Hivi Watanzania kwa nini huwa wanatumia haya maneno mawili kwa wakati mmoja? "Unless otherwise"

Sasa wabongo ndio wanaitumia katika mifano niliyotoa. ...by the way mbona wewe ndio unaonekana kenge hapa maana nimekutolea hadi mifano in what context wabongo wanaboronga lakini bado huelewi.
Hiyo heading iko very clear nini umemaanisha, na hata ndani ya uzi hujasema kama unazungumzia katika mifano hiyo tu, bali umetolea kama moja ya mifano...! Sasa omba mods wabadilishe heading, ongeza , ‘katika sentensi hizi?’
 
hujakuatan na watu wanavyotamka "Issue" "inshu" sijui wapi wameitoa hiyo herufi "n"
 
Kwa tafsiri isiyo rasmi "Unless maana yake isipokuwa/la sivyo. Otherwise maana yake isipokuwa/la sivyo". Hivyo chagua neno mojawapo tu uteleze, utaelewaka zaidi badala ya kulazimisha kuyatumia yote kwa wakati mmoja.
Nadhani shida imeanzia hapa...tafsiri yako ya kiswahili kwa neno otherwise siyo sahihi...binafsi sioni shida na sidhani Kama Kuna makosa haya maneno kutumika pamoja
 
Inabore kuona mtu anaongea maneno mawili yenye maana sawa. Sijawahi kusikia wenye kiingereza chao wanaongea hivi. Hata sisi waongea kiswahili huwezi kuongea maneno mawili ya kiswahili yenye maana sawa kwa wakati mmoja
Utasikia halafu then akaja home
 
Jf is never boring.....in The Boss voice.
 
Na ndiyo point ya lugha. Kuwa tuelewane. Ukishanielewa sababu kuu ya kutumika hiyo lugha inakuwa imetimia.
Naelewa point ya lugha ni kuelewana, lakini kama unaharibu bila kujali na ku assume nitakuelewa tu, utajuaje nitakuelewa?

This is an arrogant ignorance. Mtu anakujambia halafu ukimuambia umejamba unasema ushuzi utapita tu hauwezi kuua mtu.

Mtu kakukanyaga kwenye daladala, ukimwambia hapa umenikanyaga, anakwambia si tutafika tu, lengo la kupanda daladala ni kufika safari.

Mwachie aliyejambiwa aseme ushuzi utapita tu.

Mwachie uliyemkanyaga aseme atafika tu.

Mwachie uliyemuharibia lugha aseme amekuelewa tu.

This ignorant arrogance is normalizing verbal diarrhea.
 
Upo sahihi kabisa, ushuzi utapita na safari mtafika tu yaani.
 
Trust me ingekuwa Hivi,,mpaka Leo tungekuwa tunaongea Old English au classic arabic
 
Nimekuta thread imefika page 11. Sikuwa na muda wa kusoma comment zote hivyo pengine kuna mdau ameshaelezea. Ni hivi: Kutumia maneno Unless otherwise kwa pamoja siyo kosa kutegemea na ulivyoyatumia. Hii sentence ni correct: The guy is in trouble unless otherwise. Hapa umesema kuwa jamaa yuko kwenye shida kubwa na atanusurika iwapo kitu/hali nyingine (ambacho hatuijui) itatokea. Neno otherwise limetuka kuwakilisha kitu/hali yoyote itayomwokoa huyo jamaa aliye kwenye shida.
 
Trust me ingekuwa Hivi,,mpaka Leo tungekuwa tunaongea Old English au classic arabic
Kuna lugha zina formal custodians na nyingine hazina.

Kiingereza hakina. Kiarabu hakina.

Kifaransa kina. Kiswahili kina.
 
Sijakuelewa kabisa
Kuna lugha zinaongozwa na mabaraza rasmi ya kupitisha maneno. Mfano ni Kifaransa (Academie Francaise) na Kiswahili (BAKITA).

Kuna lugha hazina mabaraza rasmi ya kupitisha maneno. Mfano ni Kiingereza na Kiarabu.

Mifano yako ya Old English na Classic Arabic haifai.

Kwa sababu ni mifano inayoangalia lugha ambazo hazina mabaraza rasmi ya kupitisha maneno (Kiingereza na Kiarabu) katika kuzilinganisha na lugha yenye baraza rasmi la kupitisha maneno (Kiswahili).
 
Hili ndilo tatizo la kukariri kila kitu toka kwenye Biblia, Qur'an na vitabu vya shule bila hata kufikiri.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…