Hivi watumishi wenzangu mnawezaje kupata utajiri wa kuwa na mihela mingi!

Hivi watumishi wenzangu mnawezaje kupata utajiri wa kuwa na mihela mingi!

Nimejikaza ila acha niandike. Mimi nasubiri kuthibitishwa ili nikope at least 18M yote iingie kwenye hii business iiboost kutokea ilipo sasa.

Niliwahi fanya kazi private kabla sijaingia serikalini, private nilifanya kazi kampuni ya mikopo ya simu. Nilikua Team Leader, ili kukupa picha ya pesa iliyopo kwenye hii industry ni kwamba branch ya Arusha walipiga 1B na kampuni haikutetereka.

So this is what is done. Wewe muuzaji unakua una simu ambayo mfano gharama ni elfu kumi, kampuni ya mkopo (niliyofanyia kazi) inakuambia hii simu utaiuza si zaidi ya 100% this means hii simu ambayo itauzwa 14K kwa cash wewe kwenye mkopo itakuletea 20K. Kutegemea na kampuni hii inamaanisha utaipata hii pesa hapo hapo, baada ya siku tatu au baada ya siku 28 (Kampuni zipo tofauti).

Kama upo Dar, Dom au Mwanza na ukawahi kuona bajaji zimeandikwa Mandas Store ni aina hiyo ya business. Mimi kwa sasa mtaji wangu ni mdogo but si haba.

Wewe jua location tafuta kampuni ikupe akaunti (Watu Simu wamestop kuregister owner wapya so hata ukiamua hii deal make sure mtu anayekutengenezea akaunti ni legit asije kukupiga) tafuta inventory muweke kijana, mawinga wawekee pesa yao pembeni. Gharama zote za Inventory na kuwapa mawinga ganji ikawa ni 10M inatakiwa ikurudishie 18M mpaka 19M.

Hichi ndicho nakijua ambacho ni legit na kinakupa almost 80% ya profit kwa fixed duration.
Hiyo faida kwa muda gani
 
Hayo maconnection ya kupiga deal na Samia, Abdul au Kikwete, WATU WANAZIPATAJE???
Mwanangu kama hutajali funga safari ukamtembelee mzee wa Msoga kwa utakufa? Pamoja na kwamba kazee kamekuwa kapuuzi lakini wewe usijali! Kaelezee shida zako zote za connection katakupa shavu!
 
Huu uzi naufuatilia hadi namimi niwe billionea
 
KARIAKOO kuna watu wana ukwasi hadi 30-50b na huwezi kuwajua. Wenye mashahada ni wachache kutajirika sababu ya kuogopa kubahatisha. Biashara wanazichanganuwa kwenye makaratasi na kuishia kujitisha.

Kina ugonjwa unaitwa analysis paralysis.
Umenena vyemaaaaa
 
Ni ela gani mnazozitafuta ndugu zangu kila mtu anataka ela ila wakuu mko kasi sana
 
INTRODUCTION:-
Yaani nina ""fazaaa"" na mawazo hata kusalimia naona NAPOTEZA MUDA tuu...!!!

Hebu twende hoja..

Watumishi wa umma ambao ni matajiri hebu njooni hapa ndugu zangu..!!

Kabla ya yote si unajua humu hatujuani, WE FUNGUKA TU UNIPE ABC NDUGU YENU.

Hivi mtumishi wa umma anakuaje na hela hivi..!!!

SCENARIO:-
Jamani humu kwenye utumishi wa umma kuna watu wanahela yaani miji fedha..!!

Kuna raia leo nimeona kabisaa UTT anamiliki Bil 1.2 kapata wapi hela zote hizi huyu jamaa..!!

Changamoto nilichungulia kimbea hivyo hata nguvu ya kumuuliza nimekosa..!!!!

Mnapata wapi hela..!!

PROBLEM:-
Mimi bwana nimelelewa maisha magumu sanaa,
1. Maisha ya uswahili
2. Yatima
3. Kutengwa na kunyanyaswa na ndugu
4. Kudhulumiwa mali na ndugu
5. Nimelala sanaa nje tena sometimes nje stendi, bar na sehemu hatari (Ile njia ya Kinondoni Studio mpaka Mwananyamala A Via komakoma NIMELALA SANAA NJE kwenye ile lami)

Yaani kifupi NIMETESEKA SANAAA UTOTONI (Uyatima nyoko..!!)

Ila nilikuja kujiapiza kuwa LAZIMA NIJE KUWA TAJIRI, yaani TAJIRI HASA.

Kwasababu nilikuja kujifunza, ""Ukosefu wa hela ndio ulinipitisha kwenye zile shida zoteee""

Yaani sitaki huu utajiri wa kubadilisha mboga, Nataka ule utajiri wa kumiliki masheli, mashule, majengo, mabiashara.

Yaani huo utajiri wa kumiliki magari makali kama ya Abduli NDIO NAOUTAKA MIMI.

Nataka ule utajiri wakutumia mil 20 per day continiously kwangu iwe normal thing...!!!

THE BIG PROBLEM:-
Katika harakati zangu za kutafuta utajiri nilipanga mambo 2.
1. Nisome sanaa (Nikafika Masters nikaona inatosha sasa)
2. Nifungue biashara (Nimefungua kampuni)

Ila hii kampuni/biashara bado naiona ndogo sanaa, nyie mi nataka zile helaaa yaani mingiiii.

Nikajiunga na CCM ila sasa naona kazi tu maana, sina ndugu mkubwa, sina connection kifupi ""Am nothing infront of CCM papas..!!""
Nikaona napoteza muda, NIKAACHANA NA SIASA..!!

Watu wakasema una elimu kubwaa tulia utaonekana, ila ni mwaka wa 8 sasa namiliki Masters ila sioni nikiitwa kokote au lolote lile lifanyike nipate shavu niseme ""Masters imeonekana sasa""

Nyie mlipata wapi hela??

Sasa bana, sawa nina kanafasi ofisini, ila sasa leo nimepiga hesabu posho zotee nilizopata tokea Mfumo wa malipo wa serikali ufunguliwe (mwaka mpya wa fedha) ni Milioni isiyofika 10. Yaani hela yenyewe dah ndogoooo.

1. Wenzangu mnapata wapi hela?
2. Hizo connection za CCM mnazipataje?
3. Hizo connection za mashavu huko Wizarani au kwenye mavitengo, mnazipataje??

Naambiwa kuna jamaa yupo Dodoma anapata posho mpaka safari za kwenda nje ya nchi kikazi anazichagua, nyengine anazipiga chini na kuweka wenzake, kwamba zina posho ndogo.
Halafu ana Bachelor tu, huyo baharia aliwezaje kupata hiyo nafasi??!!!

Nataka hela, kampuni yangu ikiitwa kila mtu aijue.

Yaani kama vile ukisikia MATI unajua huyo ni Mulokozi. Nataka sasa ukisikia ""ABCDEF Company"" Raia waseme "Huyo ndio Mr. Liverpool""

NATAKA HELAAA.

CONCLUSION
Mnaosema nina tamaa, nisikilizeni niwaambie..


1. Nimekulia maisha ya kushindia na uji wa sembe tu bila sukari.
2. Nimekulia maisha ya kuombaomba balaaa.
3. Nimekulia maisha ya manyanyaso hasaaa.
4. Magumu mengi sanaa nimepitia.
5. Kuna kipindi nilishawahi kumuandikia Mungu barua ""KWANINI MUNGU ULIUA WAZAZI WANGU?""

Nataka kusema nini....
Nimeishi maisha ya umasikini hasaaaa yaani down the ground, lakini hata posho/fedha kidogo serikalini nimeshika""

Trust me "POVERT IS REAL MUCH PAINING" Tafuta hela ""UMASIKINI NYOKOOO SANAAA""

Siwezi ombea mtoto yoyote kwenye hii dunia apitishwe maisha ya uyatima niliyopitishwa.

NI MAGUMU HASAAAAA

Sasa.
Nahitaji pesa, Nahitaji pesa Sanaaaaaa.

NAZIPATAJE HIZO HELA???

Hayo maconnection ya kupiga deal na Samia, Abdul au Kikwete, WATU WANAZIPATAJE???

#YNWA
#YANGA_BINGWA
Wewe ungefanya kazi taasisi yangu nafikiri ungeongea peke yako barabarani.
Hakuna hata mia mbovu unapata Kama posho zaidi ya internet ya bure.
Hapa kupata Staff mwenye miaka 10 ni mtihani watu wanachomoka Kama upepo
 
KARIAKOO kuna watu wana ukwasi hadi 30-50b na huwezi kuwajua. Wenye mashahada ni wachache kutajirika sababu ya kuogopa kubahatisha. Biashara wanazichanganuwa kwenye makaratasi na kuishia kujitisha.

Kina ugonjwa unaitwa analysis paralysis.
Hizo Bil 30 - 50 walizipataje??

#YNWA
#YANGA_BINGWA
 
Mda Si Mrefu Analiwa Mtu Nnya 😆😆

Usitamani Maisha Ya Mtu Blo.
Shaur Lako 😆😆
Kwanini tunafanikiwa "KWASABABU TUNATAMANI""
Tamaa ndio inakufanya utamani kikubwa, na mapambano yanaanzia hapo na KUFANIKIWA ZAIDI KUNATOKEA.

Halafu nikushauri, kwenye mada za watu usiwe sanaa "Pesmisim"

Negative words sio poa.

Think POSITIVE.

Na kengine "Usiwe una PERSONAL ATTACK" kwenye kujibu hoja.

#YNWA
#YANGA_BINGWA
 
Back
Top Bottom