Hivi kweli jamani kwa haya Maisha yetu ya Kiafrika ( hasa Kitanzania ) huku Wazee wetu nao wakiwa na Changamoto mbalimbali za Kiafya kutoka na Umri wao huo kwenda wanaweza kuwa na Uwezo wa Kumbebesha Mimba Mabinti wa miaka kati ya 25 hadi 35 na Kuzaa?
Je, hapa siyo kwamba hawa Wazee wetu wa kuanzia Miaka ya 70 Kiumri huwa Wanabambikiwa tu hizo Mimba na hao Watoto ila Ukweli ni kwamba huwa 'Wanachapiwa' tu na Madogo / Wajuba wenye Nguvu zao na Umri sahihi wa Kubandua Kisawasawa?
GENTAMYCINE nitakuwa wa mwisho Kuamini kuwa Mzee wa Umri wa kuanzia mwaka 70 anaweza / anauthubutu wa Kupandikiza Mbegu za Ujauzito kwa Binti wa kati ya Umri wa miaka 25 hadi 35 na Kuzaa ila niliambiwa kuwa huwa Wanachapiwa na Kubambikiwa hao Watoto nitakubali na kuamini kwa 100%
Haya karibuni rasmi katika Mjadala.
Kijana,kuna muda ukifika mnatutenga baba zenu,hamtutembelei wala kutupigia simu.
Kazi yenu kubwa ni kuhakikisha mama zenu hawakaukiwi safari za kuja huko mnakoishi.
Sasa sisi baba zenu tunabaki wapweke kwa kukosa watu wakutuchangamsha km vile wajukuu (watoto wenu ambao wanatumia siku 365/1 kuwa masomoni.
Sasa tujaribu kusahihisha makosa tunaoa damu changa ili tupande begu upya huenda zikaota vizuri kuliko za mwanzo ambazo zimefifia (ninyi vijana wetu) lkn pia kupata nguvu kazi kwa ajili ya kuchotewa maji,kuchumiwa mboga kwani hata fedha japo kidoogo hamtumi mkisingizia ada za watoto.
Vijana wetu,mama zenu wakishakuwa na uhakika wa kuletewa matumizi kutoka kwenu watoto wetu hawataki hata tukumbushane stori zetu za kipindii kile tulivyokuwa tunawavizia njiani kuelekea visimani na kuchelewa kurudi nyumbani.
Sasa ukiongezea na ninyi kutusahau na kututupilia mbali sisi baba zenu basi tuaamua kuangukia kwa hivi vibinti ilimradi tu tuchangamshe afya ya akili wakati ninyi mkisubiri tufariki kwa unyong'onyevu na mawazo mfanye vikao vya kuchapisha picha zetu kwenye flana ili muwafurahishe wafanyakazi na wafanya biashara wenzenu kwamba mlikuwa mnatupenda.
Msituone pindi tukutanapo kwenye matukio yanayotukutanisha kuwa tumeinama muda mwingi7,huwa tunakumbuka mengi ya kipindi mkiwa wadogo huku tukijivunia uwepo wenu sasa matokeo yake ndiyo hayo yamekuwa kinyume na matarajio yetu.
Miezi 8 yooote mmeninyang'anya mke wangu bila hata taarifa,halafu tunapo oa mnachukia,mnakosea sana. Muwe mnawaleteeni mama zenu wadogo hawa hata vi 500 na flana za vyama vyenu angalau waendelee kuboresha afya za akili zetu huenda nanyi umri ukisogea tukingalipo akili zitawariudi.