Hivi wataalam wa kilimo toka SUA wana impact gani! Mbona hawasikiki?

Hivi wataalam wa kilimo toka SUA wana impact gani! Mbona hawasikiki?

Ukisema wakulima wa Tanzania hawataki kubadilika, uko sawa lkn hili tatizo ni kwa wakulima wote waliosoma na wasio wasomi. Maana una kuta asilimia kubwa ya watu waliosomea Kilimo(99%) hawataki kubadilika! Yaani hawataki kufanyia kazi walichosomea, namaanisha unakuta Afisa Kilimo kasoma lkn hana na hataki kulima na hana maono ya kulima hata robo eka! Afisa Mifugo naye vivo hivyo hataki wala hana maono ya kufuga hata kuku mmoja. Na wakulima wasio wasomi(99%) hawataki kufanyia kazi kitu ambacho hawajasomea.
Angalia wakulima katika nchi za Ulaya, Asia, America, Australia ni wataalamu wamesomea Kilimo lkn kwa Tanzania mambo ni kinyume waliosomea hawatekelezi/hawatendi walichosomea. Wasio soma ndo wanalaumiwa kuwa hawataki kubadilika. Wakati anayelaumu naye anafanya yaleyale!
Kuna ukweli hapa
 
siasa mbaya sana, eti serikali inashindwa hata kuweka green house 2 kila halmashauri , mabwawa ya samaki na mashamba ya kuku kwa ajili ya kufundishia wananchi na kuwa kama sehemu ya mapato inakalia porojo za kisiasa na kukomoana na
upinzani
Ni Ajabu sana
 
Ni sawa na vipi ma phd holder wa bongo wana impact gani ???
PHD Holders wa Bongo wawe na ubunifu upi?

Ukimpelekea tatizo anakuambia Its okay ngoja kuna mtafiti mmoja wa marekani au Uingereza anaweza kutatua hilo tatizo.

Sasa unasema huyu yeye anaweza kufanya nini sasa? Kutoa ushauri tu? [emoji23] [emoji23]

Ndio maana wanaingia kwenye siasa.
 
None sense we usha mtafuta mtaalam gan ukakuta hajui kukupa ushaur au wataka akufuate uliko
 
Tatizo ni kuwa serikali haiwrkezi kwenye kilimo na haijali kilimo teknolojia nyingi sana zipo developed na SUA ila implenentation haiwezekani kutokana na uhaba wa pesa.
Serikali ya CCM . .

Chama kinachotengeneza Serikali ni CCM . . HATUTOKI NG'OOO . . !
 
Kama ni ma-theory tu unategemea upate kitu gani?

Badilisha mfumo wa elimu watu wajifunze kwa matendo zaidi kama VETA uone kama inakuwa kama ufikiriavyo.

Shida ni kwamba tunajua kinacho tuharibia ila tunashindwa kuchukua hatua.
Kinachotuharibia tunakijua . . , tatizo ni njaa, ujinga, wizi wa kura, na wanafiki . .

Tukiwatoa hawa watunga Sera za ujamaa wa kutegemea wafadhili, tukiwatoa hawa watunga Sera za uongo - Siasa ni Kilimo (siasa ni ufisadi). . , wa tangu miaka 50 iliyopita labda tutapona . .
 
hivi ndo mnavofikili kisiasa kuhusu kilimo kwa kuwalaumu wataalamu wa kilimo bila kutafuta nini kinakwamisha hili tatizo,
moja ya sababu kuu ni SERA za CCM NI ZA kipumbavu zinazotungwa na wanasiasa WAPUMBAVU wasiokuwa na elimu pamoja na uchungu juu ya TANZANIA NA WATANZANIA . . !

serikali yako inapanga bajeti ya kilimo na kuipa pesa kidogo halafu bado hyo asilimia ndogo iliyotekelezeka ni 30 asilimia tu, then mwaka wa fedha ujao tena itapitisha bajeti ya uongo na kweli.

mkuu, kumbuka kilimo ni kazi ambayo inaambatana na utafiti wa kila leo ili kuendana na dunia, leo hii viwavi jeshi(armyworm) vinaibuka na kushambulia maeneo mengi na mikoa mingi lakini wizara inatoa macho tu haijui ifanyeje.

KILIMO,UFUGAJI NA UVUVI utake usitake lazima pesa itumike kwenye utafiti ili tuweze kufikia malengo....

[emoji115]

NIMEREKEBISHA MANENO KIDOGO HAPO JUU BW DAUD THE FARMER . . !

POLE SANA . . , UMEZUNGUMZA KWA UCHUNGU SANA . . !
 
Unaongelea maafisa kilimo au waandishi wa habari!! Kama ni afisa kilimo kwake shamba sasa ww uliye town utamsikiaje? Mbaya zaidi huna hata robo heka kwa mfano
 
Kwa mini msi
What i can say ni kwamba wakulima wa kitanzania hawataki kibadilika ndio maana kilimo hakisongi ,ukifanya utafiti wakulima wamefundishwa sana na taasisi za binafsi na za kiserikali but ukipima impact ya mafunzo ni zero sababu mtu amachofundishwa sicho anachokifanya ,na hapo ndipo anaepima kilimo kama mtoa mada kwa impact huoni kama kuna kilichofanyika . First ni watanzania tujifunze kubadilika na kupokea elimu ndipo kilimo kitasonga.
Huwezi amini mpaka leo hii wenzetu wanatoka kwenye hybrid wanaenda kwenye G.M.O (siungi mkono lakini gmo) ila sisi bado tunatumia mbegu za kichanjani,bado tunakamua mbegu kwenye mazao ya shambani na kuzipanda tena . Kila mtu angekua kwenye hybrid ungeona impact ,kila mtu angejua anatoa nn shambani ungeona impact. Ila mtanzania anatumia milioni 2 kuzalisha zao akivuna anauza milioni 1 na anajisifia amepata faida ,inasikitisha sana kwa sisi ambao tuko field na tunaona hali ilivyo na hakika binafsi ndio inanipa morali ya kuongeza bidii kubadili mindset za farmers
Kwa nini msianzishe kampuni za kuzalisha hizo mbegu mpaka waje wazungu? Watu wa SUA wamekosa ubunifu kabisa.Wameshindwa kuanzisha mashamba ispokuwa wachache tu.Wakiajiriwa wanaishi mjini wanapiga pombe tu.Watu wa sua wamedumaza kilimo nchini.Kila unachokiona mtaani kilichofanikiwa huchochewa na watu kutoka kenya.SUA Wameshindwa kujibu magonjwa sugu ya mimea kama mnyauko wa viazi mviringo, Kantangaze ktk nyanya nk.Sua wanatakiwa wajitafakari hakuna cha mfano mambo yanaenda hovyo,nenda njombe,mbeya angalia mashamba ya miti yako hovyo kabisa yamepandwa holela.Nasema hivi kwa sababu mimi ni mdau wa kilimo.
 
Usianze kuuliza wataalamu wa SUA. Wewe hapo ulipo umeleta impact gani? Kila mtu akianza na swali hili hata wataalamu wa SUA watakuwa na impact.

Yani mchango wao hauonekani kabisa katika kuinua sekta ya kilimo na mifugo.
Sekta ya kilimo imeendelea kuwa duni tangu nchi ipate uhuru na hawa jamaa wameshindwa kabisa ku transform kilimo.
Kifupi hawana impact kama Makapuku forum.
Siku mkirogwa mkanipa urais hiki chuo ntakifuta katika siku zangu mia za kwanza...
 
Mtoa mada hana ufahamu kabisa kuhusu SUA na kilimo kwa ujumla.
-ukiugua unatafuta tiba kwa haraka sana , lini ulitafuta msaada wa kitaalamu kwa afisa kilimo ukakosa. Afisa kilimo ni mtoa ushauri hivyo hana nguvu ya kulazimisha ushauri wake kufuatwa ukizingatia gharama za technology _ kuingiliana kwa siasa na utaalamu ni tatizo _ na mengine mengi nitafute nikujuze hivi hakuna mkulima anaeweza kujua kwamba nikiwa namimea mingi shambani nitavuna mavuno mengi ? Kwa nini anapanda ovyo (mchafukuoga)
Walimu wakifelisha hutumbuliwa,maafisa ugani kilimi duni wanakula tu mishahara.
 
Natambua kuwa wanaosoma pale SUA wanasota kweli kufunzwa na kujifunza kwa bidii wafaulu mitihani.

Lakini je hayo masomo yanawaandaa kutumia mbinu walizopewa chuoni kufanya uzalishaji, uchakataji na uongezaji mwingine wa thamani katika sekta ya kilimo?

Serikali ingeanzisha mfuko wa kufadhili wataalamu wetu binafsi au kivikundi kuendesha shughuli za kilimo katika mabonde yetu Rufiji nk.

Mpango wa kuchangia mfuko wa ujenzi wa barabara kupitia mauzo ya mafuta umewezekana. Bila shaka mfuko kwa ajili ya wajasiriamali vijana kutoka SUA ungewezekana pia.

Vijana wangepewa changamoto kabla ya kutoka chuoni waandike mapendekezo ya miradi kwa vigezo shindanishi. Mshindi au washindi wanapewa fedha awamu kwa awamu kadiri ya mipango na matokeo.

Serikali kuu au wizara husika inaweza unda timu ya wataalamu bobezi kila kanda kukagua, kushauri vijana hao kila hatua hadi wanapokomaa au kufanikiwa.

Ni fedheha kusomesha wataalamu wa kilimo kisha wanakuwa jobless au kuwa makarani wa benki.

Wahitimu hao wakianzisha miradi hiyo wataajiri watanzania wenzao toka mijini na vijijini kufanya kazi mbalimbali.

Je, serikali na SUA hawawezi fanyia kazi jambo kama hili?


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom