Pascal Mayalla
Platinum Member
- Sep 22, 2008
- 53,857
- 121,995
Karibu sana.P
Yapi maoni yako kuhusu DP World?
Au na wewe umeshalambishwa bahasha?
[emoji16][emoji16][emoji16][emoji16]
Kwanza nilianzia hapa, Watanzania tujifunze kukubali kuna vitu hatuwezi, tunaposhindwa tukubali kusaidiwa au tukomae? Baada ya Bandari ni ATCL na SGR au Tusubirie?
ikaja kuwaomba waheshimiwa wabunge wetu, kwenye kuridhia IGA ya DPW, watangulize mbele maslahi ya taifa Wabunge Wetu, Macho ya Watanzania Wote Leo ni Kwenu!. Maslahi ya Taifa Mbele!. Tuwaogope Kama Ukoma Muflis Hawa!, Kama Huwezi, ni Lazima Usaidiwe Tuu!.
Na baada ya Bunge letu Tukufu kuridhia mkataba huo bila kufanya due diligence yoyote kumhusu Mwarabu wa Dubai na hadhi ya mkataba wenyewe, kwanza nikasisitiza kuunga mkono hoja, Hakuna Ubaya Wowote kwa Mtu Yoyote, Taasisi Yoyote, Nchi Yoyote Kusaidiwa Pale Inaposhindwa, Muhimu ni Kuwa Makini Tusipigwe. Je DPW Tunapigwa?.
Kisha nikahoji uwezo wa Bunge letu na uwezo wa wabunge wetu kujadili jambo kubwa kama hili Bunge letu ni Bunge la ovyo? Bunge linafanya Uhuni? Wabunge Wetu ni Wahuni? Tumshauri Spika naye aanze kuita Watu kwenye Kamati, au waachwe tu? .
Pia nikatoa angalizo la maeneo yenye ukakasi ili HGA iwe imenyooka Japo Bunge Limeridhia, DPW Kuendesha Bandari Zetu, ni Makubaliano Tu, Tukithibisha Kuna Matatizo, Tunarekebisha Mkataba wa HGA, Kazi Nzuri Iendelee! na kesho Jumapili, nitaandika makala kwenye gazeti la Nipashe kuhusu huu mkataba
P