Mleta mada kishayatolea ufafanuzi hayo maneno hapa, Mzanzibari = waarabu walioingia visiwa hivyo na kukuta havikaliwi na binaadam mwingine yeyote. Zanzibar ilikuwa ni nchi yao, huru kabisa, na walikuwa na utajiri wa kuwaajiri watu weusi, waliowaagiza bara (watumwa); kuja kuwafanyia kazi, kama za kilimo n.k.. Hawa ndio Wazanzibara, kwa mjibu wa mleta mada. Hawa ni watu weusi (waafrika).
Bahati mbaya ni kwamba, hawa Wazanzibara walianza kujiingiza kwenye siasa za visiwani; zilizopelekea kutokea kwa mapinduzi na vifo vya wazanzibari wengi.
Hawa wazanzibara ndio wanaolaumiwa kwa kujiingiza kwa Tanganyika na kuleta muungano.
Haya ndiyo niliyojifunza kutoka kwa mleta mada hii hapa.
Kama wewe una-'version' tofauti ya Uzanzibari na Uzanzibara, itapendeza pia ukiiweka hapa tukusome.
Kwa hayo yote niliyoeleza hapo juu, ndio maana nikaomba unisaidie kupata jibu, kwa nini leo hii, au siku zote uchaguzi ukiitwa, wazanzibari ndio huwa ni washindi dhidi ya wazanzibara, ambao kwa hali ya kawaida, kutokana na hayo niliyojifunza hapa, ndio wangekuwa wengi na kushinda bila tatizo lolote.
Sasa wewe uliponistua, nikadhani kwamba pengine utakuwa na jibu, kumbe nawe mwenzangu ni kubahatisha tu?
Eleza mkuu, unayoyajua wewe.
Uingiaji wa Wabara Zanzibar tunaweza kuugawa kwa majira matatu makubwa.
Wakwanza ni wale waliongia kipindi cha biashara ya Utumwa ambacho kilikua ni miaka ya 1700's - 1800's. Hawa wengi walipelekwa kwa biashara ya Utumwa ambapo kulikua na soko kubwa la biashara hiyo, Kuna walionunuliwa na wazawa wakawa wanafanykazi Zanzibar na kuna wale waliokosa soko au wateja wa kuwanunua wakaachiwa huru wakajenga makaazi huko huko. hawa wengi. Japo kua Zanzibar hawakuitwa kama watumwa walitambulika kama ni watumishi kwa jina. hawa walijenga makaazi yao maeneo mengi ya mashamba ambayo yalikua hayakaliwi na watu wengi, Zaidi wanapatikanwa mkoa wa kusini Unguja. Wengi wao asili zao walitokea maeneo ya Kanda ya ziwa pamoja na DRC. (Maeneo ambayo watumwa wengi walipotokea) Na wapo wengi wenye asili za kisukuma, Zaidi maeneo ambayo yanatambulika kama Makunduchi na Kizimkazi. (Maeneo ambayo Mama Samia Anapotokea). Hawa Kule Zanzibar kwa umaarufu wakijulikana kama wahadimu kwa maana ya watumishi. (Ni neon lenye asili ya kiarabu).
HAWA SIO WANAOITWA WAZANZIBARA, kwa maana walitambulika kama wazanzibari na raia rasmi kwani walishakuepo pale kwa miaka mingi.
faze ya pili ni ile ilioanza baada ya biashara ya utumwa amabyo ilianza 1900's mwanzoni mpaka miaka ya harakati za kisiasa 60's
Hawa wengi walikuja kutafuta Maisha kutoka bara na wengi walikuja kwa kazi za ufanyaji kazi kwenye mashamba na Uchukuzi pamoja na kazi nyengine ndogo ndogo. Ilianzia kipindi cha Utawala wa Ujerumani ambapo Maisha yalikua magumu sana bara kipindi hicho, wananchi wengi walipata mateso kwa kazi ngumu zenye ujira mdogo (nafikiri historia hiyo utakua unaifahamu vizuri) na hapo ndipo ilipokuja trend ya watu wengi kutimkia Zanzibar. Ni iliendelea hata baada ya Muingereza kuanza kuitawala Tanganyika. Mimi binafsi niliwahi kufanya kazi na Dr. mmoja kutoka nje nikiwa kama muhifadhi wake data kwenye miaka ya 2008 - 2010 alipokuja TZ kwa research zake. Kulikua na document za serekali kabisa za kwenye 1920's na 1940's serekali ya Mfalme wa wakati huo wakiilalamika kwa balozi wa Uingereza kwa kuachia wageni kuingia Zanzibar kiholela na kuhamia, huku serekali ya kikoloni haikulishulikia kabisa hilo jambo. Na ndipo ndani ya miaka hiyo palipoanzishwa African Association ambalo lilikua ni tawi la TAA ya Tanganyika, ulikua Umoja wa watanganyika wanaoishi Zanzibar. na baada hawa hawa wakaanzisha chama cha siasa cha ASP ambacho kilianzishwa kwa support kubwa kutoka TANU Na hawa ndio waliofanya mapinduzi 1964 wakisaidiwa na serekali ya Mwalim Nyerere kwa wakati huo.
Kwahiyo neno wazanzibara lilikua ni kwa hawa wa bara waliohamia Zanzibar kwenye maika hiyo ambao wengi wao hawakua hata wamezaliwa Zanzibar walihamia tu, na hao wachache waliozaliwa basi walikua na kizazi kimoja tu.
Ndio mana wazanzibari wa wakati huo hawakuwatambua hawa kama ni wazanzibari wakiamini kuwa ni wageni,
Na kwa kukuthibitishia tu,
Abeid Karume ni mnyasa alizaliwa Malawi
Aboud Jumbe alizaliwa Mji mwema
Ali Hassan Mwinyi alizaliwa Kisarawe
John Okello alitoka Uganda
Mfaranyaki, Said washoto, Kaujore, Edison Kisasi, Seif Bakari, Natepe, Isac Sepetu, Yussuf Himid, Nassor Moyo, Mtoni rehani, hawa wote hawakuzaliwa Zanzibar walihamia.
Ba vuai, Salmini Amour, Sadalla, Kassim Hanga hawa walizaliwa ila wazazi wao ndio waliohamia Zanzibar.
Na ndio mana baada ya mapinduzi tu Karume alitangaza kuwa kila aliekuemo ndani ya Zanzibar baada ya mapinduzi basi atakua rasmi ni raia wa Zanzibar, mana karibu asilimia 80% yao hawakua raia halali.
Na ndio mana Wazanzibari wanaamini 1964 hakukufanyika mapinduzi bali yalikua ni mavamizi kutoka Tanganyika ambayo ndio mpaka leo wanaendelea kutawaliwa na Tanganyika.
Sasa hiyo term wazanzibara inamaanisha ni kwa wale wa bara wanaoishi Zanzibar ambao sio wazanzibari ila wanajivisha uzanzibari. (Kwa mfano kama raisi wa sasa baba ake hakuzaliwa Zanzibar na wala yeye hakuzaliwa wala kukulia Zanzibar lakini kapelekwa kawa Raisi Zanzibar) Haimaanishi kuwa kwa kila mwenye asili ya bara nae ni mzanzibara.
Kwahiyo suala la Uzanzibari na Uzanzibara halimanishi kuwa wazanzibari wenye asili ya kiarabu na kiafrica. Ni uzushi unaotengenezwa na serekali ya Tanganyika kuwajaza ujinga raia wao ili wajihalalishie ajenda zao za kuitawala Zanzibar kimabavu. Zanzibar hakujawahi kuwa na Tatizo la Uarabu vs Uafrica, ni propaganda za CCM kwa ajili kijihalalishia kwenye macho ya watu wao wanachokifanya, na ndio mana kila uchaguzi Zanzibar kwa pamoja wote waarabu na waafrica sauti yao hua moja na ndio mana CCM inaishia kutumia mabavu ya kupiga watu na kuuwa ili wachukue serekali kwa nguvu.