Hivi Zanzibar ni ya waafrika au ni ya wazanzibari?

Ahsante mkuu, nadhani umenipa wazo jipya kuhusu muungano wetu huu.

Tusiendelee kufichana ukweli - tatizo la muungano wetu ni kati ya pande mbili. Zanzibar waarabu, au watu wanaojitambulisha kuwa na asili ya kiarabu zaidi ndio wasiopenda muungano huu (kama wapo wenye asili ya Afrika (weusi) upande huo, hawa watakuwa na maslahi mengine pembeni.

Upande wa pili ni hawa wazanzibari (wenye asili yao kuu Afrika, na hasa hasa Tanganyika - najua hawa ni wengi, na hawa ndio hasa wanaoshikilia muungano wakishirikiana nasi waTanganyika.

Sasa swali ni hili: kweli Tanzania iache maslahi yake ya Zanzibar kwa sababu waarabu hawataki? Sioni hilo lilkitokea karibuni.
 
Kichwa cha mada kinasomeka hivi: Hivi Zanzibar ni ya waafrika au ni ya wazanzibari?

Jibu sahihi ni hili: Zanzibar ni ya waTanzania, wala sio ya waafrika au waarabu.
 
Kichwa cha mada kinasomeka hivi: Hivi Zanzibar ni ya waafrika au ni ya wazanzibari?

Jibu sahihi ni hili: Zanzibar ni ya waTanzania, wala sio ya waafrika au waarabu.
Yah hilo ndiyo jibu sahihi
Zanzibar ni tanzania

Waarabu walipokuja hapo
Waliwakuta watanzania

Ova
 
Nadhani hii kwanza angeiona dos.2020 na wenzake maana hawataki mtu mweusi atawale Kisiwa hicho kabisa.
Na wasipoelimishwa watamsumbua sana Mama Samia Suluhu Hassan anayeielewa maana hasa ya Muungano,
Ni Kisiwa kidogo sana kwa eneo lkn Hayati JK Nyerere alitamani akisukumie mbali kabisa hata Shelisheli
Kwa sasa Viongozi wa juu kabisa katika Baraza la Mawaziri la Muungano linaloketi kila wiki watakuwa wao wa Zanzibar, Rais wa JMT Rais wa SMZ sijajua Makamu Bw Othman ataingia ila yu karibu sana, watalijadili swala hilo na kuiangalia keki hiyo ila wasivunje tu Muungano mikononi mwao.
G 55 ilizaliwa kipindi km hichi vikelele vidogovidogo, wakaona bora Tanganyika yetu
 
Acheni ushamba na ujinga. Mna habari kuwa wazanzibari na wapemba wengi wako bara kuliko hivyo vijipande vyao vya ardhi? Kama kila nchi ni kwa wazawa basi walioko bara warejeshwe visiwani muone kama patatosha.
 

MKuu jitafakari, Hivi kama wanaoshikilia muungano kama ndio wengi kwanini kila uchaguzi hua wanagaragazishwa kipigo cha paka mwizi?
 

Mkuu kwanini hua unapindisha ukweli na unatoka nje ya hoja husika?
 
Itabidi uanze na Rais wako!
 
MKuu jitafakari, Hivi kama wanaoshikilia muungano kama ndio wengi kwanini kila uchaguzi hua wanagaragazishwa kipigo cha paka mwizi?
Sina jibu juu ya hili swali mkuu dos.2020.
Ninaomba kama unamchango wowote juu ya jibu, usaidie kunifumbua macho.

Lakini nilichojifunza hapa kutokana na mada hii, kama kweli "wazanzibara", kama walivyotambulishwa humu wanayaelewa haya; na bado wakaendelea kupiga kura kuunga mkono "wazanzibari", ambao ndio wenye nchi yao (yaani waarabu); basi sielewi tatizo la hao "wazanzibara" ni nini hasa.

Kiuhakika, siamini kamwe kwamba Zanzibar kuna waarabu wengi kuwazidi watu weusi walioko huko.

Labda kuna sababu zingine zinazowafanya weusi wa huko kuwaunga mkono 'mabosi' wao hao, ili waendelee kuwa chini ya himaya yao.
 

Mkuu ili kuyaelewa haya yanataka mda, na kuanza kufahamu baadhi ya mambo ambayo pengie ulikua unayafahamu kivengine kabisa ambavyo si katika uhalisia.

Kwanza mkuu unapoambiwa Wazanzibara wewe unaelewa vipi? na unafahamu asilia yake na mantiki yake hili neon?
 
Mleta mada kishayatolea ufafanuzi hayo maneno hapa, Mzanzibari = waarabu walioingia visiwa hivyo na kukuta havikaliwi na binaadam mwingine yeyote. Zanzibar ilikuwa ni nchi yao, huru kabisa, na walikuwa na utajiri wa kuwaajiri watu weusi, waliowaagiza bara (watumwa); kuja kuwafanyia kazi, kama za kilimo n.k.. Hawa ndio Wazanzibara, kwa mjibu wa mleta mada. Hawa ni watu weusi (waafrika).
Bahati mbaya ni kwamba, hawa Wazanzibara walianza kujiingiza kwenye siasa za visiwani; zilizopelekea kutokea kwa mapinduzi na vifo vya wazanzibari wengi.
Hawa wazanzibara ndio wanaolaumiwa kwa kujiingiza kwa Tanganyika na kuleta muungano.

Haya ndiyo niliyojifunza kutoka kwa mleta mada hii hapa.

Kama wewe una-'version' tofauti ya Uzanzibari na Uzanzibara, itapendeza pia ukiiweka hapa tukusome.

Kwa hayo yote niliyoeleza hapo juu, ndio maana nikaomba unisaidie kupata jibu, kwa nini leo hii, au siku zote uchaguzi ukiitwa, wazanzibari ndio huwa ni washindi dhidi ya wazanzibara, ambao kwa hali ya kawaida, kutokana na hayo niliyojifunza hapa, ndio wangekuwa wengi na kushinda bila tatizo lolote.

Sasa wewe uliponistua, nikadhani kwamba pengine utakuwa na jibu, kumbe nawe mwenzangu ni kubahatisha tu?

Eleza mkuu, unayoyajua wewe.
 
Utafiti uliofanywa na Wanaakiolojia Profesor Mark Horton kutoka Uingereza kwa kushirikiana na Profesor Chami wa Chuo Kikuu Daresalaam mwaka 2007 katika eneo la pango la Kuumbi- Jambiani Mkoa wa Kusini Unguja yamepatikana mabaki ya viumbe mbalimbali ikiwemo tembo, chui pamoja na makaburi wa watu ambao walikuwa wakiishi katika mapango hayo miaka 3000 iliyopita. Mabaki hayo yapo katika makumbusho huko huko kuumbi. Nakushauri uende ukajifunze. Swali dogo tu Watu hao na wanyama walitoka Oman na Persia?
 
Ninamshangaa sana huyo jamaa anayejiita 'Mzanzibari huru' kwa hayo anayoyaeleza kwenye mada hii.

Hata angekuwa ni mtu mwenye kisomo kidogo sana, uzoefu wa umri wake ungemwelekeza kwamba haiwezekani visiwa vikawa pori tu bila kuwemo watu na wanyama.
Tena sehemu yenyewe ni karibu kabisa na bara kuu la Afrika!

Lakini nimemsoma vya kutosha, na mwishowe nimefahamu kwamba sio swala la yeye kutojua, bali yupo tu kutetea anayoshawishiwa yeye kwa manufaa yake na watu wake.
Huyo jamaa ni 'bigot' mkubwa.

Sikujua, kumbe kuna waarabu wanaojiona wao ni bora zaidi ya binaadam wengine, hasa weusi.
 

Uingiaji wa Wabara Zanzibar tunaweza kuugawa kwa majira matatu makubwa.
Wakwanza ni wale waliongia kipindi cha biashara ya Utumwa ambacho kilikua ni miaka ya 1700's - 1800's. Hawa wengi walipelekwa kwa biashara ya Utumwa ambapo kulikua na soko kubwa la biashara hiyo, Kuna walionunuliwa na wazawa wakawa wanafanykazi Zanzibar na kuna wale waliokosa soko au wateja wa kuwanunua wakaachiwa huru wakajenga makaazi huko huko. hawa wengi. Japo kua Zanzibar hawakuitwa kama watumwa walitambulika kama ni watumishi kwa jina. hawa walijenga makaazi yao maeneo mengi ya mashamba ambayo yalikua hayakaliwi na watu wengi, Zaidi wanapatikanwa mkoa wa kusini Unguja. Wengi wao asili zao walitokea maeneo ya Kanda ya ziwa pamoja na DRC. (Maeneo ambayo watumwa wengi walipotokea) Na wapo wengi wenye asili za kisukuma, Zaidi maeneo ambayo yanatambulika kama Makunduchi na Kizimkazi. (Maeneo ambayo Mama Samia Anapotokea). Hawa Kule Zanzibar kwa umaarufu wakijulikana kama wahadimu kwa maana ya watumishi. (Ni neon lenye asili ya kiarabu).
HAWA SIO WANAOITWA WAZANZIBARA, kwa maana walitambulika kama wazanzibari na raia rasmi kwani walishakuepo pale kwa miaka mingi.

faze ya pili ni ile ilioanza baada ya biashara ya utumwa amabyo ilianza 1900's mwanzoni mpaka miaka ya harakati za kisiasa 60's
Hawa wengi walikuja kutafuta Maisha kutoka bara na wengi walikuja kwa kazi za ufanyaji kazi kwenye mashamba na Uchukuzi pamoja na kazi nyengine ndogo ndogo. Ilianzia kipindi cha Utawala wa Ujerumani ambapo Maisha yalikua magumu sana bara kipindi hicho, wananchi wengi walipata mateso kwa kazi ngumu zenye ujira mdogo (nafikiri historia hiyo utakua unaifahamu vizuri) na hapo ndipo ilipokuja trend ya watu wengi kutimkia Zanzibar. Ni iliendelea hata baada ya Muingereza kuanza kuitawala Tanganyika. Mimi binafsi niliwahi kufanya kazi na Dr. mmoja kutoka nje nikiwa kama muhifadhi wake data kwenye miaka ya 2008 - 2010 alipokuja TZ kwa research zake. Kulikua na document za serekali kabisa za kwenye 1920's na 1940's serekali ya Mfalme wa wakati huo wakiilalamika kwa balozi wa Uingereza kwa kuachia wageni kuingia Zanzibar kiholela na kuhamia, huku serekali ya kikoloni haikulishulikia kabisa hilo jambo. Na ndipo ndani ya miaka hiyo palipoanzishwa African Association ambalo lilikua ni tawi la TAA ya Tanganyika, ulikua Umoja wa watanganyika wanaoishi Zanzibar. na baada hawa hawa wakaanzisha chama cha siasa cha ASP ambacho kilianzishwa kwa support kubwa kutoka TANU Na hawa ndio waliofanya mapinduzi 1964 wakisaidiwa na serekali ya Mwalim Nyerere kwa wakati huo.
Kwahiyo neno wazanzibara lilikua ni kwa hawa wa bara waliohamia Zanzibar kwenye maika hiyo ambao wengi wao hawakua hata wamezaliwa Zanzibar walihamia tu, na hao wachache waliozaliwa basi walikua na kizazi kimoja tu.

Ndio mana wazanzibari wa wakati huo hawakuwatambua hawa kama ni wazanzibari wakiamini kuwa ni wageni,
Na kwa kukuthibitishia tu,
Abeid Karume ni mnyasa alizaliwa Malawi
Aboud Jumbe alizaliwa Mji mwema
Ali Hassan Mwinyi alizaliwa Kisarawe
John Okello alitoka Uganda
Mfaranyaki, Said washoto, Kaujore, Edison Kisasi, Seif Bakari, Natepe, Isac Sepetu, Yussuf Himid, Nassor Moyo, Mtoni rehani, hawa wote hawakuzaliwa Zanzibar walihamia.
Ba vuai, Salmini Amour, Sadalla, Kassim Hanga hawa walizaliwa ila wazazi wao ndio waliohamia Zanzibar.
Na ndio mana baada ya mapinduzi tu Karume alitangaza kuwa kila aliekuemo ndani ya Zanzibar baada ya mapinduzi basi atakua rasmi ni raia wa Zanzibar, mana karibu asilimia 80% yao hawakua raia halali.
Na ndio mana Wazanzibari wanaamini 1964 hakukufanyika mapinduzi bali yalikua ni mavamizi kutoka Tanganyika ambayo ndio mpaka leo wanaendelea kutawaliwa na Tanganyika.

Sasa hiyo term wazanzibara inamaanisha ni kwa wale wa bara wanaoishi Zanzibar ambao sio wazanzibari ila wanajivisha uzanzibari. (Kwa mfano kama raisi wa sasa baba ake hakuzaliwa Zanzibar na wala yeye hakuzaliwa wala kukulia Zanzibar lakini kapelekwa kawa Raisi Zanzibar) Haimaanishi kuwa kwa kila mwenye asili ya bara nae ni mzanzibara.
Kwahiyo suala la Uzanzibari na Uzanzibara halimanishi kuwa wazanzibari wenye asili ya kiarabu na kiafrica. Ni uzushi unaotengenezwa na serekali ya Tanganyika kuwajaza ujinga raia wao ili wajihalalishie ajenda zao za kuitawala Zanzibar kimabavu. Zanzibar hakujawahi kuwa na Tatizo la Uarabu vs Uafrica, ni propaganda za CCM kwa ajili kijihalalishia kwenye macho ya watu wao wanachokifanya, na ndio mana kila uchaguzi Zanzibar kwa pamoja wote waarabu na waafrica sauti yao hua moja na ndio mana CCM inaishia kutumia mabavu ya kupiga watu na kuuwa ili wachukue serekali kwa nguvu.
 
Naomba msiwaamini watu kama dos.2020 na wenzake wanaotaka kuleta Historia za mapokezano ya waarabu wa Oman waliogawana zanzibar kutokea Muscat Oman.
Hata ukitembelea Makumbusho zote za Zanzibar utapata Historia halisi ya Visiwa hivyo kabla ya Yesu Masihi hajazaliwa wakati Wachina wakiuza shanga zao walifika hapo na kuwakuta Wabantu, ndipo akaja Muajemi
nitaeleza kwa kifupi kutumia link

History of Zanzibar​

Travellers, traders, raiders and colonizers from around the world have been drawn to Zanzibar throughout the centuries, Sumerians, Assyrians, Egyptians, Phoenicians, Indians, Chinese, Malays, Persians, Portuguese, Arabs, Dutch and the British have all set foot on the island's beautiful white beaches, each leaving behind a different legacy. The original inhabitants of the island were the Bantu, who probably migrated from the mainland across an ancient land bridge. The first mention of Zanzibar comes from the Greek mariner's guide
Hivyo Visiwa vilikuwa vikitawaliwa na Mreno, na kwa vile walikuwa na makoloni mengi km Mozambique hawakukitilia maanani kisiwa hicho, ndipo Wabantu wenyewe na wageni wakaenda kumuita Sultani wa Oman atawale hapo penye biashara za pembe za ndovu na utumwa

History of Zanzibar​

Of course, you can go back almost 20,000 years to uncover the full depth of Zanzibar’s history, but it is its role as a major trade port and colonial site that makes it such a fascinating melting pot of cultures and architectural styles.

The island of Unguja was a part of the Portuguese empire from 1503 until 1698, when it fell under the sway of the Omani Sultanate who used the island as a major port for the trade of spices as well as ivory and slaves taken from the mainland.

Tafadhali Kalamu1
na wengine msipokee taarifa na hadithi za mapokeo bila evidence au link
hawa watu hawautaki Muungano na watamsumbua sana Rais Mama Samia na Rais Hussein Mwinyi kwani wanaanzia karne ya 16 hadithi zao kuwa walikuja huku bara wakakuta manyani na wakawakata mikia ndipo wakawapeleka kuwauza huko Bwagamoyo na Unguja
 
Wtf
 
Nakushukuru sana kwa maelezo haya mkuu 'dos.2020; yameongeza ufahamu wangu.

Lakini umemsoma alivyoeleza mkuu Zanzibari Huru' mleta mada hii?

Naona kama kuna tofauti ya maelezo kati yenu. Maelezo yako yanaeleweka, hata kama bado nina maswali kadhaa juu yake.

Labda nikuulize tu kwa haraka haraka, kuna sehemu unaposema:
Ndio mana wazanzibari wa wakati huo hawakuwatambua hawa kama ni wazanzibari wakiamini kuwa ni wageni,
Na kwa kukuthibitishia tu,
"Hawa wazanzibari wa wakati huo ni nani hasa, waarabu?

Kulikuwepo na waafrika waliotambulika kama wazanzibari; kwa maana hata wale wahamiaji wa awamu ya kwanza (watumwa) nao inaonekana uraia wao pia ulikuwa bado ni wa shaka!

Kimsingi, visiwani Zanzibar, enzi hizo za mfalme,kabla ya hiyo awamu ya wahamiaji akina Karume, palikuwepo na raia waliotambulika kuwa ni wazanzibari - ukiwaondoa hata hao watumwa.
Labda nirahisishe hili swali, wakati Sultan anaanza kutawala Zanziba, walikuwepo watu wazawa weusi katika visiwa hivyo?

Tukimaliza hili sasa, tunaweza pia kuuliza maswali juu ya watu ambao asili zao zilikuwa uarabuni. Wote au wengi wao ni wale waliokuja na Sultan na kuweka makazi Zanzibar, na hakuna waarabu wengine waliokuja baadae kweka makazi yao hapo?

Hawa "Wazanzibari" ambao asili yao ni uarabuni, lakini walikuja baadae sana kuweka makazi yao Zanzibar, na wao walihojiwa kwa nini wanakuja kwa wingi kama wale walioanzia safari zao Tanganyika na kwingine barani Africa?

Hawa na wao hadi sasa uraia wao unahojiwa?

Nisiulize maswali mengi sana kiasi cha kuchanganya.

Niseme tu tena, kwamba umeeleza vizuri zaidi kuliko alivyoelezea mleta mada hapa.

Baadae nitakutafuta kwa maswali mengine ya msingi zaidi, pengine nitapata elimu ya kutosha toka kwako.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…