi kwa kudra za Mungu pekee...


Cc: Mahondaw
 
Pokea maua yako brooo hiko kitu ndicho nachopitia mimi asaivii naenda shamba hukohuko ila bei kule sawa na mjini tu
 
Pokea maua yako brooo hiko kitu ndicho nachopitia mimi asaivii naenda shamba hukohuko ila bei kule sawa na mjini tu
Hapo ndipo ufundi na uchawi wa biashara ulipolala na hawawezi kukupa hiyo siri hadi siku umpate mtu wako wa karibu sana kisha akuonee huruma ndio atakupa hiyo siriπŸ˜„πŸ˜„πŸ˜„πŸ˜„πŸ˜„πŸ˜„
 
Hapo ndipo ufundi na uchawi wa biashara ulipolala na hawawezi kukupa hiyo siri hadi siku umpate mtu wako wa karibu sana kisha akuonee huruma ndio atakupa hiyo siriπŸ˜„πŸ˜„πŸ˜„πŸ˜„πŸ˜„πŸ˜„
Dah nahangaika sana mwezi wa tatu huu nimeagiza trip 4 na zote nimekula loss nauza kwa bei ambayo soko linahitajii ukisema uweke faida yako huuzi hupatiii wateja mpka inafikia stage nataka kukata tamaaa aisee. tena muda mwingine unaenda shamba unarud na mchele uuze labda 1500 afu unakuta wafanyabiashra wengine mchele unaotaka kuuza 1500 wao wanauza 1300 mpka unajiuliza hawa watu wanachukua wapiii mzgo naumiza kichwa mamamke hadiii nahisii kuumwa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…