Hivi wataalam wa kilimo toka SUA wana impact gani! Mbona hawasikiki?

Kuna ukweli hapa
 
siasa mbaya sana, eti serikali inashindwa hata kuweka green house 2 kila halmashauri , mabwawa ya samaki na mashamba ya kuku kwa ajili ya kufundishia wananchi na kuwa kama sehemu ya mapato inakalia porojo za kisiasa na kukomoana na
upinzani
Ni Ajabu sana
 
Ni sawa na vipi ma phd holder wa bongo wana impact gani ???
PHD Holders wa Bongo wawe na ubunifu upi?

Ukimpelekea tatizo anakuambia Its okay ngoja kuna mtafiti mmoja wa marekani au Uingereza anaweza kutatua hilo tatizo.

Sasa unasema huyu yeye anaweza kufanya nini sasa? Kutoa ushauri tu? [emoji23] [emoji23]

Ndio maana wanaingia kwenye siasa.
 
None sense we usha mtafuta mtaalam gan ukakuta hajui kukupa ushaur au wataka akufuate uliko
 
Tatizo ni kuwa serikali haiwrkezi kwenye kilimo na haijali kilimo teknolojia nyingi sana zipo developed na SUA ila implenentation haiwezekani kutokana na uhaba wa pesa.
Serikali ya CCM . .

Chama kinachotengeneza Serikali ni CCM . . HATUTOKI NG'OOO . . !
 
Kama ni ma-theory tu unategemea upate kitu gani?

Badilisha mfumo wa elimu watu wajifunze kwa matendo zaidi kama VETA uone kama inakuwa kama ufikiriavyo.

Shida ni kwamba tunajua kinacho tuharibia ila tunashindwa kuchukua hatua.
Kinachotuharibia tunakijua . . , tatizo ni njaa, ujinga, wizi wa kura, na wanafiki . .

Tukiwatoa hawa watunga Sera za ujamaa wa kutegemea wafadhili, tukiwatoa hawa watunga Sera za uongo - Siasa ni Kilimo (siasa ni ufisadi). . , wa tangu miaka 50 iliyopita labda tutapona . .
 

[emoji115]

NIMEREKEBISHA MANENO KIDOGO HAPO JUU BW DAUD THE FARMER . . !

POLE SANA . . , UMEZUNGUMZA KWA UCHUNGU SANA . . !
 
Unaongelea maafisa kilimo au waandishi wa habari!! Kama ni afisa kilimo kwake shamba sasa ww uliye town utamsikiaje? Mbaya zaidi huna hata robo heka kwa mfano
 
Kwa mini msi
Kwa nini msianzishe kampuni za kuzalisha hizo mbegu mpaka waje wazungu? Watu wa SUA wamekosa ubunifu kabisa.Wameshindwa kuanzisha mashamba ispokuwa wachache tu.Wakiajiriwa wanaishi mjini wanapiga pombe tu.Watu wa sua wamedumaza kilimo nchini.Kila unachokiona mtaani kilichofanikiwa huchochewa na watu kutoka kenya.SUA Wameshindwa kujibu magonjwa sugu ya mimea kama mnyauko wa viazi mviringo, Kantangaze ktk nyanya nk.Sua wanatakiwa wajitafakari hakuna cha mfano mambo yanaenda hovyo,nenda njombe,mbeya angalia mashamba ya miti yako hovyo kabisa yamepandwa holela.Nasema hivi kwa sababu mimi ni mdau wa kilimo.
 
Usianze kuuliza wataalamu wa SUA. Wewe hapo ulipo umeleta impact gani? Kila mtu akianza na swali hili hata wataalamu wa SUA watakuwa na impact.

 
Walimu wakifelisha hutumbuliwa,maafisa ugani kilimi duni wanakula tu mishahara.
 
Natambua kuwa wanaosoma pale SUA wanasota kweli kufunzwa na kujifunza kwa bidii wafaulu mitihani.

Lakini je hayo masomo yanawaandaa kutumia mbinu walizopewa chuoni kufanya uzalishaji, uchakataji na uongezaji mwingine wa thamani katika sekta ya kilimo?

Serikali ingeanzisha mfuko wa kufadhili wataalamu wetu binafsi au kivikundi kuendesha shughuli za kilimo katika mabonde yetu Rufiji nk.

Mpango wa kuchangia mfuko wa ujenzi wa barabara kupitia mauzo ya mafuta umewezekana. Bila shaka mfuko kwa ajili ya wajasiriamali vijana kutoka SUA ungewezekana pia.

Vijana wangepewa changamoto kabla ya kutoka chuoni waandike mapendekezo ya miradi kwa vigezo shindanishi. Mshindi au washindi wanapewa fedha awamu kwa awamu kadiri ya mipango na matokeo.

Serikali kuu au wizara husika inaweza unda timu ya wataalamu bobezi kila kanda kukagua, kushauri vijana hao kila hatua hadi wanapokomaa au kufanikiwa.

Ni fedheha kusomesha wataalamu wa kilimo kisha wanakuwa jobless au kuwa makarani wa benki.

Wahitimu hao wakianzisha miradi hiyo wataajiri watanzania wenzao toka mijini na vijijini kufanya kazi mbalimbali.

Je, serikali na SUA hawawezi fanyia kazi jambo kama hili?


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…