Hivi wana Msimbazi wenzangu mnaliona hili gharika linalokuja?

sembo

JF-Expert Member
Joined
May 25, 2011
Posts
4,350
Reaction score
3,451
Sijui kama wanazi wenzangu wa Msimbazi mnaliona hili naloliona. Baada ya Simba SC kufunga goli 38 katika msimu uliopita, ambayo ni chini ya goli 2 kwa kila mechi, huku washambuliaji tegemeo wakishindwa kufikisha angalau goli 10 tu kwa msimu.. Uongozi umecharuka na kuamua kufanya yafuatayo msimu huu;

1. Kuondoa Waliotuangisha.
Hapa kuna Dany Serunkuma na Elias Maguli ambao tuliwaamini saaana.. hawa jamaa katika nafasi 7 za kutupia kambani walizopata kila mmoja [jumla 14], walifanikiwa kufunga goli 1 kwa pamoja.. Hili suala kwa timu ya kariba ya Simba SC haliwezekani pia halikubaliki hata kidogo, na ndio mana funguo ya kufuli la mlango wa kutokeo iliwahusu.. na sasa wapo wakitafuta maisha mapya.

2. Kuleta Makocha wa Kariba ya kufundisha timu za UEFA CL.
Hapa namzungumzia Dylan Kerr [Holder wa UEFA Licence Grade A] ambae pia ni beki katili kuwahi kutokea Uingereza.
Kuna kocha wa viungo Momclovic [Huyu jamaa anaheshimika sana Ulaya ya Mashariki]. Kazi kubwa ya Kerr kwa sasa ni kuinoa safu ya ushambuliaji ili iweze kukabiliana na mabeki katili wa kariba yake.. Huku Momclovic akiwajenga fiziki washambuliaji ili waweze kukabiliana vyema na mabeki visiki kama wale wa Ruvu Shooting iliyoshuka daraja.

3. Kufanya Usajili wa Nguvu.
Simba ya sasa ipo hivi.. mchezaji anayesajiliwa lazma apite mizani ya Mtalamu Kerr.
Kuna straika ambao wamefuzu, nao ni Dany Lyanga, Mgosi na Kiiza.. Kuna waliofeli nao ni kama Papaa Niang.. Pia wapo ambao tomu zao zilitaka dau kubwa Mf. Mavugo na Ndayisenga.. Japo kuna vizingiti vingi sana, nasikia kua uongozi haujakata tamaa kutafuta 20+ goal holder straika.. na nasikia kuna washambuliaji hatari sana wawili wanatua leo kwenye chujio la Kerr, na wote hao wanatoka katika ligi za wanaojua.

4. Kuwaleta Watalamu wa Kupiga Pasi Za Mwisho.
Hapa tumeletewa, Mwinyi Kazimoto a.k.a Pass Master [kama huamini muulize Juma Seif Kijiko, anaijua shughuli yake].
Pia kuna "fundi" Majabvi toka Zimbabwe [kutokana na kabumbu anavyolisakata, kwao anaitwa "icon of zimbambwe"].. Pia kuna "mchawi" wa kupiga pasi toka Mbeya, Peter Mwalyanzi.. Sasa kwa midfield hii kwanini kina Ajibu wasiwe wanaondoka na mipira yao baada ya kufunga hat-trick?! Nitashangaa wakitoka bila ya mipira yao uwanjani.

5. Kuutoa Mvinyo wa kale Sandukuni.
Kuna stori zilizagaa mitaani kua wachezaji vijana wa Simba Sc wamekua wavivu sana mazoezini, pia hawajitumi katika mechi.. Uongozi uliliona hilo, ukaamua kuwaletea "natural born leader" a.k.a "mvinyo wa kale" a.k.a "uncle" Musa Hassan Mgosi ili awafundishe kitu.
Alipotua tu akakabidhiwa kitambaa cha u keptein. Mgosi amekua mfano wa kuigwa ndani na nje ya uwanja kwa vijana, pia anawaongoza vyema sana.. Sasa zile stori kua vijana hawajitumi hazipo tena.. Simba SC sasa ni "Nguvu Moja".. Na hii imekuja kutokana na chachu ya "uncle" Mgosi bila kuwasahau watalamu Kerr na Momclovic.

Wahenga, walishanena..

"usiruhusu adui yako, azifahamu silaha zako mapema".

Aminini nachowaambia, kilichotokea katika mechi takribani 8 za kirafiki ni rasha rasha.. mvua kamili inakuja..
Hifadhini kauli yangu.

Ni mimi sembo toka Simba TV, kuwaleteeni habari.
 
Nilikuwa mchezaji wa Simba Kids chini ya Marehemu "Baharia" na Msaidizi DENNIS "mmasai"..... niliipenda Simba SC toka moyoni.... nikaanza kukatishwa tamaa na maendeleo ya timu yangu (kama huko ulaya na liverpool) nikaacha kwenda kiwanjani kushuhudia mechi na mazoezi (maana yalijaa maumivu na presha za kufungwa) Lakini kwa mleta mada hapo juu anataka kunishawishi nirejee katika upenzi wa soka letu....hasa timu yetu ya Msimbazi
 
Duh, Sembo hii sasa sifa. Saa tisa usiku unaiwaza Simba? Ama kweli unaipenda hii klabu
 
Nilikuwa mchezaji wa Simba Kids chini ya Marehemu "Baharia" na Msaidizi DENNIS "mmasai"..... niliipenda Simba SC toka moyoni.... nikaanza kukatishwa tamaa na maendeleo ya timu yangu (kama huko ulaya na liverpool) nikaacha kwenda kiwanjani kushuhudia mechi na mazoezi (maana yalijaa maumivu na presha za kufungwa) Lakini kwa mleta mada hapo juu anataka kunishawishi nirejee katika upenzi wa soka letu....hasa timu yetu ya Msimbazi

Daaah hivi kumbe "baharia" alishatangulia mbele za haki? RIP baharia
 
Nilikuwa mchezaji wa Simba Kids chini ya Marehemu "Baharia" na Msaidizi DENNIS "mmasai"..... niliipenda Simba SC toka moyoni.... nikaanza kukatishwa tamaa na maendeleo ya timu yangu (kama huko ulaya na liverpool) nikaacha kwenda kiwanjani kushuhudia mechi na mazoezi (maana yalijaa maumivu na presha za kufungwa) Lakini kwa mleta mada hapo juu anataka kunishawishi nirejee katika upenzi wa soka letu....hasa timu yetu ya Msimbazi

Mkuu karibu tena, mambo mazuri yanakuja.
 
Jamani mpira hautabiriki bado mapema sana, tuivumilie timu yetu ila kiukweli inakatisha tamaa hadi basi, tusiikimbie jamani hakuna ajuae kesho itakuwaje.
 
Mkuu katika mechi 8 za kirafiki tulizocheza kwa ajili ya kujiandaa na msimu mpya, tumeshinda mechi 7 huku tukisuruhu mechi 1.
Kwa matokeo hayo, lazima kesho yetu iwe nzuri..
 
Mi nashangaa watu wanakata tamaa tu, mim naamin msimu huu watakuwa vizuri.
 
Msimu huu unaokuja, amini Simba SC inakuja kivingine.. Hao waliokata tamaa tutakutana nao katikati ya ligi baada ya kushinda mechi tano mfululizo, Yanga wakiwa wahanga wamojawapo.
 
Kila kukicha mambo yanazidi kunoga watani wajiandae mwaka huu wetu msimbazi

Haha.. Baada ya Mechi ya kuwania Ngao [sijui ya kuwania mkuki watacheza lini?!], kati ya Ndala na Lambalamba.. Mtalaamu sana toka Uingereza, Dylan Kerr.. alitoa kauli moja tu HAWATUFUNGI.. hapo kawakusanya wote.. Hivyo Mkuu, kuhusu watani, ondoa shaka.. VIPIGO ni stahiki yao msimu ujao.
 
Mkuu katika mechi 8 za kirafiki tulizocheza kwa ajili ya kujiandaa na msimu mpya, tumeshinda mechi 7 huku tukisuruhu mechi 1.
Kwa matokeo hayo, lazima kesho yetu iwe nzuri..

Miaka yote simba hufanya vizuri mechi za maandalizi..
 
4. Kuwaleta Watalamu wa Kupiga Pasi Za Mwisho.
Hapa tumeletewa, Mwinyi Kazimoto a.k.a Pass Master [kama huamini muulize Juma Seif Kijiko, anaijua shughuli yake].
Pia kuna "fundi" Majabvi toka Zimbabwe [kutokana na kabumbu anavyolisakata, kwao anaitwa "icon of zimbambwe"].. Pia kuna "mchawi" wa kupiga pasi toka Mbeya, Peter Mwalyanzi.. Sasa kwa midfield hii kwanini kina Ajibu wasiwe wanaondoka na mipira yao baada ya kufunga hat-trick?! Nitashangaa wakitoka bila ya mipira yao uwanjani.

Aminini nachowaambia, kilichotokea katika mechi takribani 8 za kirafiki ni rasha rasha.. mvua kamili inakuja..
Hifadhini kauli yangu.

Ni mimi sembo toka Simba TV, kuwaleteeni habari.

Mkuu sembo umenena kweli kabisa! Mechi za majaribio ilikuwa hivi: Simba 0-0 Mwadui FC, hii ndiyo rasharasha! Kinachokuja mbele yenu ni African Sports 3-0 Simba katika mechi ya ufunguzi, hiyo ndiyo masika!

Poleni sana mikia.
 
Last edited by a moderator:

Mkuu naomba nikupe taarifa Simba SC imeshinda mechi 7 mfululizo, kabla ya kudraw na watoto wa Mgodini.
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom