BigTall
JF-Expert Member
- Mar 9, 2022
- 525
- 1,257
Kwa sasa Dar es Salaam ni kama imeanza kutikisika, haijafikia kiwango hicho lakini kiuhalisia kuna mambo hayako sawa hasa yanayohusu ulinzi.
Hawa vijana wa Panya Road sijui niseme wanachekewa au mamlaka hazijapata jibu hasa la kudili nao, wenyewe mamlaka za ulinzi zinajua zinachokifanya.
Juzi hapa wametutangazia wamewakamata zaidi ya 100, kesho yake wanafanya tukio Kawe na kuua mtu, je kilichokuwa kinafanywa na mamlaka ni siasa au kweli waliwakamata.
Na wale wengine wanaokamatwa siku za nyuma wanazotutangazia ni kweli wanahukumiwa au ndio inakuwa zuga ili ionekane mambo yameenda?
Anyway, hoja yangu ya msingi pia leo ni kuhusu hizi taasisi zinazojiita zinatetea haki za binadamu, mbona sizioni zikipiga kelele wala kusema lolote!
Ajabu sana huu, hizo haki za binadamu wao wanaziona kwenye masuala ya Sheria pekee? Watu hasa wa ngazi za chini wanavyoteswa na Panya Road kwao siyo haki?
Najua hawawezi kuingia mitaani wao kupambana na Panya Road lakini kama wanaamini sauti zao huwa zinasaidia kwenye suala la malaka kuamka na kuzingatia haki za binadamu kuhusu jambo fulani, mbona sasa hivi hawaamki na kusema kitu?
Au Panya Road kuua, kupora na kujeruhi watu siyo haki za binadamu?