Hivi Zanzibar ni ya waafrika au ni ya wazanzibari?

Hapo mkuu ukimwaga mboga namwaga ugali. Ukifanya znz free port na huku DSM inafanywa free port unafikiri nani ataumia?
 
Tukumbushane the Greater Zanzibar ilikuwa inahusisha na Mikoa ya Pwani ya Bara kwaivo Mzenji yeyote akiwa Pwani ni Nchi yake ya asili
 
Tukumbushane the Greater Zanzibar ilikuwa inahusiana na Mikoa ya Pwani ya Bara kwaivo Mzenji yeyote akiwa Pwani ni Nchi yake ya asili
Nimeishi Pemba kwa kazi maalumu miaka 3 naijua vizuri. Mkoani, kengeja, chakechake, pujini, vitongoji, gombani, maeli tano, ole, wete, makangale.
e.t.c
Nikaishi Unguja miaka 8, watoto wangu wawili nimezalia Unguja.
 
Ni wakati wenu sasa kupata hizo haki zenu zote mnazo lalamikia! Rais wa Tanganyika ni Mzanzibar mwenzenu. Hatutarajii kuendelea kuwasikia mkilalwmika kila siku.

Ikiwezekana basi jitengeni tu ili malalamiko yenu yakome! Maana Tanganyika inajitosheleza kwa kila kitu! Hatumtegemei yeyote yule! Hata Mabeberu wenyewe wanalitambua hilo.
 
Kuhusu elimu tunajidanganya, zanzibar huenda wako vizuri zaidi yetu..

Angalia illiterate rate kati ya Zanzibar na Tanganyika angalia pia rate ya wanafunzi waliopo Sekondari to general population, au idadi ya Universities per general popolation.

Bado jamaa wanapata nafasi za scholarship nje zaidi yetu.

Na Mwinyi ameanza kutengeneza Medical specialists na sera yake ya Medical tourism, hawa jamaa wanaweza kutuacha...
 
Zanzibar ni ya waafrika waarabu warudi kwao Oman walikuja na boti historia inaonyesha kabisa.. Hao ni wafanya biashara ya utumwa
 
Wangekuwa bado watumwa makuli
 
Zanzibar ni ya wa Zanzibari. Ila Tanganyika ni ya Watanzania wakiwemo wa Tanganyika na Wanzanzibari na Wazanzibara wa kiwemo Wapemba.

Ndio maana kwa maneno haya ya muanzisha hii thread ambayo ni warning shot, ni muombe VP pamoja na kwamba uliitwa Mwanga siku ile kwa kusimamia maslahi mapana ya Tanganyika hii thread iwe chagizo la wewe na Watanganyika wengine Mungu alio wapa Neema ya kushika nyadhifa mbalimbali majira haya kuungana na kuendelea kulinda maslahi haya mapana ya Tanganyika kwanza then Tanzania. Kuweni na Mtazamo huo Tanganyika kwanza ndio ifuate Tanzania.

Hamtakuwa wa kwanza sanasana mtakuwa mmejifunza kutoka kwa wenzenu wa Zanzibar kwanza halafu kwa mbali na kwa kusuasua Tanzania.

Mwenye akili na akanielewe.
 
Zanzibar ni ya waafrika waarabu warudi kwao Oman walikuja na boti historia inaonyesha kabisa.. Hao ni wafanya biashara ya utumwa
Hakuna Mtu aliyeenda Zanzibar kwa miguu kama yupo ni vizuri ukamtaja
 
Mods mbona mnavumilia post za kijinga kama hizi...
Kwa jina la muungano, ondoa hii post kazi iendelee.
Muandishi hajielewi natanguliza samahani.
weye ndio maadaui wa zanzibar umepatikana kirahisi kabisa ikiwa baba enu mchonga meno hakuna atakae kuindosha Zanzibar .Zanzibar itakuwepo mpaka ya Yaumu kiama kuna mijitu mengine ya bara ina roho mbaya sana Zanzibar ndio iliowafundisha Watanganyika Ustarabu mm naoana zipigwe karata tu .
 
Nje ya Muungano kuwa Waunguja na Wapemba,So ukimaliza kupost ujinga usishau hil😵VA
 

Haya maswali uliyouliza ni maswali mazuri sana, yanaweza kumsaidia member huyu kupata majibu. Tatizo lake hapa ni elimu, na kama sio elimu basi ni ubishi usio na maana. Kama ulivyosema ni ukabila, japokuwa kuwa Zanzibar makabila yana tafsiri tofauti. Huyu mwenzetu ana kiwango cha chini sana cha akili, na ana uwezo mdogo sana wa kufikiri na hata kuchanganua mambo.

Kumeibuka wimbi kubwa la watu kutoka mataifa mbalimbali kuvamia visiwani Zanzibar na kujiita ni Wazanzibari .....Ina maana kweli watu wanavamia Zanzibar wakati polisi wapo, jeshi lipo, na wazanzibari wapo?

-Fursa zao ktk Taifa lao mama ......Taifa mama maana yake nini? Hebu basi tukubali kuwa wazanzibar Zanzibar ndio taifa mama lao. Itakuwa akili huku bara tufukuze wapemba kwa kisingizio cha kijinga kama hicho? Tufukuze wapemba kwa kuwa sisi hatujui kufanya biashara, na kusma wametuzibia fursa?

-Haki zao za msingi.....Haki za kimsingi maana yake ni nini? Unaweza kuzitaja na usem ni zipi ambazo mzanzibari anazikosa?

-Uhuru wao ktk Taifa lao mama la Asili........ Hapa anasema Uhuru, Taifa mama la Asili..... Uhuru ni nini, na ni upi ambao Mzanzibar anaukosa, kuna kitu chochote ambacho mzanzibar kunazuia huo uhuru ?

Ukiangalia taifa mama la mzanzibari, utaona kuna mataifa mengi sana, utaona kuna Oman, utaona kuna Malawi, Utaona kuna Tanganyika, Uganda, Msumbiji, utaona kuna India, utaona nchi mbalimbali duniani ni mataifa mama kwa watu wa Zanzibar. Sasa kama wameamua kuwa wazanzibari huko kwenye asili yao kunahusu nini? Kama kuna wanaotaka waende. Angalia mataifa mama ya wajumbe wa baraza la kwanza la mapinduzi, halafu uliza leo kama wana lolote wanalotaka kwa hayo mataifa mama ya asili unayosema. Ungemuuliza Sheikh Karume aliyepigania mapinduzi, au mkewe mwambie leo aende kenye taifa lake la asili.


-Haki zao stahiki kwenye Taifa lao......Haki stahiki za kitaifa ni zipi ambazo mzanzibari anakosa. Sheria na katiba viko wazi na haki zote zimelindwa.

-Maamuzi ya kitaifa na kiraiya pamoja na kiuongozi.... Maamuzi ya kitaifa? Maamuzi ya Kiuongozi? Maamuzi ya kiraia? Wewe haya unayajua kweli?

Mambo kama haya yanatakiwa kusomeshwa na wataalamu wa elimu ya sayansi ya siasa, huyu mwenzetu anatakiwa kujiunga japo na darasa la Politics 100.
 
Zaidi ya nusu ya wazanzibar wanaishi nje ya Zanzibar, majority wako bara, na wengine kiduchu schemi nyingine.
 
Nadhani umefahamu ila unajitoa ufahamu
 
Unaakili ndogo kama ubongo wa funza utakua umeishia form 2 pale Skuli ya Dole
 
Ukifuatilia vizuri utaona hakuna wazanzibari asili bali wote ni wahamiaji, wangazija, washirazi na wamatumbi.
Hata wewe ukifuatilia babu yako utakuta katokea mafia au Tanga

Mzanzibar Asili ni nani ama ukienda Zanzibar ukasema nataka niwaone wakazi wa hapa wale wa asili ni akina nani?Mi nyumbani zanzibar pemba tena mchanga mdogo.

Hakuna Mzanzibar asili, wote ni wahamiaji. Ila bado sio sababu ya kuwa anaekwenda kuhamia leo nae apate haki zote kama mzanzibari.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…