Hivi wanajeshi wa Congo wanajielewa kweli? Yaani wameiacha nchi yao wamekimbilia Rwanda kujificha?

Hivi wanajeshi wa Congo wanajielewa kweli? Yaani wameiacha nchi yao wamekimbilia Rwanda kujificha?

Beira Boy

JF-Expert Member
Joined
Aug 7, 2016
Posts
19,976
Reaction score
32,195
Amani iwe kwenu watumishi wa MUNGU

Nimechoka kabisa jeshi la nchi limeikimbia nchi na kuwaachia wananchi msala

Wanajeshi wa kongo wamekimbilia Rwanda na kupokelewa kama wakimbizi hii ni hatari sana aisee

Screenshot_20250127-224927.png
Screenshot_20250127-224914.png


SAYUNI BOY
 
Amani iwe kwenu watumishi wa MUNGU

Nimechoka kabisa jeshi la nchi limeikimbia inchi na kuwaachia wananchi msala

Wanajeshi wa kongo wamekimbilia Rwanda na kupokelewa kama wakimbizi hii ni hatari sana aisee

SAYUNI BOY
Lilimtoa Mobutu ndio ije huyu,anyway Congo River Alliance ni muungano wa Makundi mengi ya Waasi ambao hawaridhishwi na utawala wa Tshisekedi.

Sasa hivi wanatengeneza Momentum na logistics ili waende all the way to Kinshasa.
Congo River Alliance wamesema wameukaribia mji wa Bukavu halafu Kalemie na hatimae Lubumbashi.
Wakubwa wao wapo dhidi yao,wakitumia silaha kubwa dhidi ya m23,wanapokonywa zinarudishwa kambi zingine,cha kufia nini!?
Hao Waasi wa M23 Wanaungwa mkono na Watu wengi Sana waishio kwenye maeneo hayo yenye migogoro.
Aidha, hata baadhi ya Vigogo wengi sana waliopo ndani ya Serikali ya Congo DR pia wanawaunga mkono hao Waasi wa M23. Hivyo, hao Waasi wa M23 Wana Watu wao ndani ya Serikali ya huko na wamekuwa wakipata taarifa zote kabisa muhimu za kiintelijensia kutoka Serikalini kupitia kwa hao Mawakala wao.
Mbaya zaidi sana, ndani ya Majeshi yote kabisa ya Serikali ya Congo DR kuna Mamluki wengi sana ambao pia ni Wapiganaji wa Vikosi vya Waasi wa M23, that's why unaona kwamba kuna matukio mengi sana ya Uasi wa chini chini ndani ya Majeshi ya nchi hiyo.
Jeshi la Congo DR jinsi lilivyo ni sawa sawa kabisa na jinsi Jeshi la Nigeria jinsi lilivyo. Wanajeshi wengi sana wa Nigeria pia ni Wapiganaji wa Kundi la Boko Haram, na Wanajeshi wengi sana wa Jeshi la Congo DR pia ni Wapiganaji wa Vikosi vya Waasi wa M23.
 
Wanajeshi wa kongo wamechoka hatari Kombat azieleweki na mabuti ya mvua kama wanaenda shamba
Lilimtoa Mobutu ndio ije huyu,anyway Congo River Alliance ni muungano wa Makundi mengi ya Waasi ambao hawaridhishwi na utawala wa Tshisekedi.

Sasa hivi wanatengeneza Momentum na logistics ili waende all the way to Kinshasa.
Wacongo wanajua kukata mauno tu huku nchi yao inateketea.
Siyo kweli kwamba WaCongoman siyo wazalendo kwa nchi yao, la hasha. Kabla ya kuwalaumu hao raia/Wananchi tunapaswa tujiulize: Je, ni kwa nini hasa huko DR Congo Vita na uasi havikomi miaka nenda rudi? Ni hasa kiini au chanzo cha kuwepo kwa huo Mgogoro na vurugu huko DR Congo?

Kimsingi, DR Congo kuna matatizo mengi Sana ambayo yanasababisha hali hiyo ya kuwepo kwa migogoro na Vita isiyokwisha. Kwa kifupi, DR Congo is a failed State! Hakuna Utawala ulio madhubuti nchini DR Congo, Utawala wake unaundwa na Magenge ya Watu wachache Sana ambao umejikita kwenye ufisadi na uporaji wa rasilimali za nchi hiyo ili kujinufaisha wao wenyewe pamoja na Vibaraka wao (wafuasi wao wachache) huku kundi kubwa zaidi la Wananchi wengi zaidi wa nchi hiyo wamebaki kuwa mafukara wa kupindukia. Mbaya zaidi Sana, Utawala wa nchi hiyo unafanya Siasa za Propaganda hatari za Kuwagawa Watu kwa misingi ya Ukabila, Ukanda, Itikadi za Siasa, n.k. Siasa za kuwagawa watu ni jambo baya na la hatari kubwa sana, matokeo yake ndiyo hayo unayoyaona ya Wanajeshi kuasi na kujiunga na Wapiganaji Waasi.
Hata baadhi ya Wananchi wengi waishio kwenye hayo maeneo yenye vurugu na Vita wamekuwa wakiwaunga mkono Waasi wa M23.
 
Back
Top Bottom