Hivi wanajeshi wa Congo wanajielewa kweli? Yaani wameiacha nchi yao wamekimbilia Rwanda kujificha?

Hivi wanajeshi wa Congo wanajielewa kweli? Yaani wameiacha nchi yao wamekimbilia Rwanda kujificha?

Sana...wanajeshi wamevaa yebo na shamba boot.
Very sad. Hawathaminiwi watapataje morari?
Yan unaona bora hata mtu angejifanyia biashara zake tu kuendesha maisha
Hali hiyo ya Wanajeshi kutothaminiwa na Watawala waliopo madarakani pia ipo nchini Msumbiji, ndio maana unaona kwamba Waasi wa RENAMO kule Cabo Delgado waliliteka eneo hilo kwa urahisi Sana bila kikwazo chochote kile
 
Lilimtoa Mobutu ndio ije huyu,anyway Congo River Alliance ni muungano wa Makundi mengi ya Waasi ambao hawaridhishwi na utawala wa Tshisekedi.

Sasa hivi wanatengeneza Momentum na logistics ili waende all the way to Kinshasa.
Hao ni mamluki wa Kagame na jeshi la Rwanda, hamna waasi wenye nguvu kiasi hicho.
 
Huo sasa ndio usaliti at its best! Soldiers ku-side na adui ndilo kosa la juu kabisa jeshi linapokuwa vitani. Na adhabu yake ni moja tu... inajulikana.
Hawa hata kuwapa adhabu ya kifo ni kama kuwaonea tu

Maana watu wenyewe wamejichokea kweli yaan
 
Solution in kuigawa DR Congo kama ilivyotokea kwa Sudan. DR Congo ni chi kubwa sana na kulingana na udhaifu wa serekali yake haiwezi kuitawala nchi yote.
Kuna taarifa (sina uhakika) kuwa kulikuwa na makubaliano kati ya Laurent Kabila, Kagame na Museveni kwamba wamsaidie kumtoa Marshal Mobutu Seseseko then yeye Kabila aatoa pande la ardhi huku mashariki ya Congo kwa ajili ya watutsi. Jambo ambalo Kabila alishindwa kulitekeleza na ndiyo Kagame kwa ushirikiano na Museveni wakaanzisha Kundi la M23 la Laurent Nkunda kwa ajili ya kumtoa Kabila madarakani au kuchukua eno la mashariki ya congo.
 
Siyo kweli kwamba WaCongoman siyo wazalendo kwa nchi yao, la hasha. Kabla ya kuwalaumu hao raia/Wananchi tunapaswa tujiulize: Je, ni kwa nini hasa huko DR Congo Vita na uasi havikomi miaka nenda rudi? Ni hasa kiini au chanzo cha kuwepo kwa huo Mgogoro na vurugu huko DR Congo?

Kimsingi, DR Congo kuna matatizo mengi Sana ambayo yanasababisha hali hiyo ya kuwepo kwa migogoro na Vita isiyokwisha. Kwa kifupi, DR Congo is a failed State! Hakuna Utawala ulio madhubuti nchini DR Congo, Utawala wake unaundwa na Magenge ya Watu wachache Sana ambao umejikita kwenye ufisadi na uporaji wa rasilimali za nchi hiyo ili kujinufaisha wao wenyewe pamoja na Vibaraka wao (wafuasi wao wachache) huku kundi kubwa zaidi la Wananchi wengi zaidi wa nchi hiyo wamebaki kuwa mafukara wa kupindukia. Mbaya zaidi Sana, Utawala wa nchi hiyo unafanya Siasa za Propaganda hatari za Kuwagawa Watu kwa misingi ya Ukabila, Ukanda, Itikadi za Siasa, n.k. Siasa za kuwagawa watu ni jambo baya na la hatari kubwa sana, matokeo yake ndiyo hayo unayoyaona ya Wanajeshi kuasi na kujiunga na Wapiganaji Waasi.
Hata baadhi ya Wananchi wengi waishio kwenye hayo maeneo yenye vurugu na Vita wamekuwa wakiwaunga mkono Waasi wa M23.
Umeshusha madini ya kiwango sana mkuu
 
Kongo ina mapedeshee na matapeli zamana wakiitwa kamanyola. Wangekuwa na jeshi hata robo ya Tanzania, kusingkuwa na upuuzi wa M23 au Rwanda ambao wametengenezwa na M7 tuliyemtengeneza baada ya kumchapa nduli na kumchoka Obote.
Duh

Kwahiyo mseven mumemuweka nyie pale ikulu?
 
Inasikitisha sana
Wanajeshi wanakuwa HAWANA Morali na Hamasa ya kupigana vitani.

Kwanza Mishahara waakati mwingine huwa wanalipwa kwa kuchelewa Sana, na mbaya zaidi wakati mwingine pia huwa wanakopwa na wanalipwa Nusu mshahara. Katika Mazingira mabaya kama haya, ni Mwanajeshi gani hasa ambaye yupo tayari kupigana vita hadi kufa kwa ajili ya kuwatetea Watawala wa nchi wa namna hiyo?
 
Wanajeshi wanakuwa HAWANA Morali na Hamasa ya kupigana vitani.

Kwanza Mishahara waakati mwingine huwa wanalipwa kwa kuchelewa Sana, na mbaya zaidi wakati mwingine pia huwa wanakopwa na wanalipwa Nusu mshahara. Katika Mazingira mabaya kama haya, ni Mwanajeshi gani hasa ambaye yupo tayari kupigana vita hadi kufa kwa ajili ya kuwatetea Watawala wa nchi wa namna hiyo?
Ngumu sana kwakwel. Na una familia ma watu wanaokutegemea.
 
Hao ni mamluki wa Kagame na jeshi la Rwanda, hamna waasi wenye nguvu kiasi hicho.
Waasi wenye nguvu kubwa za kijeshi kiasi hicho wapo, tena wapo wengi sana. Inategemea na aina ya Waasi wenyewe, Mazingira waliyopo, uungwaji mkono, na sababu zingine nyingi sana kama vile 'motives' mahsusi zinazowafanya hao Waasi kupingana na Utawala uliopo.

Uasi wa kupigana HAKI mara nyingi sana huwa unapata uungwaji mkono kutoka kwa Wapenda Haki, hivyo Basi, upo uwezekano mkubwa sana Waasi wa namna hiyo kuwa na Jeshi au Wapiganaji wenye nguvu zaidi kuzidi Majeshi ya Serikali/Watawala. Mfano mzuri kwenye suala hili ni Vita kali ya Kosovo kujitenga kutoka katika nchi ya Yugoslavia. Waasi wa Kosovo walikuwa na nguvu za kijeshi kubwa sana kuliko Majeshi ya Serikali ya Yugoslavia
 
Back
Top Bottom