Hivi, wanaume mnaposema kuwa wanawake wa siku hizi tunapenda usawa huwa mnamaanisha nini?

Kiongozi lazima awe na majukumu mengi kuliko msaidizi na ayatimize kikamilifu sasa inapotokea kiongozi hatimizi majukumu yake anamwachia msaidizi huyo kiongozi ana sifa tena ya kuwa kiongozi?

Halafu unapotolea mifano ya babu zetu na bibi zetu usiangalie upande wa ndoa kudumu tu jiulize bibi zetu walikuwa wanafurahia hayo maisha? Yaani kwenu nyie wanaume ili mradi ndoa imedumu na nyie mnafurahia maisha basi haina shida hata kama wanawake huku wanaugulia maumivu? That's selfishness at it's best.
 
Tufafanulie mpenzi, maana mwanamke anaetoa elfu moja yake akanunua fungu la kitunguu huyo pia anachangia huduma.....
 
Kwanza, hiyo ya wanaume kufa mapema siyo sababu.

Pili, wanaume wangapi mnalalamika kuwa wake zenu wamewaachia kazi zote wadada wa kazi na hatimaye mnaamua kutembea na hao wadada wa kazi?
 
Wanafanya hivyo kwa sababu ya mgawanyo wa majukumu kumbuka mwanamke ambaye anafanya kazi zote za nyumbani peke yake wakati mumewe yupo na hamsaidii, ni ngumu kwa huyo mwanamke kutumia pesa zake kwenye maendeleo ya kifamilia
 
Kwanza, hiyo ya wanaume kufa mapema siyo sababu.

Pili, wanaume wangapi mnalalamika kuwa wake zenu wamewaachia kazi zote wadada wa kazi na hatimaye mnaamua kutembea na hao wadada wa kazi?
Mwanaume kutembea na dada wa kazi ni utashi wake yeye mwenyewe tu kama atakavyoamua kuchepuka na mwanamke mwingine yeyote yule..

Nataka nijue hayo majukumu unayoyazungumzia ni yapi haswa.. itapendeza ukiyataja..
 
Hahahaha hapana mkuu tunaposema mtusaidie siyo kwamba tunakuwa tunawaambia ila tunataka mjiongeze wenyewe yaani mchukulie hayo ni kama majukumu yenu na msione kama vile kuyafanya ni dharau

Halafu kuhusu kitafuta mfanyakazi kwani wanaume wangapi wanatembea na hao wafanyakazi kwa kisingizio cha kuwa wake zao wamejisahau na majukumu yote wamewaachia wafanyakazi?
 
Izo ni sifa za wanaume wa dar,

Huku mikoani wanaume tunalima mashamba, tunapasua mbao, tunafanya kazi ngumungumu ambazo mwanamke hawezigusa!

Ndomaana uku heshima bado ipo
Oohh basi hapo sawa
 
Hahaaa..."Mafahali wawili......."
 
But at the same time you want us to take care of you especially in the financial matters. hapa ndo nliposhindwaga kuwaelewa ni 50/50 gani mnayoitaka!
Tunataka mtuhudumie kiuchumi kwa sababu ya huo huo mgawanyo wa majukumu
 
Thats a valid point.... Hao wanatembea na mabosi wanafanya hivyo kama sehemu ya income kwao....
 
Sawa mkuu
 
Sawa ila inapotokea mwanamke naye ni mtafutaji inakuwaje?
 
Suala la mtu kuoa mtua aliyemzidi kipato au elimu na akaendeshwa huo ni uzembe wake na inabidi asubirie huruma au utashi wa mwanamke au atulie awe chini, ingawa kwangu mimi hata mwanamke awe na hela kivipi lazima nimdhibiti na lazima atulie.

Na kuhusu hilo la ndoa, ni kwamba ili ndoa idumu lazima kila mtu atimize majukumu yake, mke kujishusha kwa mume wake hata kama kosa ni la mume ( nafikiri hili lipo kwenye organization zote nchi; raisi , chuo; mkuu wa chuo, bunge; spika). Hivyo mwanamke akitimiza jukumu la kujishusha, ndipo mume atajieleza vizuri.
 
Inategemea, kama na wewe mkeo siku akiumwa au akiwa na mimba kubwa huwa unamsaidia kufanya kazi za ndani basi na yeye siku ukiyumba kiuchumi atakusaidia tu ila tofauti na hapo usimlaumu na inaonyesha wewe hata mkeo akiumwa au akiwa na mimba kubwa hauwezi kumsaidia chochote bado utataka kazi zote afanye mwenyewe
 
Ndo maana kuna ma house girl halafu huwa nawashangaa wengi wenu tunawawekea wasaidiz wandani kabisa mnalalamika eti majukumuu
 
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]wewe naona umeamua kunichekesha uko sahihi nimekuelewa ila nakuhakikishia mkuu kuna ndoa wanaume hawatimizi majukumu yao kabisa yote wamewaachia wake zao na hao hao wanaume nao wanataka heshima ndani kutoka kwa wake zao na jamii nzima mimi nina mifano ya ndoa hizo
 
Tatizo mnaexaggerate utadhani hizo ndoa hata 50 zinafika.... Tukitoa vijijini ambapo wanaume kwa asilimia kubwa ni walevi na hivyo ni unfit kudeal na familia.
 
Kuhusu maandiko mwanaume kaumbwa kutawala , mwanamke kma msaidizi t
Pia ukisem ufuate maandiko bas vitu vingi tumeenda kinyume na maandiko
Ndiyo mliambiwa mtutawale ila pia mliambiwa mtakula kwa jasho lenu sasa siku hizi kuna wanaume hawali kwa majasho yao wanakula kwa majasho ya wake zao halafu bado wanataka kuwatawala wake zao kwahiyo mnachagua maandiko ya kuyafuata (yanayowafaidisha) na maandiko ya kuyaacha (yanayowabana) si ndiyo?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…