Hivi zile Scania benz za kampuni ya Azam (approximately) zinauzwa shs ngapi?

Hivi zile Scania benz za kampuni ya Azam (approximately) zinauzwa shs ngapi?

Magari sio utajiri,unaifahamu kampuni ya Sumry? Kama ndivyo yule bwana kampuni imebaki jina tuu,yard kuna scrapers zaidi ya 100 zipo juu ya mawe.

Khs huyo jamaa sa SUMRY ni hatari hadi sasa kabakiwa na mkweche mmoja hesabu ya GARI ni laki mbili naikirudi moja kwa moja Gereji kwakweli km unaPESA itie kwenye majengo lkn maGARI daah.....!
 
Mkuu scania benz ndio nini??!!! Scania na benz (mercedes) ni vitu viwili tofauti kabisa mkuu...!!! Au unamaanisha kila lorry ni scania!!??.....yale yale ya nyerere wa kenya anaitwa nani?!)

Unapokuwa unajaribu kufanya utafiti ni lazima ujue kiundani kitu unachokitaka na majina sahihi...hapa JF wengi wao ni vichwa ..utajiaibisha mkuu...kwa mtu mwenye fedha kama hizo unahitaji ushauri na ukaribu na watu wenye uelewa mkubwa wa masuala hayo!
 
Safi kabisa ... niongezee tu bakhressa ananunua gari kabisa , mpya lakini standard version,
Unapotaka kununua malori (tractor units ) kuna vigezo vinazingatiwa ,hasa aina ya matumizi ,uzito utakao beba na njia utakazo pita ukisha jua hilo ndio unakwenda kununua horse kutokana na horse power .
Watu wengi biashara hii inawashinda kwa kuwa wananunua magari bila kudhingatia ugumu au urahisi wa njia au kazi watakazofanya , mf horse power 200-300 hutakiwi kuzidisha tani 18, gari standard kwa sasa ni 400-500hp, ingawa una weza uka opt kwenye extravagants 500-750Hp bands,
Nikirudi kwa mtoa mada ,kusema tu unataka lori kama la bakherssa unakuwa hauko specific ,na nina wasiwasi hata biashara yenyewe hujaijua vizuri, yeye anakwenda njia zozote kwa hiyo ameamua kununua 6x4 hii ni nzito lakini imara ,kwa kulifahamu hiyo anatumia trailer za Serin (Turkey) full air ride . kimsingi lori za bakhresa ni combination ya (horse) tractor unit, nzito na imara6x4 na trailer nyepesi sana ,but a very expensive combo kwa wanaoanza biashara ya lori.
kwa kuwa unaanza ni vema ukatumia 6x2 ambayo kwanza ni rahisi kununua , nyepesi, hivo utabeba mzigo mwingi n.k.. halafu tafuta trailer za imara.


Nakubaliana na mdau kuwa unapotaka kuingia kwenye biashara ya usafirishaji huna budi kufanya utafiti ili ujue ni muundo gani wa lori utakaokufaa. Lengo hapa ni kuweka gharama za uendeshaji chini ili kuzidisha faida.
Unaweza kuwa unapenda sana Scania, kwa mfano, lakini Scania wana idadi kubwa ya modeli na miundo ambavyo vimetengezwa kwa kazi na mahitaji maalum. Msafirishaji ambaye kazi yake ni kusambaza bidhaa mjini anahitaji lori tofauti na yule anayesafirisha bidhaa wa wingi umbali mrefu. Hapa pia kuna masuala kama aina ya barabara na mizigo inayobebwa. Je aina ya lori (tractor) linalohitajika ni 4x2, 6x2 au 6x4 na lenye horsepower ngapi? Na ‘suspension’ inayofaa ni ya upepo au chuma (steel)?
Ni muhimu pia kujua aina ya trela linalofaa. Siku hizi matrela yanayotumika sana ni yenye suspension za upepo na tairi moja moja. Hii kwa kiasi kikubwa inapunguza uzito wa trela, lakini aina hii ya matrela inafaa zaidi kwenye barabara za lami. Aina ya trela pia inategemea na aina ya mizigo inayobebwa.
 
Khs huyo jamaa sa SUMRY ni hatari hadi sasa kabakiwa na mkweche mmoja hesabu ya GARI ni laki mbili naikirudi moja kwa moja Gereji kwakweli km unaPESA itie kwenye majengo lkn maGARI daah.....!

Yah real estates investments ni stress free zone toka enzi.
 
Hakukuwa na sababu ya kumtukana mleta mada kias hicho.
Kukosea si jambo baya

Anatusababishia usumbufu sana kusoma vitu vya giza maana tuko mapumzikomya mwisho wa mwaka tunataka vitu laini visivyo vigumu ku digest
 
Scania mpya inauzwa milioni 200 wazee hazifiki milioni 600...used inategemea na km ilizotembea...ukitaka faw/howo zinacheza kwenye 100-120mil na ukitaka tata zinacheza kwenye 150mil na hapo nazungumzia kichwa tu
Zinaweza fika bei hiyo. Cheki hapa
http://www.trucksales.com.au/buy/new/OAG-AD-675803/2014-Scania-R560
 
Back
Top Bottom