DullyJr
JF-Expert Member
- Apr 10, 2011
- 13,983
- 11,857
Huyu mwehu anajua kama ujumbe huu anawafikishia watu wengi sana nchini? Asilimia kubwa ikiwa ni hawa mashabiki wa Yanga wanaopambania kuingia bure uwanjani kwa kukosa elfu tatu.
Wengine ni majeruhi hadi leo na wengine wamepoteza uhai kwa ajili ya Yanga yao halafu yeye anatoka mbele waziwazi na kutoa hizi kebehi, na utakuta mashabiki maandazi wanafurahia kauli hizi wakati yeye akitoka hapo Mbagala anapofanya shughuli za kumuingizia kipato cha kila siku anatakiwa arukie daladala ili afike Chamazi kwenda kupumzika na familia yake!
Nahisi kuna siri nzito imejificha hapa kati ya kuwa shabiki wa Yanga na kukosa akili timamu. Utamkuta mtu kazaliwa vizuri na wazazi wake na kapitia hatua zote za ukuaji vema kabisa, ila anapoanza tu kuingia hapo Yanga akili zinabadilika zinakuwa za ovyoovyo.
Ehhh Mungu wasamehe hawa watu, na uwakomboe kama ulivyomkomboa Feisal Salum maana akili zake zimekaa sawa sasa.