Hivi wapo wanaofanikiwa kupata wenza makini (serious) mitandaoni?

Teknolojia imerahisisha Sana maisha, hivi karibuni kumetokea website na Apps mbalimbali za kupata marafiki wachumba na hata kuoana kabisa. Wengi wa walioko mtandaoni wapo kwa ajili ya maslahi, wengi wao ni matapeli, unaweza Kuta mwanaume kaweka picha ya Binti mzuri kweli kweli jilengeshe uone sasa, hata Kama ni wa kike unakuta Kuna vigezo vinavyokukwamisha kama unataka kumuoa mfano mwenye mtoto.

Kuna [emoji2765] site nyingi kv JF, Telegram, na nyinginezo play store. Waliofanikiwa na kutofanikiwa kupatana kupitia mtandao tupeni uzoefu humu.

Karibuni.
 
Kama unavyoona mtaani wengi ni wadangaji,watu safi wachache, basi huko mtandoni hali ni hiyo hiyo, wema wachache, wadangaji wengi.
 
wengi wa hao wachumba ni wajasiria-uchi,
Wanajitangaza wazi yaani ukiingia Instagram na Telegram ni mitandao ya ovyo kabisa unakuta mtu kaanzisha group la wauza malaya JF Pekee ndio mtandao safe
 
Ushauri mzuri na wenye busara, kutangaza hadharani hili suala inahitaji umakini wa hali juu. Na wale walio siriazi wanaweza wakachukulia tofauti na mhitaji.
 
Unaweza pata πŸ˜…πŸ˜…πŸ˜…

Nina watu wa4 nawajua wameolewa wanaishi safi tu na wote walikutana na wenza wao mtandaoni tena sio mtandaoni tuu ila ni kule kwenye dating sites
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…