Sababu za msingi na zinazomaliza wengi ni Vyakula & Life style, Msongo wa mawazo kupindukia (high level stress).
Vyakula Kwa maana vijana hawali vyakula vya kuupa mwili Faida kubwa, ukitaka kuamini Hilo angalia fast food restaurants zilivyo nyingi na zinavyomaliza Chakula Kwa haraka, fast foods Huku mijini havibaki siku hizi, watu wanavishambulia Sana. Ukiacha fast foods, pia ulaji na upikaji wetu si mzuri, pilau au wali utakuta limejaa mafuta kibao, rosti ya nyama mafuta kibao nk, wale wazee wa pombe Kila kukicha nao wanahusika Hapa...Ndizi ambayo ina kiwango Kikubwa cha potassium mitaani ni miambili but kijana Yuko Radhi atoe 5k akale chips yai. Vile vile si lazima Kula Milo mitatu Kwa siku, ukiweza Fanya miwili tu ambapo usiku iwe lazima, unaweza ukawa Hauli Sana but unachokula kina mafuta mengi kupitiliza na Faida ndogo.
Msongo mkali wa mawazo nao ni Jambo lingine kubwa Sana, ukiwa na msongo mkali unaharibu mfumo wote wa mwili maana msongo unaanza kichwani, unavuruga wiring yote ya mwili, unapoteza focus, unapoteza kumbukumbu, unalazamisha blood flow iende Kwa Kasi Sana nje ya inavyotakiwa yaani Kila kitu kinakwenda mbio, kimbilio la wengi sasa ili kutibu wanajipeleka kwenye matumizi ya kompyuta (simu nk) hii ni hatari nyingine maana blue lights ya hivi vifaa ni hatari Sana kuliko tunavyodhani....Stress nyingine za kujitakia kama vile mapenzi, Mahusiano.
Cha mwisho ni kutofanya mazoezi ambayo yanajumuisha shughuli zote za kushughulisha mwili kama vile kutembea, kukimbia, kuogelea nk, siku hizi watu wanatembea na boda boda wao siku nzima, huwezi kutoboa, Kama Mimi muongo mwambie Rais wa nchi ya Malawi akimbie hatua kumi Tu uone kama hatujamzika but unaona Emanuel Macron rais wa France alivyokata upepo Nairobi na Kipchoge, he is very fit.
Hizi Nafikiri ni sababu za msingi Sana zinazosababisha presha siku hizi.