Hivi walioanzisha utaratibu wa mwanamke kulipiwa mahari walikuwa na sababu gani za msingi?

Anhaa kumbe inawezekana nafikiri itakuwa njia njema kuonesha utu kwa mabinti zetu na kuacha utamaduni wa udhalilishaji
Unakomplicate mambo sana. We fanya unaloona ni sawa boss.
 
Unakomplicate mambo sana. We fanya unaloona ni sawa boss.
Nimecomplicate ki vipi mwanangu.
Tujitahidi kufungua vichwa vyetu kuwaza vitu hata ambavyo ni tamaduni na mazoea ambayo yapo yapo pasipo kujua kwa sababu gani za msingi kwa nini yapo.

Tunapo hoji kuhusu masuala fulani tunapata uelewa mkubwa tofauti na awali
 
Reactions: Tsh
mi naona mahari ifutwe ili twende sawa na ile 50/50
Utaitwa marioo, utaambiwa tafuta hela, utaambiwa wewe mwanaume dhaifu unakwepa majukumu. Linapokuja suala ambalo linamuingiza gharama au linamuweka hatarini mwanaume hawa wanawake hawataki kabisa 50/50
 
50/50 sio kwenye uchumi tu dada angu. Kuna vipengele vingi sana. Mfano vitani ni wanaume tu ndio wanaenda kwenye batle field tukisema na wanawake waende matari wa mbele vitani mpo tayari?, mkiachana mnagawa mali tukiweka 50/50 kila mtu achukue alichokitolea jasho mpo tayari?, bungeni kuna viti maalumu kwa ajiri ya wanawake tukisema tuondoe zile nafasi hamtalalamika?
 
Kwenye vita sio lazima ni hiyari.
Pia kimaumbile mwanamke hawezi kupigana vita kama wapo basi ni wachache.

Viti maalum mimi sikubaliani navyo. Wanawake wapewe nafasi kutokana na uwezo wao, bila upendeleo wowote. Sina tatizo.
 
Mkuu, kwani wewe ungekuwa Mwanamke ungekataa kulipiwa MAHALI ??

Samahani lakini[emoji3578]
 
Kwenye vita sio lazima ni hiyari.
Pia kimaumbile mwanamke hawezi kupigana vita kama wapo basi ni wachache.

Viti maalum mimi sikubaliani navyo. Wanawake wapewe nafasi kutokana na uwezo wao, bila upendeleo wowote. Sina tatizo.
Ndo hapo ujue 50/50 haiwezi kuwa practible. By any means lazima mwanamke awe chini ya mwanaume iyo ndio nature
 
Mbona Kuna jamii wanaume ndio wanalipiwa?ni utaratibu tu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…