Jadda
JF-Expert Member
- May 20, 2019
- 30,567
- 86,748
- Thread starter
- #161
Kiongozi lazima awe na majukumu mengi kuliko msaidizi na ayatimize kikamilifu sasa inapotokea kiongozi hatimizi majukumu yake anamwachia msaidizi huyo kiongozi ana sifa tena ya kuwa kiongozi?Ni suala la kupima tu, kwanini siku hizi ambapo haki sawa inapiganiwa sana, ndoa nyingi zinavurugika na watu wanaachana sana kuliko zamani ambapo wanawake hawakuwa na elimu, kumiliki mali na wanaume walikuwa wanaoa wake wengi lakini kuachika ilikuwa ni nadra sana.
Jibu ni moja tu, hakuna nyumba inayoweza kuendeshwa na viongozi wawili na ikafanikiwa, labda mmoja awe msaidizi.
Halafu unapotolea mifano ya babu zetu na bibi zetu usiangalie upande wa ndoa kudumu tu jiulize bibi zetu walikuwa wanafurahia hayo maisha? Yaani kwenu nyie wanaume ili mradi ndoa imedumu na nyie mnafurahia maisha basi haina shida hata kama wanawake huku wanaugulia maumivu? That's selfishness at it's best.