Hivi, wanaume mnaposema kuwa wanawake wa siku hizi tunapenda usawa huwa mnamaanisha nini?

Brother wewe ndoa yako ipoje!?
 
Nitajibu kifupi tu.. Kwamba, mwanamke unapoolewa huwa unatoka mikononi mwa wazazi na kuingia mikononi mwa mume. Hivyo yote ulokua unawaskiza wazazi yanahamia kwa mume isipokua kwa mume kuna nyongeza. Heshima, usikivu, uvumilivu nk vyote vinahamia kwa mume. Hivyo hupaswi kushindana na mume kama vile ambavyo hushindani na wazazi. Mfano huwa tunasema mzazi hakosei. Na hata akikosea huwezi kumsema kakosea Bali atajua Na ataseti mambo. Si jukumu kuanza kukomaa eti mzazi akuombe msamaha. Hivyo hivyo kwa mume. Mwendee kwa unyenye kevu.

Tatizo mnaona kuwa kumnyenyekea mwanaume ni utumwa. Eti haki sawa na hakuna aliye Juu ya mwingine. Hivyo kama unavyowatreat wazazi wako na mume awe hivyo hivyo. Tena uongeze zaidi ikibidi maana yeye ndo wako wa maisha.

Mambo ni Mengi ILA chukua huo mfano then utathmini
 
Mkuu kifupi ni kuwa wanalilia huo usawa lakini hata ukiwauliza ni usawa Gani hawawezi kujibu. Maana unaweza kumkubalia anachotaka halafu badae anabadilika anakua hataki tena. Yani basi tu we can't understand women at all. Ndo mana Mara nyingi ukiona huelewi unanyuti kimya ..
 
Tatizo ni mgawanyo wa majukumu wanaume hawataki kufanya majukumu yetu ila wanataka wanawake tufanye majukumu yao na matokeo yake wanawake tunajikuta tunafanya majukumu mengi kuliko wanaume something which is not fair I think.
Kama yapi hayo ?
 
Mbavu moja ya kushoto kutoka kwa mwanaume haiwez kua sawa na mbavu zilizobaki....

Wanawake muwe wapole, kwanza nyie ni option baada ya kuonekana mwanaume yuko mpweke

So jukumu la msingi la mwanamke to make sure mwanaume hayuko bored period.
Je hilo ndio jukumu wanalolifanya wanawake siku hizi??
 
Sawa Mkuu
Mbona tunawahurumia sana... mambo mengine tunawapitisha au kuwapatia bila vikwazo...

Ila ndiyo hamuachi kusema what a man can do a woman can do better wakati in reality tunawahurumia...


Cc: mahondaw
 
Ni kwamba hauyajui au makusudi tu?? Na nimeshajua lengo lako la kuuliza hayo majukumu ni yepi basi kwa kejeli ngoja nikutajie kufanya kazi za ndani na kulea watoto (ndiyo mnayaweza kama ambavyo sisi tunaweza kutafuta pesa na kuhudumia watoto)!!
kama yapi? hem yataje
 
Sawa mkuu ila je ni wanawake wangapi wanyenyekevu kwa waume zao ila waume zao wanawanyanyasa??

Labda unisaidie jibu kwanini kila mume akifanya kosa kwenye ndoa chanzo kinaonekana ni mwanamke??
 
Vizuri ila si unajua majukumu ya wazazi kwa watoto wao eenh?? Je vipi kama mume hatimizi majukumu kama hayo kwa mke wake na tena anataka mke wake amsaidie naye anastahili heshima kama ya wazazi??
 
Siyo ukweli mkuu nadhani hamtaki kabisa kugusia zile familia ambazo mke anatoa hela katika familia sawa na au kuliko hata mume sasa hapo mume naye anaweza akaongea maneno kama haya?? Kwamba eti women 'can not' do better than men wakati mfano wa kwanza anao hapo nyumbani kwao??
Usisononeke huyo ndiyo ukweli...


Cc: mahondaw
 
Sawa mkuu ila je ni wanawake wangapi wanyenyekevu kwa waume zao ila waume zao wanawanyanyasa??

Labda unisaidie jibu kwanini kila mume akifanya kosa kwenye ndoa chanzo kinaonekana ni mwanamke??
Habari za wanawake kunyanyaswa zimekuja zama hizi. Zimeletwa na wazungu nasi tukkazidakia bila utathmini madhara yake. Aina yamanyanyaso ni kaama mtoto a kike kunyimwa elimu, kumiliki mali, haki ya kutofanya shughuli za nyumbani kwsabbabu mtoto wa kiume hafanyi nk. Hayo ndio manyanyaso, mengine ni uzhshi tu. Mwana,ke kupigwa ni utaduni wa enzi na enzi kwa sababuboss waa familia ni mmoja tu. Mwanamke anatakiwa kutii, sio huo utamaduni wenu wa kimagharibi mliotuletea sasa.
 
MMMH MAMBO HAYA NI MAGUMU SANA DADA YANGU....

KWA KWELI DUNIA YA LEO LINAPOKUJA SWALA NA USAWA KATI YA MKE NA MUME NI MJADALA MPANA SANA NA WAKATI MWINGINE UNAKOSA MUAFAKA KUTOKANA NA MAKUNDI AMBAYO NI WAHUSIKA KATIKA HILI.

KWA UFUPI TU MAKUNDI KAMA YA IMANI ZA DINI, WANAHARAKATI WA MASUALA YA JENDA NA MAKUNDI YASIYOSOMA NA YALIYOSOMO WANATOFAUTIANA SANA KIMITIZAMO NA KUNA NAMNA TOFAUTI TOFAUTI ZA UFANYAJI WA MAKOSA UYASEMAYO NA HATA KAMA YAKIFANYIKA UTATUZI WAKE PIA HUTOFAUTIANA.

MFANO KATIKA UKRISTO KUNA BAADHI YA MAKOSA HAYARUHUSIWI KUFANYWA KABISA..... MAKOSA KAMA UZIZI, ULEVI NA UGOMVI HAYARUHUSIWI KABISA. NA MSISITIZO NI MUME KUMPENDA MKE NA MKE KUMTII MUME. MTU AKIMPENDA MKEWE KATIKA MAPANA YAKE NA KWA MAANA YAKE HATAWEZA KUZINI, KULEWA, KUMPIGA NA KUTOMSHIRIKISHA KWENYE JAMBO LOLOTE LILE. VILE VILE NA MKE AKIMTII MUME HATAWEZEKANA KUDAI KIITWACHO HAMSINI KWA HAMSINI KATIKA NYUMBA WALA KUINUA MDOMO MREFU KAMA SAMAKI CHUCHUNGE NA KUMSONYA MUMEWE HATA KAMA KAMKOSEA. MAMBO YAO HUMALIZWA KATINA NAMNA YA KIMUNGU KWA HOFU NA UTII.

NA UKIKUTANA NA KUNDI LISILOMJUA MUNGU NALO LINA NAMNA YAKE WANAVYOCHUKULIANA KATIKA NDOA NA MAHUSIANO HALIKADHARIKA MIFUMA YA KISOMI HUSUSANI YA KIMAGHARIBI AMBOA WANA HADI NDOA ZA MIKATABA AMBAPO MKATABA UNAWEZA SEMA SIKU UKINIKUTA NA MCHEPUKO WANGU USINIGUSE WALA KUNINYOOSHEA KIDOLE. KTK ULIMWENGU WA UISLAM MWANAMKE HAWEZI KULALAMIKA KUHUSU KUTOFANYA KAZI NA KUKAA NDANI TU NA WALA KUTOENDESHA MAGARI (KAMA VILE SAUDIA....JAPO SASA HIVU KUNA MSUKUMO USIO NA NGUVU WA KUTAKA KUWAPA WANAWAKE FURSA MAGARI YA KUENDESHA NA KUSHIRIKI MCHAKATO WA UCHAGUZI ILI WAPIGIWE KURA) KAMA ILIVYO KWA WANAUME. IMANI NA MAFUNDISHO YAKE YANASEMA HIVYO NA HALIWEZI KUHOJIWA. UCHAGANI MTOTO WA KIKE HAKUWA NA NAFASI TANGU DAHARI KURITHISHWA KIHAMBA KAMA WARITHISHWAVYO WANAUME.

HIVYO BASI USAWA HUO UUZUNGUMZIAO UNATEGEMEANA SANA NA MAKUNDI NA SALSAFA HUSIKA ZA MAKUNDI HAYO KUHUSIANA NA SUALA LA NDOA. USIPOYAELEWA HAYA MAMBO NA KUKUELEKEZA KUWA UNAINGIA KWENYE NDOA AU MAHUSIANO NA KUNDI LIPI UTAYUMBA SANA KTK MAHUSIANO YAKO.
 
Mimi ni mume na mke wangu ni mke!! Huwa naonekana kama mtu wa kizamani lakini msimamo wangu ndio huo. Mke wangu ni house wife, kwani nilitaka hivyo awe hivyo. Alee watoto, sitaki habari za house girl.

Mwanangu unajua unachokifanya nikiwa mkubwa nataka niwe kama wewe,

Yes kama wewe mzazi no 50/50 https://jamii.app/JFUserGuide 50/50


Nikimuona mtu anaandika kwa herufi kubwa paragraph kadhaa kwanza huwa sisomi halafu namuona kama hana akili vile
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…