Hivi wanajeshi wa Congo wanajielewa kweli? Yaani wameiacha nchi yao wamekimbilia Rwanda kujificha?

Huo sio uasi ila uvamizi wa nchi jirani ya Rwanda....Rwanda ina askari 4000+ wanaopigana bega kwa bega na M23 dhidi ya serikali ya Drc

Hata ripoti za UN na nchi kubwa kama US, UK, France wamethibitisha hilo....

nasisitiza uasi wenye nguvu kubwa kiasi hicho haupo Drc.

 
Duh

Kwahiyo mseven mumemuweka nyie pale ikulu?
Ngumu sana kwakwel. Na una familia ma watu wanaokutegemea.
Ndiyo, Yoweri Museven ameingia Ikulu kule Uganda kutokana na kupata msaada mkubwa sana wa kijeshi kutoka Tanzania. Nyerere alimsaidia Sana kijeshi hadi akashinda vita dhidi ya Wapinzani wake,hili liko wazi kabisa.
Watawala wengine ambao pia waliingia Madarakani kwenye nchi zao baada ya kupata msaada mkubwa sana wa kijeshi kutoka kwa Nyerere ni:-
1. Robert Mugabe na Chama chake cha ZANU kule Zimbabwe.
2. Samora Matchel na Chama chake cha FRELIMO kule Msumbiji., etc
 
Hao wanawaza kuimba mziki na kuchubua ngozi za miili yao....pour Congolese!
 
Hao wanawaza kuimba mziki na kuchubua ngozi za miili yao....pour Congolese!
Unawaonea bure kabisa hao Watu.
Je, wewe uko tayari kupigana Vita hadi kufa kwa ajili ya kuwatetea na kuwalinda Watawala waovu, Mafisadi, Wabaguzi na/au Watekaji? Wewe unaweza kufanya hivyo?
 
🤣🤣🤣 dah! Kama hawa ndyo jeshi la Congo hapo hawawezi hata kuongoza kijiji kule mara! Sasa image kama uyo wambele kavaa buti kama anaenda kulima mboga mboga ndyo kwl wapgane na m23! Mm bnafs naona kwl Wa Congo man hawpo sriaz kweny nch yao wakate tu mauno wajinga sana
 
Vita viangalie kwenye Movie tu, ache cheza kwenye PS2 au X Box;
 
Mkuu, Uzalendo ni saikolojia. Mtu kuwa tayari kufa ili wengine wakae kwa amani haitokei tu. Pengine hata wewe pakinuka vizuri hii nchi ukakataa kufa.
Wazalendo wanatengenezwa na viongozi,kama viongozi wote ni wabinafsi hao wazalendo wanatoka wap
 
Reactions: Tsh
Hawawataki walinda amani hawana faida kwao.walisema nchi yao watailinda wenyewe. Sasa Rwanda wamefuata nini? Watapewa chakula na maji waoge wakimaliza wanapewa kombati na silaha wakapigane tena huko huko walikotoka.
 
Huo sasa ndio usaliti at its best! Soldiers ku-side na adui ndilo kosa la juu kabisa jeshi linapokuwa vitani. Na adhabu yake ni moja tu... inajulikana.
Movies zisikudanganye. FARDC hawapewi logistical support na higher command yao, hawana evacuation wakiumia wanaachwa wajifie uko, hawana ammunition supply wakiishiwa walizonazo wanakamatwa bila upinzani kama vibaka, hawana heavy weapons wako almost sawa na M23, hawana intelligence wanapelekwa kama kubeti.

Upande wa serikali haina mwamko inapiga porojo ila vitendo hamna wakati upande wa M23 wako very determined, vigogo serikalini na jeshini hawana maamuzi ya maana.

Kwa wananchi wa Goma na jirani zake ndio kabisa wanaongeza maumivu, wanaitaka M23 kuliko FARDC.

Vitani hupigani kichwakichwa kama mwehu, unapigana na reasoning. Kuna mazingira upigane usipigane hakuna mabadiliko yatatokea na ukipigana una uhakika wa kufa au kujeruhiwa. Pale wamejisalimisha hawajasaliti nchi, kama vipi serikali yao ndio imewasaliti wakakosa option. Pia mji wa Goma uko mpakani kabisa na mji wa Gisenyi wa Rwanda, ule ni mji mmoja wenye jina lake kila upande. Na ni rahisi kutoka Goma kwenda Gisenyi kuliko kwenda sehemu yoyote ya Congo.
 
Kuna maza kwenye News anasema baweke mabunduki chini tuchapane bangumi.Kagame alisema DRC ni puto tu ukilichoma sindano linalipuka naona keshachoma sindamo.
 
Ukiangalia Muonekano wa wanajeshi wa Rwanda & Congo utaona utofauti.

Ni kwamba Congo haiwajali Wanajeshi wake, Na huenda Hata hao wanajeshi hawaelewi wanapigania nn.
 
Yaani ufe kizembe unawapigania watu wako Kinshasa wanakulana uroda?

Nawapongeza Kwa kuokoa maisha yao
 
Wacongo watu wa raha tu.. mambo ya vita ni magumu sana kwao..
 
Wanaonekana kama wanamgambo wasio na mafunzo yoyote Wala vifaa vya kijeshi ona wamevaa rain boots halafu wanakimbilia kule kule nyumbani kwa adui wao
 
Vita ya Kongo imekaa kimtego sana. Kwenye meza ya upatanisho anatakiwa kukaa raisi wa Kongo na Rwanda, na ukumbuke kuwa wanaopigana vita ni jeshi la Kongo vs waasi wa M23.
 
Tangu Enzi za Mobutu Wakongo siyo watu WA kuwaamini hata kidogo...ni watu wasio na discipline, watu WA majivuno na misifa isiyo na maana. Wanapenda sana Raha.. Halafu ni Waongo na rahisi kurubuniwa na kudanganywa. Wewe waangalie wacheza mpira walivyo ..Wakongo ni watu WA hivyo kabisa...Binafsi Wakongo huwa nawaangalia Kwa jicho la dharau kabisa...hawaaminiki, awe ni mwanamke au mwanaume..
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…