Kiuumbaji ndoa imara hutegemea sana akili na maarifa ya mke anavyom-handle mume.
Kwa kawaida sisi wanaume huwa tuko weak sana kwa mwanamke anayetuheshimu, kutupenda kwa dhati, mcha Mungu, kutunyenyekea, mtiifu na anayetujali. Ukiyafanya hayo kwa moyo wa dhati i.e ni lazima kuwa mvumilivu ndoa yako inakuwa imara sana.
Mke pafanye nyumbani pawe mahala pa mumeo kupakumbuka na kupenda kuwa hapo kila wakati awapo mbali yaweza kuwa kazini ama safari na hadhalika.
Kuna wanawake ni vichomi hadi kero. Yaani mume ikifika jioni badala ya kufikiria kurudi nyumbani anatamani siku ianze upya maana nyumbani akifika ni pa moto badala ya kuwa pahala pa kupumzika.
Huwa hatuna mbwembwe nyingi mbele ya mwanamke anayetujulia namna ya kuishi na sisi, na ni rahisi sana kututeka mioyo yetu