Hivi, wanaume mnaposema kuwa wanawake wa siku hizi tunapenda usawa huwa mnamaanisha nini?

Ninyi ndiyo hamtaki hizo equal responsibilities
 
em yataje majukumu ya kike ambayo mwanaume inabidi afanye

Majukumu ya mwanaume ni kutafuta pesa na kuhudumia mke na watoto na ya mwanamke ni kufanya kazi za ndani na kulea mume na watoto sasa leo hii wanaume mnataka wanawake tuingilie majukumu yenu ila ninyi hamtaki kuingilia majukumu yetu
 
Mwanaume yeyote mwenye familia anatakiwa atimize majukumu yake hata akiwa shoga
Nyie mnachagua ma hesam majukum ya kiume watayatimizaje na u hesam wao?
 
Kwani kuna ubaya gani kumshirikisha mke wako?? Kwani haujui kuwa mke ndiyo mshauri namba moja wa mume?? Kama haujui nafasi ya mkeo kwako basi usioe tu kama umeoa basi nampa pole mkeo
Usawa ni pale mnapotaka wanaume tusifanye maamuzi yeyote nyumbani mpaka tuwashirikishe yaani hata mshahara wangu unataka unipangie tuutumiaje hapo ndio mnapotuchosha
 
Sasa ndiyo kwanini msituhurumie??
Mnapenda usawa kwenye kila kitu...

Kitu ambacho hakiwezekani kua na usawa wa 50/50 kati ya mwanamke na mwanaume..

Ili mwanamke aende sawa na mwanaume inampasa mwanaume amuhurumie mwanamke kwenye mambo mengi sana...


Cc: mahondaw
 
Huruma wao wanaona ndio haki yao.
Yaani Hawa wa hivi ndio mama wa mabinti watakaokuwa wake za watu miaka ijayo.
Nawaonea huruma Sana waoaji wa miaka hiyo
Lakini hata tukitumia akili tu ya kawaida ninyi hamuoni kama mnawabebesha mizigo wanawake??
 
Agiza pombe kali san itakayokufny uwepo kitndn cku mbil ila ujilipie
 
Hayo uliyoyataja juu ni matokeo ya wanaume kutaka wanawake wawasaidie majukumu yenu hivyo na wao wanaona ni haki yao muwasaidie majukumu yenu na ni ndoa nyingi siku hizi wote mwanaume na mwanamke wanatafuta pesa na wanahudumia familia wote wanaenda kazini asubuhi wanarudi usiku sasa unategemea huyo mwanamke anapata wapi huo muda wa kufanya hizo kazi?? Kama hamuwezi tafuteni housegirl au houseboy!!
 
em yataje majukumu ya kike ambayo mwanaume inabidi afanye
Ukitoa majukumu yetu ya kubeba mimba kuzaa na kunyonyesha je na majukumu yetu mengine nayo hamyawezi??
 
Mbavu moja ya kushoto kutoka kwa mwanaume haiwez kua sawa na mbavu zilizobaki....

Wanawake muwe wapole, kwanza nyie ni option baada ya kuonekana mwanaume yuko mpweke

So jukumu la msingi la mwanamke to make sure mwanaume hayuko bored period.
 
Sasa ndiyo kwanini msituhurumie??

Mbona tunawahurumia sana... mambo mengine tunawapitisha au kuwapatia bila vikwazo...

Ila ndiyo hamuachi kusema what a man can do a woman can do better wakati in reality tunawahurumia...


Cc: mahondaw
 
Kwani kuna ubaya gani kumshirikisha mke wako?? Kwani haujui kuwa mke ndiyo mshauri namba moja wa mume?? Kama haujui nafasi ya mkeo kwako basi usioe tu kama umeoa basi nampa pole mkeo

Hivi sifanyi?
 
KUTAKA KUKITWAA KITI CHA ENZI CHA MUME.
 
Mwenye ndoa ni mwanamume, mwanamke umeletwa ndani kumsaidia mume baadhi ya maeneo. Ni ukweli ambao wanawake wa siku hizi umeukiuka, mkijifanya much know. Mumeo akivutiwa na vya nje maana yake kuna mambo ndani hayajakaa sawa, imekupasa kujitazama na kurekebisha hapo, sio kuleta ushindani. Ndivyo ilivyokuwa tokea awali, pale wanawake walipotambua nafasi ya mwanamume kwenye ndoa.

Umewahi kusikia msemo mwanamke moumbavu huivunja ndoa yake kwa mikono yake mwenyewe? Basi ni kwa ujuaji wa kijinga, kujifanya kupambana na mumeme ndani ya ndoa. Asikudanganye mtu, ndoa ya kweli haina haki sawa, anayetoa mahari ndio mwenye ndoa yake.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…