Hivi wanafunzi wengi wanaopata ufaulu mkubwa, huwa wanakwenda wapi?

Hivi wanafunzi wengi wanaopata ufaulu mkubwa, huwa wanakwenda wapi?

Hamza Nsiha

JF-Expert Member
Joined
Jul 25, 2022
Posts
221
Reaction score
197
Ndugu, mwanajamii Forum, hili swali nimekuwa nikijiuliza mara nyingi hivi ni kwanini wanafunzi wengi waliowahi kuingia katika orodha za wanafunzi bora mara nyingi baada ya hapo huwa hatuwasikii tena katika kuendeleza jitihada zao hususani katika safari yao ya elimu.

Mfano, baadhi ya wanafunzi waliowahi kuwa Tanzania One (TO) kidato cha sita, huwa hatuwasikii tena wanapoenda vyuoni. Kwa maana wanafunzi hawa ndio walitakiwa kuwa vinara katika kutia chachu katika sekta ya elimu kupitia jitihada zao au mawazo yao pia lakini si hivyo maana wengi wao wanapoenda vyuoni safari yao huwa tofauti.

Kama mwana Jamii Forum unahisi hiki kitu hutokea kwa sababu gani?

Nimewaandikia pia uzi uitwaio "vita ya vijana dhidi ya maendeleo ya sayansi na teknolojia" kama kijana unaweza pitia kuona tunamaliza vipi vita iliyopo baina yetu.
 
Wewe unawataka ili nini ni sone point wako tu kama watu wa kawaida.Mimi nawajua wengi ni malecturers wapo kwenye vyuo mbalimbali nchini na duniani .Waliobahatika kipaata scholarship wengine wameishia huku huko nje ya nchi nk
Hao unao sema kuwa ni ma lectures wengi wao ni wale wanaofanya vizuri vyuoni ambao hata ukifuatilia nyuma hawakuwahi kuwa katika orodha ya wanafunzi bora. Ninazungumzia hawa TO katika elimu ya kidato cha nne na cha sita. Asante kwa jawabu pia.
 
Yaani unataka uone nini cha ajabu kuwahusu? Upishane nao barabarani wakiwa wamepakwa rangi au? Wapo wanaendelea na maisha yao.
Hawa ni watu muhimu sana waliotakiwa kuwa ktk mstari wa mbele kuboresha baadhi ya mambo kupitia maarifa waliyojaaliwa. Mfano wakina Isaack Newtons ndio waliokuwa vinara katika kuboresha misingi ya kifizikia akina Nichole Tesla na wengine wengi hivyo tunahitaji mchango wao maana wanaweza kuleta mabadiliko chanya. Asante kwa jawabu pia
 
Yaani unataka uone nini cha ajabu kuwahusu? Upishane nao barabarani wakiwa wamepakwa rangi au? Wapo wanaendelea na maisha yao.
Hawa ni watu muhimu sana waliotakiwa kuwa ktk mstari wa mbele kuboresha baadhi ya mambo kupitia maarifa waliyojaaliwa. Mfano wakina Isaack Newtons ndio waliokuwa vinara katika kuboresha misingi ya kifizikia akina Nichole Tesla na wengine wengi hivyo tunahitaji mchango wao maana wanaweza kuleta mabadiliko chanya. Asante kwa jawabu
Kukariri darasani na kutoboa kwenye maisha ni vitu viwili tofauti.. wengi tupo nao kitaa tu
Mh! Pia inaweza kuwa sababu mkuu! Asante kwa jawabu pia.
 
Hao unao sema kuwa ni ma lectures wengi wao ni wale wanaofanya vizuri vyuoni ambao hata ukifuatilia nyuma hawakuwahi kuwa katika orodha ya wanafunzi bora. Ninazungumzia hawa TO katika elimu ya kidato cha nne na cha sita. Asante kwa jawabu pia.
Mwanzoni kipindi mie nasoma,by that time kwenda form one kijiji kizima kinajua wale ma T.O walikiwa wanasomeshwa na Serikali na badaye wanapelekwa kufanya kazi katika sekta Fulani.

Sasa hawa Ma T.O wa Siku hizi wa sijui
 
Wapo

Wengi ni walimu wa vyuo ama wahandisi ama madaktari ama wachumi wako wizara ya fedha pale na wengine wako kwa mwanasheria Mkuu wa serikali wakiendesha kesi za wizi wa kuku, hakimu kuhongwa elfu 50 nk.

Unajua shule na maisha ni vitu viwili tofauti.

Kwenye maisha huku unakuta kinachotawala sio ufaulu tena, ni network.

Mfumo wetu wa elimu pia una changamoto kubwa.
 
Back
Top Bottom