Habari za usiku huu wana JF?
Mie wala siyo mwingi wa habari ila nilitaka tu kuwauliza ninyi kaka zetu hili swali kama kichwa cha mada kinavyojieleza hapo juu.
Swali: Hivi, wanaume mnaposema kuwa wanawake wa siku hizi tunapenda usawa huwa mnamaanisha usawa kivipi yaani kwenye mambo yepi haswa?
Swali la nyongeza: Je, mnataka wanawake tusifanye makosa ila wanaume mfanye makosa halafu wanawake tukae kimya tusiwaambie na wala tusiwafanye chochote au mnatakaje?
Naombeni majibu yenu tafadhali na hata wanawake wenzangu pia mnaweza kujibu chochote mnachojua kuhusiana na hayo maswali maana mimi sina majibu kabisa.
Wanawake wengi wa leo wanapemda usawa hasa katika mambo ya ndani...
*kuna baadhi ya wanawake huweza kuwapangia wanaume majukumu kwa mfano, wanawake wengine wanathubutu kumwambia mumewe." leo ni zamu yako ya kumuogesha mtoto.."
* Usishangae mwanamke kumwambia mumewe mmoja apike ugali mwangine apike mboga.
*mmoja aoshe vyombo mwingine apike
* mwanamke anapanga yeye afue, mume atapiga pasi.
* wanawake wa leo wanataka wakorome ndani, mume awe anapikea maagizo tu
Mwanamke anataka akitenga chakula kikishaliwa, mume atoe vyombo...
******wanawake wa leo kwenye tendo wanataka wakae juu, sisi tukae chini..[emoji43][emoji43][emoji43]....binafsi napenda kukaa chini, yeye aje juu..[emoji85][emoji85][emoji85][emoji87][emoji87]
Kwa misingi ya kiafrika, hayo mambo niliyoyaeleza mume anaweza kufanya kama sehemu ya mapezi kwa mkewe, ila kuna wanawake wwngine wanakaza sauti na kugawanya majukumu hayo kwa mumewe..
######Jukumu kuu la mume ni kumoenda mke, watoto na kutimiza mahitaji ya familia mf chakula, kodi, ada n.k...
######Jukumu la mke ni kuhakikisha familia inanufaika kutokana na kile baba aliyokileta, kumsaidia baba kazi kama kufua, kupiga pasi, kupika,nk ili baba awe na muda mzuri wa kutafuta kwa ajili ya familia.
Yaani wanawake wamekuwa wakitaka usawa wa 50/50 lakini cha ajabu mwizi akinyata huko nje usiku, utasikia "baba fulani we ndiyo mwanaume, toka kamfukuze mwizi"
Tunaomba na hapa pia mtusaidie ili 50/50 ifanye kazi vizuri.