Hivi wapenzi wa King'amuzi cha Azam tofauti na ligi ya Tanzania kuna nini?

Azam nje ya kuonesha mpira wa Ligi kuu ya Tanganyika; hakuna kitu kingine cha maana cha kunivutia mteja kama mimi.
 
Mimi ni mteja wa mwanzoni wa Azam ,nilinunua Dish 2014 ,Mwanzoni walikuwa na channels nyingi halafu ilikuwa cheap sana,ila sasa channels nyingi famba.

Wanawake wanapenda kwa ajili ya tamthilia zao zilizotafsiriwa.
 
Kumshindanisha dst iliyoanza 1996 na azam wa mwaka2013 sio sawa naiman hata wao walianza na makosa mengii kabla ya kufikia huo ubora unao uona leo big up kwa azam mpaka kushindwanisha na mkongwe wa kimataifa si jambo dogooooooo
 
Unatumia router ipi na unalipia shingapi?
 
Mkuu hebu naomba uni-enlighten zaidi kuhusu huu mchakato mzima
 
Azam amejikita katika burudani ya ndani,na ni kitu ambacho amewazidi hata DSTV.
Azam ukiondoa mpira kuna channel za Azam one,azam two,sinema zetu ameweka tamthilia ambazo zinakamata akili za kinamama na watoto hadi baadhi ya kinababa.
Tamthilia hizo huzikuti sehemu yeyote hata DSTV huzikuti.
Hasa sinema zetu ameweka tamthilia ambazo ndizo zinachukua tuzo za TIFF,hiyo imepelekea soko la filamu Tanzania kutekwa na Azam media.
Kiufupi Azam kateka burudani ya ndani.
 
Angalau wanajitahidi mkuu.
Usiwe mtu wa kukosoa kila kitu.
Kuna movie inaitwa the kidnap.
Iliingia hadi viwango vya Netflix ile movie.Ilitengenezwa kwa dola laki moja ila mauzo yake yalipita dola laki tano.
Kuna tamthilia kama Shilingi,Kombolela,Haikufuma aisee walioandika hizo tamthilia ni noma.
Na hiyo ni chachu kidogo ya uwekezaji wa Azam.
Usiponde tu mzee haifai.
 
Azam wanajitahidi kuleta ubora wa HD.
Kwa television za ndani wamefanikiwa ila za nje bado.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…